Kumbe voynich manuscript ilishakuqa decoded

Kumbe voynich manuscript ilishakuqa decoded

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
Kuna kile kitabu ambacho kilikuwa na michoro ya mimea ambayo haifahamiki na haipo dunia hii, pia kilikuwa na michoro ya nyota na sayari pamoja na mambo ya unajimu.
Kilikuwa kimeandikwa kwa lugha ambayo haieleweki wataalamu walihangaika sana kutengua kitendawili cha kitabu hicho wakiwa wanahisi kuna elimu kubwa ya dawa na mambo ya nyota lakini kwa miaka mingi kila aliyejaribu aligonga mwamba.
Kuna familia moja ya Kituruki ya baba mtaalamu wa masuala ya umeme akiwa na watoto wake wawili aliposikia kuhusu hicho kitu na akaona picha zake mtandaoni moja kwa moja akahisi ile ilikuwa lugha ya Kituruki cha kale.
Yeye na watoto wake waliweza kupata copy ya kitabu hicho japo ilikuwa ni lugha ya kituruki ya kale ila pia ilikuwa imeandikwa kwa code.
Waliweza kutengua kitendawili na kutafsiri kile kitabu kumbe hakikuwa na kitu chochote cha maana yani wanasayansi na wataalamu na nadharia zote kumbe zilikuwa bure tu hakuna la maana lilikuwemo japo kitabu kinakisiwa kuandikwa miaka ya 1400-1430
 
Nimesoma makala nyingi sana kuhusu hiki kitabu, ila sijaona mtu alieweza kutoa a plausible anti-code.
 
umenichekesha tu,mwisjo wa kusoma hatipati lolote.
 
umenichekesha tu,mwisjo wa kusoma hatipati lolote.
Mkuu yani walitegemea kuna siri nzito kweli kwenye kitabu hicho nadharia nyingi walikuwa wakiibuka nazo mara ooh kiliandikwa tu hakina maana mara oh kakiandika ronaldo da vinci lakini carbon 14 ikanoyesha kimeandikwa miaka mingi kabla ya kuzaliwa kwake mara oh kakiandika tapeli flan jina nimemsahau aliwahi mtapeli mfalme kwa kumdanganya kuwa anaweza tengeneza dhahabu kwa kuchanganya kemikali na kweli akachanganya akamwonesha kipande cha dhahabu.
Huyo tapeli pia alikuwa anadanganya watu kuwa anajua lugha ya malaika hadi akataka mtapeli mke mwanamahesabu flan kwa kumwambia malaika wamemwagza wabadirishane wake.
Mara oh kiliandikwa na aliens yani assumptions nyingi kumbe kitabu kinaeleza uvunaji uhifadhi wa mazao yani hakuna kitu kikubwa
 
Ni kweli kabisa, wameweza kudecode "voynich manuscript"kwa kutumia " Artificial intelligence"` (AI). Google kuhusu hili upate ukweli huu.
 
Back
Top Bottom