JiweLinaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,737
- 2,139
who is that??Ongezea mumiani....
who is that??
mid twenties, 23<my age<27Duh! una umri gani we bwana?
mid twenties, 23<my age<27
yeah, you are right, ilikuwa ni mwaka 1988, ilisemekana jamaa alikuwa na nyumba ndogo, sasa mke akamwendea kwa mganga huko Kipalang'anda akapewa dawa aiweke kwenye maji yake ya kuoga ili jamaa akioga tu anamsahau nyumba ndogo na kumpenda mkewe.... sasa kwa mujibu wa uvumi huo, jamaa alipojimwagia yale maji si ndio akageuka nyoka aina ya chatu....
Nilikuwa naishai Buguruni wakati ule maeneo ya Kwa Makukula nyuma ya Kituo cha Polisi cha Buguruni na huo mkasa nilikuwepo mwanzo mwisho ni bahari mbaya tu nilivunjika mkono baada ya kuanguka wakati tukiwakimbia FFU waliokuja kutawanya watu...........
Nakubaliana kabisa na hiyo assessment. Nataka tu kujua nani alifanya huo utafiti kwa sababu kusema ukweli, mtu wala huhitaji kufanya utafiti rasmi kugundua kuwa sisi Watanzania ni watu wa kuamini amini tu bila mpango.
Ila mtambuzi hilo la kunatana ni la kweli kama lilivyowasilishwa that time...source a friend of mine doctor Temeke and another Muhimbili kwani picha nzima iliishia Mhimbili. Na mwanaume alifariki kwa pressure..Sitaki maswali kwani sikuwepo.
Hebu ngoja kwanza...hiyo ya jamaa kugeuka nyoka ilisababishwa na jamaa kutoka na mke wa mtu ama ilisababishwa na dawa ya penzi ambayo mkewe na huyo nyoka mtu alimwekea mumewe kwenye maji ya kuoga ndiyo jamaa akageuka chatu?
Halafu kwa kumbukumbu zangu, hiyo ilitokea miaka ya '87 au '88. Hiyo si miaka michache iliyopita. Ni miaka 26 au 25 iliyopita...hiyo ni miaka mingi.
Nakubaliana kabisa na hiyo assessment. Nataka tu kujua nani alifanya huo utafiti kwa sababu kusema ukweli, mtu wala huhitaji kufanya utafiti rasmi kugundua kuwa sisi Watanzania ni watu wa kuamini amini tu bila mpango.
halafu magazeti ya GP yakaandika front page bila aibu, nilichefuliwa kweli bcoz it took me 2min to prove the story is fake -_- wakati GP wanadai alitokea kidume wa kumtoa 'bikra' ptuuu. do you remember the 'giant snake in the dead sea' story iliyowekwa JF na ikatokea GP later that week?! i wish ningeweza ku-perform so poorly kazini kwetu kama wahariri wa GPMike Tyson story ?lol