Kumbe Nchi Iko Vitani na Al-Shabaab | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Nchi Iko Vitani na Al-Shabaab

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by dudus, Oct 29, 2011.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,097
  Trophy Points: 280
  Akihojiwa na the Daily Nation, Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono hatua za kijeshi za Kenya huko Somalia ili kujilinda dhidi ya Al-Shabaab. Source: JF twitter.

  Hii maana yake unapomuunga mkono adui wa rafiki yako maana yake automatically unakuwa adui wa adui wa rafiki yako pia. Hivyo, kwa maana nyingine indirectly tumetangaza vita na Al-Shabaab.

  Pengne pia kauli hii ya Rais imekuja ili ku-support kauli ya Kova kuhusu kufuta maandamano yaliyokuwa yafanyike kupinga kulipwa DOWANS. Anyway, mbinu za kisiasa ni nyingi.
   
 2. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  pilipili usiyoitafuna yakuwashia nini?!! kauli zingine tuziangalie la sivyo zitatuweka matatani.
   
 3. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kituko cha aina yake yaani Watanzania wanatishwa na Al Shabaaby na serikali inakubali? Kwa maana nyingine ni kwamba Serikali ya Tanzania ilikubaliana na serikali ya Kenya wapeleke majeshi huko Somalia.

  Lengo hapa ni kuwapa furusu Al shabaab kuingia nchini tena wanaweza kusaidiwa na serikali ili kuwatisha Watanzania. Hii ni nini maana yake, ni kuwa Serikali ya Tanzania inajua mahali na sehemu ambapo imewahifadhi Al Shabaaby hapa nchini. Serikali itakuwa tayari kuwasaidia Al shaababy kutekeleza mashambulizi yao.

  Watanzania kuweni macho, CCM ni Al Shaababy ya Tanzania. Ukweli unajieleza wenyewe kuhusu viongozi wa Serikali kukumbatia makundi ya kihalifu ili kubaka demokrasia nchini.

  Hii ni hatari sana.
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hapa ndipo Dr. amefikia, ndo uwezo wake jamani wa kujibu maswali, hivi kuna la kushangaa kwenye matamshi ya JK!!!
   
 5. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Mbona hakutoa msimamo wetu wakati wa kumng'oa Gaddafi.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,845
  Trophy Points: 280
  Amefanya mistake kubwa sana...al shabaab waachie wakenya wenyewe
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ana kiherehere sana
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Mbona nasikia Waingereza wanatutuhumu kuwa tuna wahost Al Shabbab?
   
 9. Z

  Zenji Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo ndo ya kujipendekeza kwa watu, kama kweli unasapoti si na wewe upeleke wanajeshi au .....?

  Magamba wanataka kututoa ktk mode ili walipe DOWANS.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wewe vipi, kwa hiyo ulitaka rais aunge mkono Al-shaabab? Jamani, mambo gani haya. Ushabiki gani huu. Tanzania tujihadhari na watu wa aina hii ambao hawana uzalendo. Sote tuunge mkono kauli hiyo ya Rais. wote tuwe walinzi popote pale tunapotembea. Inawezekana kabisa Al-Shaabab wakawa na vibaraka nchini, wote hao tuwaumbue, tuwe kitu kimoja katika hili bila kujali tofauti zetu za kichama, kidini na hata kijamii
  Tukumbuke wanaoathirika sana na matukio haya ni wazee, watoto, walemavu na wanawake. Tusifike huko. Aidha ni lazima tuwekane wazi kwamba GAIDI hachagui wewe ni adui yake au la, lengo lake ni kutimiza azma yao popote pale. JK tunaungana na wewe kulinda nchi yetu kwa gharama yoyote.
  Mungu Ibariki Tanzania, tuepushe na wenye wivu na amani yetu
   
 11. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na inaashiria "Intelijensia" ya Kova inasema al shababy wapo hapa Dar na nimemsikia Manumba DCI akizungumza na BBC kuwa "ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji" sijui alimaanisha Kenya au Libya
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  chanzo gani hizo?. Tuache mambo ya kughushi yahana maana yoyote kwetu. Tuunge mkono juhudi zozote zitakazoiweka nchi yetu katika amani na siyo ushabiki wa kisiasa, katika hili siasa hazina nafasi
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  unafikiria kimasaburi saburi type...
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Jamani mimi binafsi nikisikia tu habari za Al-shabaab naweweseka. Hili suala si la kutolea tamko. Wakisikia tuwabebea mbeleko gani hawa. Tungewaacha wapigwe kimya kimya na hao Wakenya na Wamarekani kama tulivyo kaa kimya wakati Gaddafi anapigwa. Afadhali tungesema wakati wa Gaddaffi.
   
 15. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 280
  kuna kipindi alikuja Rais wa Somali..pengine ana msupport mwenzake...
   
 16. jockey emmanuel

  jockey emmanuel JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 330
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali ya somalia imewashindwa hao so-called al-shabaaby sijui,watz na shida zote tulizonazo bado tunawatafuta,tukilipuliwa ndo tutaelewa somo eeh?...kusema rahisi kweli,...wahenga wanasema 'kupanda mchongoma,kushuka ndio ngoma'...tunajaribu kuupanda huo mchongoma,tutaweza kushuka kweli?...
   
 17. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Na wewe nawe akili yako imekupeleka huko kumuunga mkono raisi kwamba Alshabaab ni tishio kwa Tanzania pia.
  Hawa Alshabaab wana jeshi na silaha kiasi gani kiasi kwamba Ethiopia,Kenya,Uganga,Burundi na sasa Tanzania wako vitani nao.
  Nyinyii! wacheni fitna na chokochoko mchokoe pweza binadamu atakushinda.
  Umesema wanaoathirika ni wanawake,watoto na walemavu na wazee.Hizi ni lugha za kisiasa na za kipropaganda.Huko Kenya na mabwana zake wanakopiga mabomu kwani ni nani wengine wasioathirika na mabomu yao muda huu.Au ubaya ni kuathirika makundi hayo ya kitanzania pekee.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Amekuja mara mbili. Kuna wakati alipewa msaada wa mahindi!
   
 19. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Raisi gani huyo mbona sina kumbukumbu.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,573
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaona mbali!

  I was thinking the same.Wanasema "kihere here" na mambo mengine,lakini hawajui wameingizwa mkenge.

  Hakuna kitu serikali inachopenda kama kuwaingiza hofu wananchi.Watatumia tactic ambayo nchi kama marekani walishawahi kulaumiwa nayo...Ya "fear mongering"

  Especially walipokuwa wakiambiwa kuwa wanatumia issue ya Alkaeda kuwasahaulisha wananchi kuhusu domestic issues kama economy etc.

  Sitashangazwa mafisadi wakiiga sepecially this time ambapo inaonekana serikali yao ina collapse na uchumi ukielekea kaburini.

  Umeme hamna,mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilling si jambo la kubeza kwa serikali yoyote iliyopo madarakani.

  Tena wakizidiwa wanaweza kupandikizaa shambulizi wao wenyewe,same thing kama wanavyolaumiwa wengine kuhusu kupandikiza mashambulizi.

  Hawa mafisadi siwaamini kabisa , wanaweza kufanya lolote ili tu waendelee kubaki madarakani kwasababu wanajuwa mwisho wao hautakuwa mzuri endapo watakuwa hawana grip on power.
   
Loading...