kumbe mtandao wa chuzi umeenda mpaka ulaya?

Rugas

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
1,048
196


Gazeti pendwa la Ijumaa, kwa mara kwanza linauanika kwa upana mtandao wa Mkurugenzi wa Jumba la Dhahabu, Jumanne Kihangala ëMr. Chuzí ambao kwa idadi ya watu, linabeba majina mengi kuliko ule wa Miss Tanzania 2006-06, Wema Sepetu ambao ëulichanwa laivuí na gazeti ndugu la hili, Risasi katika toleo la hivi karibuni.

Hata hivyo, katika kuonesha kuwa mastaa wanazungukiana wao kwa wao, majina yaliyoonekana kwenye mtandao wa Wema, yote anaibuka kwa Chuz, ingawa ni katika sura tofauti.

Tochi la Ijumaa, linamtaja muigizaji, Jacqueline Steven Pentzel kama nambari moja kuunga mtandao huo ambapo penzi lake na Chuz ëlilimachuaí na kufikia hatua ya kutangaza ndoa, ingawa hivi karibuni ëwametibuanaí na kila mmoja hataki kumuona mwenzake.

Katika ëchapachapaí za hapa na pale, Chuz, aliwahi kutuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada mmoja wa kazi wa nyumba ya jirani yake na habari hiyo kuripotiwa kwenye magazeti.

Mtandao wa Chuz unaunga pia kwa muigizaji aliyewika zamani na Kundi la Nyota Ensemble ëMambo Hayoí, Leila Ismail ëLillieí ambaye katika uhusiano wao, waliweza kupata mtoto mmoja kabla ya kumwagana.

Chuz pia, aliwahi kuripotiwa kutoka na muigizaji ambaye pia ana kipaji cha kuimba, Joan Matovolwa, ingawa walibaki kufanya siri, lakini ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi kati yake na staa anayetambulika kwa uhusika wa kijini, Miriam Jolwa ëKabulaí uliwekwa kila kitu kweupe.

Habari zinasema kuwa Chuz alianza kutoka na Joan kabla ya kuhamishia majeshi kwa Kabula na ëishuí nzima ilipovuja, ikawa ugomvi usio na mwamuzi kati ya msanii huyo na Kabula aliye mzazi mwenza wa mkurugenzi huyo wa Jumba la Dhahabu.

Mtandao wa Chuz unapanuliwa kwanza na Joan ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Flava, marehemu Steve 2K aliyefariki dunia mwaka 2004 kwa kuchomwa kisu na mtayarishaji wa muziki, Castro ambaye kabla ya kesi hiyo, alikuwa anafanya kazi kwenye Studio ya Baucha Records.

Joan pia, amewahi kuhusika kimapenzi na Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El-Saadat ambaye ni mjane wa mnenguaji mwenye jina kubwa Bongo, marehemu Rukia Bruno.

Mtandao unaongezwa ukubwa kuwa Rukia amewahi kuripotiwa kutoka na Kanumba ambaye alijiweka kwa Wema na akaganda mpaka kuibuka ëkashkashí za kugombana na kufikishana mahakamani.

Katika mtandao huo, uchunguzi unaonesha kuwa Wema alianza kuandikwa kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa Bongo Flava, Khaleed Salum Mohamed ëTIDí ambaye aliwahi kuripotiwa kutoka na mzungu.

TID pia, aliwahi kuandikwa kuhusu kumpa ujauzito binamu yake ambaye walikuwa wanaishi nyumba moja, nyumbani kwao, Kinondoni, Dar lakini mwanamuziki huyo aliikana mimba hiyo.

Dogo mwenye heshima tele katika ulingo wa Bongo Flava, Heri Samir ëBluí naye anaunga kwenye listi, baada ya kuwa kati ya wanaume wa kwanza kwanza kuandikwa, wakihusishwa na penzi la Miss Tanzania huyo mstaafu.

Orodha hiyo inapanuliwa na wigo kwamba Kanumba amewahi kuripotiwa kutoka kimahaba na Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed ambaye alikuwa mchumba wa mtangazaji aliye pia ëkatunistií mwenye jina kubwa Bongo, Masoud Kipanya.

Inazidi kuchambuliwa kuwa, Kabula kwa sasa yupo kwa Mfalme wa Takae, Nice Lucas Mkenda ëMr.í ambaye ni mzazi mwenzake Diana Aston Villa aliyewahi kuhusika kimapenzi na mchekeshaji maarufu nchini, Steven Mangere ëNyerereí.

Hivi karibuni, magazeti mbalimbali ëyalimchoraí Wema kuwa anatoka kimapenzi kwa nyakati tofauti na ëbrazamenií wa Bendi ya African Stars ëTwanga Pepeta Internationalí, Charles Gabriel Mbwana ëChalz Babaí na Mkurugenzi wa Hartmann Production, Hartmann Osmund Mbilinyi.

Wigo wa mtandao huo, unaonesha kuwa Hartmann ana mke wake anayeishi Uingereza, wakati huo huo hapa nchini amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Miss Mwanza 2006, Aunt Ezekiel na ëmdadaí anayekwenda kwa jina la Linah.

