G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,592
- 36,008
Wa Afirka tunachukiana mno kisiasa, tunabaguana sisi kwa sisi kusiko kawaida kutokana na maslahi ya kisiasa!
Ikiwa tutaachwa kujitawala wenyewe, kuna hatari kubwa sana ya kuteka haki, wanyonge watanyanyasika kusiko kawaida! Vyama dola vitayateka mataifa mengi na kujitwalia ufalme!
Ikiwa bado hatutaweza kujiongoza wenyewe, kwa hakika hatutaweza kuongoza wenzetu wa mataifa ya mbali!
Kwa hakika tunahitaji kuongozwa zaidi na wenzetu kuliko hata ilivyo sasa! Kwa maana hiyo basi Robert Mugabe ametetea udhaifu wake, amejitahidi kuhalalisha dhuluma yake ya kuibaka demokrasia nyuma ya pazia la kuutetea u Afrika! Bado tunahitaji kuongezewa usimamizi mara dufu zaidi!
Hapo nimejibu hotuba aliyotoa leo rais wa Zimbabwe Robert Mugabe!
Twende kwenye mada husika!
Ndugu Nape Nnauye ambaye amepewa uwaziri wa kusimamia vyombo vyote vya habari, sasa amehisi kuwa amejitwalia ufalme! Amejitakasa kwa kutoa maamuzi ya ajabu ikiwa ni matokeo ya kujikweza ili kuthibitisha kuwa sasa ni mfalme wa vyombo vya habari nchini!
Miaka michache iliyopita, Nape alitamani sana bunge lisionyeshwe live! Kwa hakika amekidhi matumaini yake hayo! Alisikika mara kwa mara akikemea tabia ya bunge kuonyeshwa live! Nyuma ya pazia alijua alichokisimamia, anajua anachokisimamia!
Ni mpuuzi pekee atakayeangalia chombo kinachoitwa huru kikionyesha habari zake zilizohaririwa! Nape ameanza na chombo cha umma kwa kuwa ana mkono wa moja kwa moja ndani ya chombo hicho! Baadaye atavigeukia vyombo binafsi! Anatamani kuyaishi matamanio yake/anatamani kukidhi haja yake kwa vitendo!