Kumbe UKAWA walikuwa Wanatupotosha?

Kumbe UKAWA walikuwa Wanatupotosha?

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,976
Eti walidai kuwa Rasimu ilitakiwa "iboreshwe" tu na sio kubadili chochote!
JK amewapatia akina Tundu Lissu na wenzake vifungu kimoja baada ya kingine! Kinachowapa shida sasa hivi UKAWA ni namna ya kufuta uongo wao!
Hongera JK, umekuwa smart sana kuhusu Katiba Mpya so far!
 
Wanasheria wameinisha kwa umakini majukumu na mipaka ya CA. JK ni zaidi ya wanataaluma kweli? Acha upumbavu.
 
Hivi hii ID ilikuwa moderator???!!
Sikuchukii lakini kwa uandishi wako kama ulikuwa mod basi hukutakiwa kuwa!!!! Au umebadilika baada ya kumaliza???!!!

Kwa nini usiandike in a neutral manner wasomaji ndio waseme kama wanapotoshwa au laa???!!!
 
Mkuu,
Tatizo taaluma imeingiliwa na Siasa, akina Tundu Lissu na wenzake wame-fall in love na siasa kwa hiyo wanachakachua vjfungu kwa kwenda mbele!
 
Hivi hii ID ilikuwa moderator???!!
Sikuchukii lakini kwa uandishi wako kama ulikuwa mod basi hukutakiwa kuwa!!!! Au umebadilika baada ya kumaliza???!!!

Kwa nini usiandike in a neutral manner wasomaji ndio waseme kama wanapotoshwa au laa???!!!

Back to topic plse!
 
Nadhani tulichukulie hili jambo kwa uwazi na kwa lengo la kushawishi wengine waone na kukubaliana na hoja zako. Kama mtu huna haja ya majadiliano kaa pembeni na chuki zako. Huna haja ya kupoteza mda kuja kutibuana JF
 
Eti walidai kuwa Rasimu ilitakiwa "iboreshwe" tu na sio kubadili chochote!
JK amewapatia akina Tundu Lissu na wenzake vifungu kimoja baada ya kingine! Kinachowapa shida sasa hivi UKAWA ni namna ya kufuta uongo wao!
Hongera JK, umekuwa smart sana kuhusu Katiba Mpya so far!

kwa mtu kama wewe mlengo wa ccm, japo hujasema, utawapotosha watu kuwa rais kalonga na UKAWA waongo! ccm wana lengo lao kwa maslahi yao, na ukawa ni wakweli, wana lengo kwa maslahi ya nchi! serikali 2 ni zanzibar kuendelea kubebwa na bara na viongozi wasio kubalika bara kuitumia nec ya ccm yenye nusu ya wajumbe toka zenj (na wote wa dini moja) kufanikisha mambo yao kama ilivotokea kumpata mgombea urais 2005! katiba mpya itapitishwa kwa nguvu lakini italeta matatizo makubwa! kumbuka katiba ni makubaliano kati mtawala na mtawaliwa, sasa la ajabu kwa tanzania,mtawala peke yake(kumbuka bunge letu haliisimamii serikali, ni muhuri wake tu!)anakaa kutunga jinsi atakavyo tawala, mtawaliwa kaliona, hamshtuki!
 
Nadhani tulichukulie hili jambo kwa uwazi na kwa lengo la kushawishi wengine waone na kukubaliana na hoja zako. Kama mtu huna haja ya majadiliano kaa pembeni na chuki zako. Huna haja ya kupoteza mda kuja kutibuana JF

What is your point?
 
Kwa MACCM wenye akili fupi na za kushikiwa.

Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla ya kutoa rasimu hiyo.

DKT SALIM AMSHANGAA RAIS KIKWETE | MALUNDE

Wapotoshaji wakubwa hawa!
 
kwa mtu kama wewe mlengo wa ccm, japo hujasema, utawapotosha watu kuwa rais kalonga na UKAWA waongo! ccm wana lengo lao kwa maslahi yao, na ukawa ni wakweli, wana lengo kwa maslahi ya nchi! serikali 2 ni zanzibar kuendelea kubebwa na bara na viongozi wasio kubalika bara kuitumia nec ya ccm yenye nusu ya wajumbe toka zenj (na wote wa dini moja) kufanikisha mambo yao kama ilivotokea kumpata mgombea urais 2005! katiba mpya itapitishwa kwa nguvu lakini italeta matatizo makubwa! kumbuka katiba ni makubaliano kati mtawala na mtawaliwa, sasa la ajabu kwa tanzania,mtawala peke yake(kumbuka bunge letu haliisimamii serikali, ni muhuri wake tu!)anakaa kutunga jinsi atakavyo tawala, mtawaliwa kaliona, hamshtuki!

Mkuu,
Asante kwa maoni yako, mimi nazungumzia UKAWA kutunga Sheria na Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, kisha kwenda "kushtaki kwa wananchi" eti Rasimu inatakiwa "kuboreshwa" tu! Hivi hawa watu walikuwepo kweli Bungeni au walikuwa wanasimuliwa yaliyokuwa yanaendelea Bungeni?
 
naona ccm wanajitahidi kupotosha ukweli ccm hawana nia njema na katiba mpya ukawa ndo wana nia njema wanataka maoni ya wanachi yaheshimiwe kwanza
 
Wanasheria wameinisha kwa umakini majukumu na mipaka ya CA. JK ni zaidi ya wanataaluma kweli? Acha upumbavu.

Ni kweli Bunge Hutunga SHERIA na ni kweli Bunge Maalumu la Katiba linatakiwa kutunga Katiba (lakini iliyopendekezwa!).Uhalisia katika mabunge yote mawili ni kuwepo kwa draft/rasimu. Kwa Bunge la kawaida, serikali kupitia wizara ya sheria huandaa Bill ambayo hupelekwa bungeni kwa kujadiliwa, kama bunge litakubaliana nayo huwa ni sheria, ikifanyiwa maboresho mengi basi hurudishwa kwa serikali na ikingangania bunge huvunjwa. Kwa tafsiri hii rasmi ni jambo la kawaida tu kama bill yeyote kwa bunge (tofauti ni kwa kuwa hii ni sheria mama, uandaaji wa bill/rasimu ushirikishe wananchi kupitia kazi ya tume. Haiwezekani kamwe BMK likafanya marekebisho makubwa au kuibadili halafu zoezi likaendelea, itabidi irejeshwe kwa Tume! Tafsiri anayotoa mleta hoja hapa na zile za CCM inadhamiria kubadili rasimu kuwa kitu kingine nje ya maoni ya awali ya wananchi.

Kinachotegemewa na WATU WA AINA YA CCM ni kuburuza ipatikane Katiba na kwenye kura za maoni kazi kubwa iwe ni uchakachuaji. Kinachoogopwa ni kuwa na katiba isiyokidhi mahitaji ya CCM
 
Hivi hii ID ilikuwa moderator???!!
Sikuchukii lakini kwa uandishi wako kama ulikuwa mod basi hukutakiwa kuwa!!!! Au umebadilika baada ya kumaliza???!!!

Kwa nini usiandike in a neutral manner wasomaji ndio waseme kama wanapotoshwa au laa???!!!

Mod wa namna hii Jf itapotea
 
Kwa MACCM wenye akili fupi na za kushikiwa.

Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla ya kutoa rasimu hiyo.

DKT SALIM AMSHANGAA RAIS KIKWETE | MALUNDE
JK kafafanua hili la kupewa taarifa ya kila kilichokuwa kinaendelea, halina mashiko tena!
Tafuteni singo nyingine!
 
Back
Top Bottom