Cynic,Wiki chache zilizopita nilitakiwa nitoe taarifa wazazi wangu walizaliwa lini na wapi. Nikataja mwaka na kwamba walizaliwa Tanzania. Jamaa akaniuliza nina uhakika mara tatu na mimi kwa kujiamini nikamwambia ndiyo. Baada ya muda akaniambia haiwezekani! Nikamwambia labda kwenye database yake itakuwa imeandikwa United Republik of Tanzania,
Akaniambia pia haiwezekani. Ndipo akaniuliza nchi yenu haijawahi kubadili jina? Ndipo akili zikanijia na kumwambia kwamba ilikuwa inaitwa Tanganyika. Ndipo system yake ikakubali, na copy ya printout kuonyesha walizaliwa Tanganyika.
Nilichojifunza hapa ni kwamba kumbe Tanganyika ipo na kumbe wengine bado wanaitambua. Na waTZ mliozaliwa kabla ya muungano msijisahau -
hamkuzaliwa Tanzania
Hili jina Tanganyika hata mie huwa napata shida kuelewa ni wakati gani linakuwepo na wakati gani Tanganyika haipo.
Ukiangalia kwa mfano Chama cha wanasheria huitwa Tanganyika Law Society na siyo Tanzania.Hebu tuchanganue ni wapi Tanganyika ina apply..na ni wapi haipo.Kulikwa pia na Tanganyika Packers japo imekufa miaka ya mwanzo ya 80.
Wiki chache zilizopita nilitakiwa nitoe taarifa wazazi wangu walizaliwa lini na wapi. Nikataja mwaka na kwamba walizaliwa Tanzania. Jamaa akaniuliza nina uhakika mara tatu na mimi kwa kujiamini nikamwambia ndiyo. Baada ya muda akaniambia haiwezekani! Nikamwambia labda kwenye database yake itakuwa imeandikwa United Republik of Tanzania,
Akaniambia pia haiwezekani. Ndipo akaniuliza nchi yenu haijawahi kubadili jina? Ndipo akili zikanijia na kumwambia kwamba ilikuwa inaitwa Tanganyika. Ndipo system yake ikakubali, na copy ya printout kuonyesha walizaliwa Tanganyika.
Nilichojifunza hapa ni kwamba kumbe Tanganyika ipo na kumbe wengine bado wanaitambua. Na waTZ mliozaliwa kabla ya muungano msijisahau - hamkuzaliwa Tanzania
kwa tarifa yako Tanganyika ipo na itaendelea kuwepo,na kwa wale wasioipenda Tanganyika Mungu awataremshie lana katika maisha yao.
Hili jina Tanganyika hata mie huwa napata shida kuelewa ni wakati gani linakuwepo na wakati gani Tanganyika haipo.
Ukiangalia kwa mfano Chama cha wanasheria huitwa Tanganyika Law Society na siyo Tanzania.Hebu tuchanganue ni wapi Tanganyika ina apply..na ni wapi haipo.Kulikwa pia na Tanganyika Packers japo imekufa miaka ya mwanzo ya 80.
Cynic,
Ni kweli TANGANYIKA ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo na Muda si mrefu toka sasa Jinamizi lake liotaibuka kudai nafasi yake. Narudia Muda si mrefu toka sasa.................
duh nitafurahi ikiwa itarudi tunamuomba mungu irudi kama leo na kesho na sio kufichwa inajulikana kuwa tanganyika ipo na serekali yake ipo sasa hii ni kuonyesha kuwa mnawakandamiza wazenji tu
Ngoja nikuongezee na nyingine:
1. Medical Council of Tanganyika ( sijui madaktari wa Zanzibar kama wana yakwao tofauti na hii au hii ndio yenye kushughulikia kote)
2. Tanganyika Farmers' Association
Naona Wakuu mnajidanganya wote nyinyi jina la (Tanganyika) litabaki lakini halitatumika kama mnavyotaka nyinyi lakini suala la Muungano upo bado pale pale na hiyo Tanganyika imekufa kama zamani alivyo kufa Baba Wa Taifa Mwalim Nyerere na Mzee Abeid amani Karume ikiwa hao watafufuka na hiyo Tanganyika itafufuka na Unguja pia itafufuka lakini kama hawatafufuka mpaka siku ya hukumu yaani kiama basi hiyo Tanganyika na Unguja hayo majina hayatarudi kama zamani hizo ndio ndoto za Sakafuni.......................Asanteni sana
WANAOTAKA KUUVUNJA MUUNGANO BASI HAO NDIO NI MAFISADI.
WANAOTAKA KUUVUNJA MUUNGANO BASI HAO NDIO NI MAFISADI.
SWALI: Hivi timu ya taifa ya Zanzibar inapocheza mpira dhidi ya timu ya taifa ya bara kwenye Challenge inakuwa ni Zanzibar dhini ya Tanzania au Tanganyika? Mimi nadhani ni Zanzibar dhidi ya Tanganyika ila hawataki hilo jina litamkwe. Lakini nchi ipo.Tanganyika ipo, kuna ziwa, kuna wilaya huko DRC.
Ila nchi iliuawa katika muungano na Zanzibar katika mazingira ya kutatanisha na hesabu mpya za federation ambazo hazijawahi kuonekana tena dunia nzima.