Ni kweli Bunge Hutunga SHERIA na ni kweli Bunge Maalumu la Katiba linatakiwa kutunga Katiba (lakini iliyopendekezwa!).Uhalisia katika mabunge yote mawili ni kuwepo kwa draft/rasimu. Kwa Bunge la kawaida, serikali kupitia wizara ya sheria huandaa Bill ambayo hupelekwa bungeni kwa kujadiliwa, kama bunge litakubaliana nayo huwa ni sheria, ikifanyiwa maboresho mengi basi hurudishwa kwa serikali na ikingangania bunge huvunjwa. Kwa tafsiri hii rasmi ni jambo la kawaida tu kama bill yeyote kwa bunge (tofauti ni kwa kuwa hii ni sheria mama, uandaaji wa bill/rasimu ushirikishe wananchi kupitia kazi ya tume. Haiwezekani kamwe BMK likafanya marekebisho makubwa au kuibadili halafu zoezi likaendelea, itabidi irejeshwe kwa Tume! Tafsiri anayotoa mleta hoja hapa na zile za CCM inadhamiria kubadili rasimu kuwa kitu kingine nje ya maoni ya awali ya wananchi.
Kinachotegemewa na WATU WA AINA YA CCM ni kuburuza ipatikane Katiba na kwenye kura za maoni kazi kubwa iwe ni uchakachuaji. Kinachoogopwa ni kuwa na katiba isiyokidhi mahitaji ya CCM