Kumbe TANESCO wanatoa rushwa kwa wabunge!?

Kumbe TANESCO wanatoa rushwa kwa wabunge!?

Babu Lao

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
2,042
Reaction score
180
:A S-alert1:
January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.

“Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch’ ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge,” alisema January.
:sad:
 
"Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch' ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge," alisema January.
:sad:
Tatizo wakichukua hukaa kimya hivyo siyo rahisi kujua nani mkweli, January atakapoanza ziara tutarajie Wakuu wengi wa mashirika kuwekwa mikononi mwa Takukuru sababu ya kujaribu kuwapa bahasha za kuwaziba midomo wahe. , hapo ndo tutajua kweli kaamua kupambana.
 
makambaaaa endelea mkuuu I hope ni uwezo wako na si nguvu za baba yako zimekufikisha huko! ENDELEA MAKAMBA :clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
Big up makamba,vijana tunatakiwa kulifia taifa letu tuache unafiki unaoangamiza taifa,ukiona ya tanesco pia sehemu zote zinafanya hivyo,sasa sijui kama wengine watakuwa na mshipa wa kuzikataa.cha kushangaza ni kwa nini wapokee wakati bunge linagharamia,kichwa kinaniuma kwelikweli.Inabidi hili likemewe na Mh.Anne semamba Makinda.ukali wako mama naupa :A S thumbs_up: sasa hamishia kwenye hayo maujinga aliokuonyesha makamba J.
 
Anyway, ngoja tuweke siasa pembeni tumpe support, maana ni kwa maslahi ya umma.

Big up, Ila isiwe nguvu ya soda.
 
Na hii inavoonekana ni kwa kamati zote... Mnakumbuka ugomvi wa Dk. Mwakyembe na Dk. Hosea... wakati Hosea alipotaka kuwahoji wabunge kuhusu kuchukua posho mara mbili, sasa ndio imejulikana mpaka kiasi walichokuwa wanachukua:coffee:!!!!
 
haya tune kama hii siyo nguvu ya soda...
 
dah! Sarakasi za chama tawala bwana!
Don't you smell something buddies?..... Mi hawajanipata bado!
 
haya tune kama hii siyo nguvu ya soda...

Linapofanyika jambo zuri jamani tupongeze kwani kila mara lazima tuwe na tuwe na mtizamo hasi tu? Mimi nampongeza sana Makamba na wanakamati kwa kugome hayo malipo na nimesiki kuna waraka wa spika wa kukataza malipo mara mbili wakati wameshalipiwa na Bunge halafu lunch gani hiyo ya Milioni Moja kama si Rushwa?
 
Ni mapema mno kuanza kujudge,let us sit and wait,only time will tell
 
Hapa tunaweza kuwa tunahesabu vifaranga kwenye yai viza, bado mapema sana kujua dhamira yake January Makamba
 
:A S-alert1:
January alisema baada ya kupitia taarifa zilizopita za kamati hiyo, aligundua kuwepo kwa bahasha za mlo wa mchana kwa kila mjumbe wa kamati ambazo ndani yake kunakuwa na shilingi milioni moja hivyo aliwaomba wajumbe wa kamati yake kuzikataa.

“Baada ya kupitia taarifa zile tumeona kuwa wajumbe wa kamati walikuwa wakienda kwenye ziara kama hivyo hupewa bahasha za ‘lunch’ ambazo ndani yake kunakuwa na sh milioni moja sasa nimewaomba wajumbe wenzangu tusizikubali… safari hii tutagharamiwa na Ofisi ya Bunge,” alisema January.
:sad:

Wana JF tuwe makini sana na michango yetu. Kamati hizi za bunge zimeundwa kimkakati zaidi wa kuwasafisha mafisadi. Kama mnakumbuka ni taarifa ya kamati gani vile iliyolazimisha mafisadi kujiuzulu?, Fikiria mara mbilimbili. Kwa nini January mtoto wa Makamba asitetee kundi lililompatia ubunge?, linalimlindia baba yake ulaji?. Haya ni matope wanayotaka kupakwa kina Dr Mwakyembe et al. Kuwa wao si lolote bali walikuwa wanachukua mshiko wa TANESCO. Kama ni kweli basi TANESCO itakuwa ilitumia mamilioni kuihonga kamati na hivyo sasa tuhitaji watueleze kuwa hela hizo zilikuwa zinatoka wapi? wakati gharama za uendeshaji zimepanda?
 
