Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Huyu Mzee mwaka 1550 alijiona anachoka sana, Aliangalia chakula anachokula na kukipunguza kufikia 350g na 414 mls za wine kwa siku.
Kwa hesabu za haraka haraka alikula yai moja asubuhi kama kifungua kinywa.
Kipande cha nyama, kuku au samaki saa kumi jioni kikiwa na kiazi na mboga. Ukubwa wa kopo la Coca Cola aliweka wine. Maji ni muhimu hapa kati kati.
Tunakula vyakula vingi tusivyo vihitaji. Wakati wa WWII, wanajeshi wa Magharibi waliotekwa Japan walilishwa kibakuli cha wali na kipande cha nyama kila baada ya masaa 24. Wengi waliishi mpaka kurudi makwao wakiwa wamekonda sana.
Iliwachukua zaidi ya mwezi kuzoea milo mitatu kwa siku.