Kumbe simu feki zilizofungiwa zinaweza kurudi mtandaoni

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
8,807
17,141
Wakati wabongo wengi simu zao za kichini zilizo na IMEI zikifungiwa zikiwemo smart phone zenye gharama kubwa.Imebainika kwamba zinaweza kupandikizwa IMEI halisi na kusajiliwa upya mitandaoni kwa kutumia program maalum inayobadili IMEI na kupewa IMEI namba halali itakayosajiliwa na mtandao husika (Genuine IMEI Implant Program).Program kama hiyo ilianzishwa India miaka ya 2009 wakati nao walipoanza kudili na simu feki.India waliweka program hiyo kwa kuzingatia haki za binadamu kwani waligundua kwamba watumiaji walinunua simu hizo bila ya kufahamu au kujua.Hivi sasa kuna simu zenye thamani ya mabilioni ambazo zimeshafungiwa hapa tz na zimebaki screpa tu.TCRA inabidi waingize hiyo program ili serikali iwanusuru wananchi wake na wakati huohuo ionekane inazingatia haki za wananchi wake.

Angalia hapa:How to Get a Valid IMEI Number For Mobile Phones in India
 
sijui sheria gani ila cha msingi sheria si msahafu inaweza badilika
Mkuu kama unakumbuka vizuri hata kuflash simu ni kosa tena ukikamatwa ni hatari kwa maisha yako sembuse kuapply hiyo programm! Chonde chonde usijaribu kabisa wala kumshauri ndugu au rafiki yako.
 
Suala halikuwa simu kutokuwa na IMEI bali ubora wa simu feki hauamini, ndo maana zikapigwa marufuku kutumika ili kulinda afya ya mtumiaji,

Sasa kama mtumuaji ataforge IMEI siatakuwa anajidanganya mwenyewe wakati athari za simu bado anaendelea kuzipata
 
Nadhani hapa hatujaelewana, hiyo program nayozungumza hapa si software au program ya kompyuta bali ni zoezi maalum/au mradi maalum ambao serikali kwa kushirikiana na makampuni ya simu ndio wanafanya zoezi hili la usajili kwa watumiaji wa simu feki ambapo wao wanaposajili simu feki hutoa IMEi namba kwa hiyo simu ambapo inatambulika na inakuwa halali.Kuhusu ubora wa simu sio kweli.Simu hizo zina viwango kama simu nyingine na material ni yaleyale kinachofanyika ni kutumia majina ya simu nyingine(brand) ili kupata soko.Sababu kubwa ambayo serikali haijaibainisha ni suala la usalama na uhalifu kwani simu zenye IMEI feki ni shida ku-trace inapotumika kwa uhalifu na makosa ya kimtandao
 
Back
Top Bottom