Pata picha mheshimiwa unaamka asubuhi na hangover huna hili wala lile, unaelekea zako mjengoni, unatumia muda wote wa asubuhi (wakati wa maswali na majibu) umepiga usingizi, ghafla unadondoshewa bahasha ndani kuna millioni moja...! inahitaji uzalendo wa kifisadi kuziacha hizo!
 
Si vibaya kumpa Mh. January Makamba imani lau ya muda (benefit of doubt) kwa mwenendo aliouonyesha hadi sasa katika majukumu yake. Ila ajue kabisa kwamba jukwaa analotumia (CCM) hivi sasa limepoteza kabisa matumaini na imani ya wananchi na usanii si kitu kinachoweza kumjenga mtu nyakati hizi. Hivyo, ni yule tu anayeonyesha mkakati wa dhati na endelevu wa kupindua status quo inayosimamiwa na chama tawala, ndiye, hatimaye, atakayeweza kukubalika na watanzania wa leo. Faida aliyo nayo ni kuwa ameidhihirisha kuwa mtu aliyeelimika na mwenye uwezo wa kuelewa na kuchambua mambo. Mzigo alio nao ni kule kuwa mtoto wa kiongozi wa ngazi ya juu wa CCM asiye na mvuto na ambaye heshima yake imeshuka sana kwa watanzania wenye kutaka mabadiliko na maendeleo ya kweli. Hapo ni lazima ajiulize kikamilifu kuwa yuko upande upi na anasimamia kitu gani hasa.
 
yes I do agree with you! Huu mchezo uko kamati zote hata hizo walizo akina Zitto na Cheyo.
Ukweli utajulikana tu.
ngoja tusubiri
Na hii inavoonekana ni kwa kamati zote... Mnakumbuka ugomvi wa Dk. Mwakyembe na Dk. Hosea... wakati Hosea alipotaka kuwahoji wabunge kuhusu kuchukua posho mara mbili, sasa ndio imejulikana mpaka kiasi walichokuwa wanachukua:coffee:!!!!
 
Lets give it time. The move is good and that how it is supposed to be but the customs of the MPs is to receive more! There are still MPs who are running offices and they are under pay roll of other companies/organisations though they are receiving salaries from the parliament. These are also corrupt and they infact "wahujumi uchumi". Here comes a time when a spade is called a spade. I do agree with Makamba vision if he will religiusly exeute it b/se life is constantly changing and hence the vision will also be changing.
We need people who can address the pertinent issues, our issues is not about the bahasha so long they are appropriately approved and is not intended to grease the MPs. We need them to shout to the executives on performance and have clear Key Performance Indicators in place well agreed in advance to avoid subjectivity which is the main tool used by politicians!!!!!
 
Ataaminika zaidi pale atakapokamatwa mmoja wao kwa maneno ndugu zangu january ni kama february nae n binadamu lolote latokea na wakipewa wako wenyewe sirini utojua lolote nahsi kazi yake ya kwanza angefwatilia huko tanesco nani anasaini vocha za hizo pesa na kumfikisha takukuru si kwa maneno..si ana makabrasha na waliochukua..watoe ushahdi na si tanesco we mnakwenda shirika kama atcl linapumulia icu unakomba million moja moja si unatafuta mauti ya wazi wazi jamani...je nani atamfwata january??
 
dah! Sarakasi za chama tawala bwana!
Don't you smell something buddies?..... Mi hawajanipata bado!
Yes I can smell something fishy, Mr. J. Makamba is trying at all cost to discredit the previous members of the committee , that incl. Dr. Mwakyembe ( I stand to be corrected) , note that it is the previous members that never honoured the request to purchase Dowans generators . Hope he is not palying as an agent of RA
 
Tatizo wakichukua hukaa kimya hivyo siyo rahisi kujua nani mkweli, January atakapoanza ziara tutarajie Wakuu wengi wa mashirika kuwekwa mikononi mwa Takukuru sababu ya kujaribu kuwapa bahasha za kuwaziba midomo wahe. , hapo ndo tutajua kweli kaamua kupambana.

Tuache kumpamba! Huyu kaja kisasi chake kwa vile anajua mwenyekiti aliyemtangulia aalikuuwa mzee Shellukindo na wajumbe walipoita ndiyo waliomjeruhi bosi na mungu wao wa pesa. Kama yeye ni msafi amehonga milioni moja kila mjumbe ili aupate uenyekiti ili apate nini? Hela hizi atazirejeshaje na kule kuna biashara gani? Asituzuge hapa!
 
Back
Top Bottom