Kumbe na mkataba walishasign! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe na mkataba walishasign!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Njowepo, Jul 31, 2011.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkataba mwingine kama wa Dowans huu hapa!
  Na Gerald Kitabu
  31st July 2011
  Ni ule mwekezaji aliyepewa ardhi kwa miaka 99
  Kodi ya ardhi sh. 200, Halmashauri kupata sh.500


  Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo (kulia) akiwa na viongozi wa serikali ya mtaa na wanakijiji cha Kambuzi Halt, Katumba, wilaya ya Mpanda, wakilalamika kwa watafiti wa Shirika la Haki Ardhi na waandishi wa habari.
  Wananchi, watendaji wa vijiji na Madiwani wa kata za Litapunga na Mishamo Wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, wamepinga yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Mishamo na Katumba, kukodishwa kwa mwekezaji ambaye ni kampuni ya Agriosol ya Marekani, kwa maelezo kwamba uwekezaji huo, hautakuwa na tija kwa taifa.
  Makubaliano ya awali (ambayo NIPASHE inayo nakala yake), kati ya mwekezaji huyo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, yanaonyesha kwamba kampuni ya Agrisol itakodisha kwa miaka 99, eneo la Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.
  Mwekezaji pia atalipa Sh. 200 kama kodi ya ardhi kwa ekari na Halmashauri itapata Sh. 500 kwa ekari, hata hivyo haijulikani malipo hayo yatalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.
  Makubaliano hayo yanaonyesha pia kwamba iwapo kutatokea mgogoro, serikali itatumia busara kuutatua lakini ikishindikana, shauri hilo litasikilizwa jijini London, Uingereza na msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce).
  Kadhalika, inaelezwa kwamba mwekezaji huyo ataajiri mameneja wa mashamba kutoka nje hususan Afrika Kusini na ataendesha kilimo cha mbegu za kimaabara.
  Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri na wale wa Halmashauri ya Mpanda, wamekuwa 'wakipigia debe' uwekezaji huo, kwa madai kwamba utaongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza ajira kwa Watanzania.
  WANANCHI
  Watendaji wa vijiji na Kata zinazozunguka maeneo hayo, wamepinga uwekezaji huo kwa maelezo kwamba hawajashirikishwa kikamilifu na hati hiyo haina maslahi kwa taifa.
  Wakizungumza na waandishi wa habari walioongozana na timu ya watafiti kutoka shirika la HakiArdhi kuhusiana na uwekezaji huo, viongozi hao na wananchi wameitaka serikali ijifunze kwa yaliyotokea kwa kampuni tata ya Dowans kwa kujifunga na mikataba mibovu, ya muda mrefu kwa bei chee.
  Mwekezaji pia anaitaka serikali ibadili sheria ili kuruhusu kilimo cha vinasaba (Genetically Modified Crops), ambacho kimsingi kinaua mbegu za asili na kudhoofisha ardhi.
  Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo, alisema madiwani wa kata zinazozunguka eneo hilo, hawakuwahi hakualikwa kwenye mikutano iliyopitisha makubaliano hayo tata wala kwenda kwenye ziara nchini Marekani.
  “Viongozi wa wilaya wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wenyeviti wa kamati na Madiwani wa kutoka mbali na hapa kama vile Mpimbwe na Ulwila ndio waliokwenda Iowa- Marekani na waliporudi tu sisi tukawa tunaletewa maagizo bila kujua undani wake,” alisema.
