Kumbe Serikali ina Pesa Nyingi eee

Kumbe Serikali ina Pesa Nyingi eee

Makachu

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
449
Reaction score
465
Habari JF Members, nadhani wote ni wazima. Naomba niende kwenye Mada moja kwa moja

Kumbe Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina Pesa nyingi sana kiasi cha kwamba waliamua kusamehe deni la Tsh Trilioni 360 za MAKINIKIA na kukubali kulipwa Tsh Bilioni 900.

Sasa Je, Serikali kama iliweza kuacha fedha zote hizo, kwanini leo hii bado wanamg'angania kutukamua kwenye TOZO?

Unasamehe Matrillion ya Makinikia(BARRICK) alafu unakuja kutukata sisi Watanzania TOZO tena bila huruma. Kwahiyo Makampuni ya Kizungu ndio ya kuonewa huruma na kusamehewa kuliko sisi Watanzania?

Ushauri wangu kwa Serikali, iziondoe Tozo kwa Maana hazitunufaishi Watanzania Directly.
Nawasilisha
 
Mungu tusaidie tupate viongozi wanaotumia akili zao vizuri 2025

🙏🙏🙏
 
background-banner-colors-country-wallpaper-preview.jpg

Tundu Lissu
 
Back
Top Bottom