Kumbe purukushani za kujitawala ilikuwa ili tuwe vibaraka wa Wachina?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Kumbe purukushani zote za kujitawala lengo lilikuwa tuliusaka uhuru ili kuwa vibaraka wa wachina.

Hawana Facebook, Whatsup na Google basi hiyo ni sababu tosha ya kuwaiga

Hawana mfumo wa vyama vingi basi nasi ni kuigaiga tu huku tukidai kuhamia Dodoma ni kumuenzi "baba wa taifa" aliyeshauri kurejeshwa mfumo wa vyama vingi!

Wanapiga risasi watuhumiwa wa ufisadi basi nasi risasi kona kwa kona maana hata wachina wanapiga risasi.

Wanaikopesha serikali ya marekani basi nasi tuanze kuikopesha

Wachafuzi wakuu wa mazingira basi nasi kiguu kwa njia

Wamefuta ukomo wa Urais basi nasi ni copycats hatuna historia na urithi wowote hivyo ni kufuta ukomo wa Urais ili mmoja wetu na ndugu zake na wapambe zake waendelee kula na kusaza sis tuokote makombo yao tu kwani Mchina ndiye Mungu wetu na anapaswa kuabudiwa.

Wana chama chao tawala basi tufute vyama vyote vya siasa na kuwapigia magoti chama chao cha kikomunisti jina tu kishike "utamu" wa uongozi! Sijui ccm sijui cuf sijui wanamagwanda ni kuvifuta kwa kubadili katiba na sheria na kukitangaza chama tawala cha uchina ndicho pekee tawala hapa nchini!

Tusikomee hapo:-

Wanatawaliwa na wachina wenzao basi watumishi wote wa umma wajiuzulu kuanzia siku internet itazimwa na kuwakabidhi serikali wachina. Rais na baraza la mawaziri wachina, wakuu wa mikoa na wilaya wawe wachina, wabunge na madiwani wawe wachina. Tusiishie hapo tuendelee kutimua raia wote kwenye utumishi wa umma na kuwakabidhi wachina inji hii ya wagagagigikoko!

Kweli Akutukanaye hakuchagulii tusi.

Nionavyo

Ukiona kiongozi wa umma anachukia uwazi na hataki kuwajibika kwa umma JIULIZE haya ayafanyayo ni KWA MANUFAA YA NANI?
 
kuondoa ukomo ndio target yake
sijui kwa nini jamaa ni mroho wa madaraka kiasi hiki!!!
oh,nimekumbuka...1.5 is sweet
 
Kama kweli wanataka tuwaige Wachina; binafsi sina tatizo ili mradi tu tusiwaige nusu nusu!

Nitakuwa tayari kui-support serikali yangu ikiwa pia watawaiga Wachina nini wanafanya kwa viongozi na watendaji mafisadi!
Yote wataiga lakini sio hili. Wangefanya hivyo sijui ni wangapi tungekua nao, kuna ambao wasingetinga kule tunakoweka magogo na wengine wasingetoka salama achilia mbali vifisadi vidogo dogo. Rejea EPA, ESCROW, NYUMBA, KIWIRA, etc mlolongo usio isha.
 
kuondoa ukomo ndio target yake
sijui kwa nini jamaa ni mroho wa madaraka kiasi hiki!!!
oh,nimekumbuka...1.5 is sweet
One of the targets not the only one, my bro! Kuongeza urefu wa vipindi kutoka tano kuwa saba. Kufuta mfumo wa vyama vingi, kuimarisha sheria ya kuweka wapinzani wake kizuizini, chama kushika hatamu na kufuta uwajibikaji bungeni ni baadhi ya mikakati
 
Yote wataiga lakini sio hili. Wangefanya hivyo sijui ni wangapi tungekua nao, kuna ambao wasingetinga kule tunakoweka magogo na wengine wasingetoka salama achilia mbali vifisadi vidogo dogo. Rejea EPA, ESCROW, NYUMBA, KIWIRA, etc mlolongo usio isha.
Wanachagua ya kuiga. Yanawajenga no mbele mbele kwa mbele mbele yanayowadhoofisha ni vipofu wa khiari
 
One of the targets not the only one, my bro! Kuongeza urefu wa vipindi kutoka tano kuwa saba. Kufuta mfumo wa vyama vingi, kuimarisha sheria ya kuweka wapinzani wake kizuizini, chama kushika hatamu na kufuta uwajibikaji bungeni ni baadhi ya mikakati
Haitashangaza. Wakati wa kampeni nafikiri akiwa Tanga aliyasema haya. Anataka Chama kimoja na kuwa CCM ina uwezo wa kujibadilisha na kuwa bora kama ilivyo China! Hatufuatilii tu na kutunza kumbukumbu. But it will be the worst mistakes the country has ever done if we take that route.
 
Back
Top Bottom