  Msafara wa wajumbe kumi waliokwenda Iowa-Marekani uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutenge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, Philip Kalyalya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Silvester Nswima, Mkurugenzi wa Wilaya Eng. Emmanuel Kalobelo, Mjumbe wa kamati ya fedha Rose Mayaya, na Mjumbe wa Kamati ya maadili Teddy Nyambo.
  Wengine ni Mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa Kilimo na Mifugo Fabian Kashindye, na Haruna Mwakitanile (cheo hakikuweza kupatikana mara moja).
  Alisema wajumbe hao waliporudi kutoka Marekani, wananchi walishangazwa na kitendo cha Serikali kutenga mipaka kwa ajili ya mwekezaji wakati vijiji hivyo havijawahi kupimwa.
  Ofisa Mtendaji wa kata ya Mishamo, Agustino wanga, alisema hawajawahi kuiona kampuni ya AgriSol wala wawakilishi wao ambao ni Agrisol Tanzania Limited, na kwamba wamekuwa wakiwasikia viongozi wakieleza kuwa makazi hayo ya wakimbizi yatakodishwa kwa Wamarekani kwa miaka 99.
  “Mimi binafsi nina mpango wa kuhama kabisa maana wakiondoka wakimbizi tu, huduma muhimu nazo zitakoma, hatuwezi kuwezana na mwekezaji ambaye hatumjui,” alisema.
  Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya wafugaji mkoani Rukwa, Masanja Katambi, alisema inashangaza kuona serikali inaingia mkataba usio na maslahi kwa taifa badala ya kuwapatia wafugaji maeneo hayo ambao wamekuwa wakigombea malisho na wakulima.
  “Kila siku wafugaji wanagombana na wakulima na mara nyingine kuuana, kwa sababu ardhi haitoshi katika mkoa wetu. Wafugaji hudiriki hata kuwahonga askari wa wanyamapori katika mbuga ya Katavi ili kuingiza mifugo yao kwa malipo maalumu, hili Serikali hailioni?” alisema.
  Mkuu wa Makazi ya Katumba na Mishamo, Athuman Igwe, alisema anachosubiri ni kutekeleza amri ya serikali pindi taratibu za uwekezaji zitakapokamilika.
  Hata hivyo, alisema wakimbizi walipaswa kuwa wameondoka kupisha uwekezaji lakini anashangaa kuona kuwa bado zoezi hilo halijakamilika mpaka hivi sasa.
  “Hili Zoezi la kuwahamisha wakimbizi linaratibiwa na Tamisemi, sisi tunasubiri utekelezaji tu,” alisema mkuu huyo ambae pia ni mratibu wa makazi ya Ulyahulu yaliyopo Kigoma.
  Alifafanua kwamba kikwazo ni wakimbizi ambao wanataka walipwe Sh. 19 milioni kila mmoja kama fedha za uhamisho badala ya Sh. 300,000 walizopangiwa.
  Mmoja wa wakimbizi, Andrea Helmashi, alisema Sh. 300,000 ni ndogo kwa kuwa wengine wanafamilia ya watu zaidi ya 10 na kupendekeza kwamba wangelipwa Sh. 13 milioni.
  SERIKALI INASEMAJE
  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Rajab Rutenge, alitetea uwekezaji huo akieleza kwamba ni wa faida kubwa kwa taifa na wakazi wa maeneo yanayozunguka makazi hayo kwani utaboresha upatikanaji wa chakula nchini.
  “Mimi ni mtalaamu wa masuala ya chakula na nchi yetu inakabiliwa na janga la njaa, ni lazima tushirikiane na kampuni ya Agrisol kumaliza tatizo hilo,” alisema.
  Kwa upande wake, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambaye ni mmoja wa waliotia saini makubaliano hayo, Patrick Mwakuysa, alisema kampuni hiyo ina lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula, masoko na kutengeneza ajira kwa Watanzania.
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Sasa ufisadi uko wapi hapo? kwani hiyo ardhi anaondoka nayo, au anapanda mazao ya mbegu bora? Na kama kuna Watanzania wanataka ardhi si na wao waombe wapewe? au kuna mtanzania aliyenyimwa ardhi ya kuwekeza namna hiyo?

