Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Hapo jana tumeshuhudia shirikisho la kandanda nchini kwetu likifanya uchaguzi wake huko mjini Dodoma na kupata viongozi wapya wataoliongoza shirikisho hilo la mpira wa miguu kwa kipindi kijacho.
Katika uchaguzi huo aliyeshinda nafasi ya Urais wa shirikisho hilo ni Wallace Karia na aliyeshinda nafasi ya Umakamu wa Rais ni Michael Wambura.
Kabla ya kufanyika uchaguzi huo kulikuwa na kila aina ya mizengwe, kama vile kuweka zuio mahakamani ili uchaguzi huo usifanyike, mizengwe mingine ni kumuwekea pingamizi mgombea wa nafasi ya Urais Wallace Karia kuwa siyo raia wa Tanzania.
Hatimaye Mahakama ilitupilia mbali mapingamizi hayo na kusema kuwa Wallace Maria ni raia halali wa nchi hii na uchaguzi uendelee kama ulivyopangwa na hapo jana ukafanyika na Wallace Karia akaibuka na ushindi wa kishindo kwa nafasi ya Urais.
Tukumbuke pia katika uchaguzi wa jana TAKUKURU walitanda katika kila kona ya Hoteli zote walizofikia wajumbe hao kuhakikisha hakuna rushwa yoyote inayotembezwa kwa wajumbe wa mkutano huo.
Ingawa TFF ni shirikisho la kandanda Tanzania na CCM ni chama cha siasa, lakini vyama hivyo viwili vinafanana sana kwa matendo yao.
Tunaijua CCM kuwa ni mabingwa wa kuendesha siasa za mizengwe za kuwasingizia baadhi ya wagombea ambao wanawaona tishio kwa kuwaita siyo raia na katika chaguzi zao zote rushwa huwa inatembea nje nje, jambo ambalo huwa linassbabisha wagombea ambao huwa wanapata uongozi siyo wale viongozi bora ambao wangepaswa kupita kwenye nafasi hizo, Bali huwa inatokana na ubora wa kutengeneza mizengwe na ubora wa kutembeza pesa ya rushwa kwa wagombea wa chama chao.
Kitu ambacho tumejifunza kutokana na uchaguzi wa jana wa TFF ni kuwa kumbe hata katika uchaguzi mkuu wa vyama vya siasa,iwapo TAKUKURU na vyombo vya dola vitaamua kufanya shughuli zao kwa weledi kutokana na taaluma yao, ni dhahiri kuwa vyama vya upinzani vitapata ushindi wa kishindo dhidi ya CCM!