  Ingekuwa mimi hata hiyo kodi ya 200 na 500 nisingewalipisha kabisa, unajua hizo ni fedha nyingi sana kwa hizo eka ulizozitaja:

  Total Hectars: 300117 = Acres 741602.2197879696 x 700 = 519,121,553.85

  Hiyo ni kodi tu, mbali kodi ya mazao, kodi ya faida, na kodi nyingi za indirect, ajira, mbegu. Aaaaahhh aaahhhhh aaaahhh halafu mnasema ufisadi? kafanyeni nyinyi basi!

  Au wewe hujaona mashamba aliyotaifisha Nyerere akayafanya ya umma yalivyokufa hovyo na kugeuka mapori? Unanshangaza sana!
   
 3. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Bongo wenye mamlaka karibu wengi wana akili za samaki, unaona mtego lkn unalazimisha kupita. Haiwezekani uende ukasign mkataba USA halafu utegemee kuna maslahi ya taifa hapa!!, tumekuwa waombaji wawekezaji wa kutunyonya na sio kutuendeleza. Hii mikataba ni matokea ya Vasco da Gama (JK) wetu!
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  inabidi kabla ya mikataba kusainiwa ipitishwe kwa wananchi ipigiwe kura
   
 5. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye bold, kwa mtu asiye na akili timamu hataliona hilo. Na mara nyingi walamba miguu ya mafisadi huwa hawaoni tazito.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Faizaaa dah yaani mkataba wa 99 years kwako poa tuu na incase of disputes ni chamber of commerce uk
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ukisoma colonial economy in kenya under settler economy ndio utaona mikataba kama hii,,setttlers given land for a lease of 99 years,,,,,leo tunaizungumzia TANZANIA????je mkataba ueweka waz asilimia ngapi ya chakula ipatikane????je umesema watanzania wangap wenye elimu wataajiriwa????nadhan ni fursa kwa wataalam wa sua kupata ajira,mkataba useme waz kuwa watakaopata ajira ni watanzania tu,kama ni laboratory technicians wapo,SUA,UDSM,isije baadae tukajuta,TRL ilipigiwa debe KIKOWAPI????
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hata kama ardh haondoki nayo issue inakuja how watanzania watanufaika,umeona yanayojiri kapunga???umesikia juu ya mambo ya TRL????wawekezaji hawa wanakuwa wanawanyanya sa sana watanzania wa maeneo ya vijijin,hata huko kisarawe mwekezaj alopewa ekari mia nane sasa anawanyanyasa wanakijiji,,,,so sad!
  <br />
  <br />
   
 9. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 692
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  foxy ni foxy tu
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Nawashangaa sana watu wenye fikra finyu, kuna nchi zingine duniani zinawalipa wakulima ili walime, nyie wanakuja na fedha yao na vifaa vyao bado mnaona wanawadhulumu?

  Hebu niambie ni mkulima yupi wa kitanzania mweye uwezo wa kulima ekari zote hizo?

  Nijibuni, mashamba aliyotaifisha Nyerere yako wapi? si mngeendeleza yale, na aliyataifisha yana kila kitu na yanazalisha kwa wingi tu.
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
 12. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,873
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hata kama ni unafk wa kimagamba huo wako umezd, and am asking my self if ur mentally normal?
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  wakati mwingine huwa ninaposoma michango ya FAIZAFOXY huwa natamani kutapika lkn ninapokumbuka malengo halisi ya hii mitandao ya kijamii basi huwa na-take easy.
  Nadhani lengo lake ni ku-irritate watu humu ili wakasirike kama anavyofanya malaria sugu.Haiwezekani kila siku mtu anakuwa predictable kuhusu atakachochangia.Kwake yeye serikali yetu haikosei hata siku moja.
  Lkn pia kuna kitu kinanichanganya kuhusu huyu kijana FF.Muda wote anapatikana humu jf hivi ana kazi nyingine kweli? na hapo ukiachilia mbali ID nyingine anazotumia kwani tunajua anazo nyingi kama mwenzake MS
   
 14. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hivi hiyo kodi ya 700 kwa heka/ekari ni kwa viwango vya wapi wamechukulia?maana pale kwetu kilolo shamba linakodishwa hadi 20000 kwa heka kwa msimu/mwaka,sasa hawa hata wakisema ni kwa mwezi hiyo ni sawa na 8400,na kwenye mkataba huo bei itaendelea kubaki hiyohiyo kwa miaka yote 99 au kuna nafasi ya kufanya mabadiliko kadri muda unavyoenda?maana ukichukulia na thamani ya sarafu yetu inavyoshuka.......
   
 15. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  NILISHAWAHI SEMA TUWE NA PUBLIC DATABASE YA MIKATABA YA KITAIFA NCHINI TANZANIA,pia tuwe na public records ya Tume zinazoundwa na gharama za hizo tume na pia outcome za hizo tume
  asante kwa taarifa nisingeweza jua juu ya huu mkataba wa kibazazi ,thanks to JF.
  viongozi pia wapimwe kwa kuzingatia aina ya mikataba waliyoipitisha.kimsingi hapa rushwa imetolewa kwa wooote waliohusika ktk hii transactions
  1.rushwa ya safari kwenda USA,wamepewa per diem na ukichunguza gharama zote wamelipiwa na kampuni husika
  2,Mkataba umepitishwa fasta fasta,sheria inasema mwenye mamlaka ya kutoa Ardhi zaidi ya heka 500 ni Waziri wa Ardhi.na siyo halmashauri,hivyo basi watu wa wizarani ndio wangekuwa wahusika wakuu
  3.Tecknologia inarusu kupata taarifa za mwekezaje bila kusafiri kwenda America.na pia tuna Ubalozi wetu in USA wangeweza kutoa taarifa zote za mwekezaji
  4.Mwekezaji angepewa eneo moja la majaribio kabla ya kupewa eneo kubwa la pili bila ku-proove uwezo na nia yake kwa Tanzania
  5.Food Security ni swala la kimataifa.e.g Dubai,Baharain,Mauritius wamelima na kuwekeza Africa kwa ajili ya malisho nchini mwao.
  6.GM food/seeds ni hatari sana kwa Africa ,tuna wataalam waliogundua mbegu bora za mahindi unazoweza kuotesha mbegu zaidi ya mara 5.

  hayo yooote hayakuzingatiwa ,kwani wahusika walipewa a Shoping Trip to USA wakauza nchi yao. ni sawa na machifu wetu walipouza nchi kwa kupewa Vioo na Shanga na wakolini.   
 16. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kweli wewe ni balaa. kwan hapo hunaona poa tu, kwann mkataba ukasainiwe marekani na si tz? kwann hiyo mikataba hisiwausishe wananchi na kufanya uchunguzi wakina kama hiyo kampuni inaweza kuleta faida na si hasara kama magonjwa ya kansa? Unajua kuhusu hiyo kitu wanayokuja kuleta hapa tz? Nakwambia sasa ndoutaona balaa la kansa na magonjwa ya ajabu na mbegu zetu za asili zitakufa zote tutabaki kuwategemea wao kila muda wakupanda sasa mkulima wakawaida ndowameshammaliza kabisa. Wewe dada hacha mambo ya ushabiki fikilia kuhusu wananchi wavijijini na uone madhala yake.
   
 17. Rugambwa31

  Rugambwa31 JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  So what now if the US pays its farmers!
   
 18. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  labda alitaka na sisi tz tutoe ruzuku kwa wakulima wakubwa[ambazo na agrisol watazipata pia]analau ndo nilivyomuelewa
   
 19. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu yaonekana ww wayafurahia haya. Kwanza swala la kutumia genetically modified crops ni kinyume cha sheria ,hii ni kwa sababu ya madhara yake kwa binadamu. Wanaweza kukuzalishia chakula lakini hasara ya chakula hicho ni faida yao.....kwa nini ?genetically modified crops can influence your body na baada ya miaka kadhaaa zikatokea mutation za ajabu kama madhara ya kule Nagasaki na Hiroshima. They modify these crops to produce changes they wish in u.The problem is that our govt is no ccordinated at all hata maoni ya wanasayansi wetu haayapo. Baada ya hapo huu mkataba hauna tofauti ni ile ya ukolonoi wenyewe na babu zetu. Kuwapa ardhi miaka 99 ina maana hatutapata matumizi na ardhi kwa karne nzima. Sasa huono kuwa hawaitakii mema nchi maana hawatuachia ujuzi tuendeleze wenyewe. hata hivyo ndani ya miaka michache kwa kutumia mazao hayo wote mtakuwa matahira hiyo mtaachia kila ktu kwao. heri yangu nichukue uraia wa huku niwe safe,,,,lakini ndugu zangu, think big mkubwa. Pia ww kumbe ni dada ,sikiliza tukuambie madhara ya GMC kama hukusoma sayansi secondary , primary utakuwa unakumbuka kitu kinachoitwa kutegemeana katika mazingira.Genetically modified crops GMC affect every sphere of life ndio maana haihitajiki tz.OK ecolojia ikiharibika unafikiri utabaki unaishi? Si ajabu ukaja kuzaa viumbe vipya kwa sababu ya GMC ya wausa. Jitahidi kuelewa waeleweshe wengine pia,,,ikiwezekana ingia kabisa internet kula somo hilo ukipata tatizo npm.
   
 20. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NO huu mkataba haufai kabisa maana kwanza wanasema wataajiri mameneeja kutoka AAfrika kusini. kama ni maendeleo hapo si mahali pake.tafadhali watanzania tuwe makini. Mimi kutokana na thread ninazosoma zinanikatisha tamaa kuishi tanzania kweli kabisa. kwa nini tuna majuha wanatuongoza? Dr.slaa upo wapi?Lissu?Zitto tunauzwa jamani msaada wenu basi.
   
Loading...