Aidha, Aunt pia amewahi kuhusika kimapenzi na Mtanzania asiyejali thamani ya fedha katika matumizi, Jack Pemba ambaye alipoachana naye alijirusha na mrembo mmoja wa Kibongo, wakati huo huo akiwa na mke wake mzungu nchini Uingereza.
Kwa upande wa Chalz Baba, siyo stori kwamba alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kimwana manywele namba mbili 2007, Husna Sajenti, wakati huo huo hivi karibu akiwa amekorofishana na mrembo aliyekuwa akiishi naye kinyumba, anayekwenda kwa jina la Mariam.

Ijumaa limebaini kuwa Mariam pia yupo kimapenzi na mzungu ambaye humtumia kwa kumchuna, wakati alipokuwa na Chalz alikuwa na lengo la kula kitu roho inapenda.

Chalz pia kabla ya kuwa na Mariam aliwahi kuwa na uhusiano wa kudumu na mrembo anayekwenda kwa jina la Sada, wakati huo huo mwanamuziki huyo akiwa ni mzazi mwenzake Mama Jack.

Aidha, Wema anatajwa kutoka kimahaba na mheshimiwa mmoja nchini ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na mheshimiwa mwingine, wakati kiongozi huyo ana mchumba wake anayetaraji kufunga naye ndoa siku za usoni.

Mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe naye hasahauliki kwenye mtandao huo kwa kuwa amewahi kuishi na Wema kama mke na mume na kujitangaza kwamba wao ni wanandoa halali kabla ya kuachana kwa mbwembwe.

Kutokana na orodha hiyo, ni wazi kuwa mastaa wanazungukiana wao kwa wao, hivyo kuibua hatari ya kuenea kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kama mmoja atakuwa amevinasa, pia endapo hawatozingatia matumizi ya kondomu. Ijumaa linawashauri kuwa waaminifu kwa kutulia na mpenzi mmoja. MHARIRI.


Ni udaku,lakini naona kama kuna ukweli ndani yake,na km ni kweli ni hatari...

from www.globalpublisherstz.com/ijumaa/
 
yanakuhusu sana tu...we angalia huo mtanado.Siku moja utajikuta humo..tunahitaji kushauriana.
Tanzania bila ukimwi inawezekana?

Ah na wewe nini tena bana.

Tanzania bila ukimwi inawezekana ikiwa kila mtu atafuata kanuni zinazoimbwa kila siku za kujikinga, sio kwa umbeya wa tabloids na blogs.
 
Hawa mbwa-watu siku moja inabidi mtu awapige lawsuit ya $ 5m wafilisiwe vizuri tu ndiyo watatia akili.
 
Ah na wewe nini tena bana.

Tanzania bila ukimwi inawezekana ikiwa kila mtu atafuata kanuni zinazoimbwa kila siku za kujikinga, sio kwa umbeya wa tabloids na blogs.

nDOTO ZA MCHANA HIZO ABDULHALIM!

Ukiangalia threads za humu JF utakutana na watu wanauliza jinsi ya kuanzisha vitu vinavyoitwa gentlemen strip clubs hapa Tanzania, na madude mengine meengi yanayolingana na hayo...je kuna Tumaini la kumaliza ukimwi hapa kweli?

Mi namsupport RUGAS, kwa thread yake, maana kama umo humo kwenye mtandao, au haumo, au ulipata kumsaundisha mmoja wao hao akakukataa kwa njia moja ama nyingine, utajua jinsi ya kubadilisha mwenendo wa maisha!-Nakupongeza RUGAS ki-JF!
 
nDOTO ZA MCHANA HIZO ABDULHALIM!

Ukiangalia threads za humu JF utakutana na watu wanauliza jinsi ya kuanzisha vitu vinavyoitwa gentlemen strip clubs hapa Tanzania, na madude mengine meengi yanayolingana na hayo...je kuna Tumaini la kumaliza ukimwi hapa kweli?

Mi namsupport RUGAS, kwa thread yake, maana kama umo humo kwenye mtandao, au haumo, au ulipata kumsaundisha mmoja wao hao akakukataa kwa njia moja ama nyingine, utajua jinsi ya kubadilisha mwenendo wa maisha!-Nakupongeza RUGAS ki-JF!

Kwa kifupi sikuelewi.

Kwenye post ilopita nimeongelea kuhusu umuhimu wa watu kuzingatia wanayoambiwa na wataalamu ili kuepuka maambukizi ya HIV.

Kwenye post iliyotangulia, nimepinga suala la udaku la kusema sijui fulani mchumba wake sijui wameachana amemchukua sijui nani. Huu ni udaku pure na unawafaa watu wenye akili za wastani.

Sasa naomba unieleweshe post yako ina-respond hoja ipi?

Nitashukuru.
 
Kwa kifupi sikuelewi.

Kwenye post ilopita nimeongelea kuhusu umuhimu wa watu kuzingatia wanayoambiwa na wataalamu ili kuepuka maambukizi ya HIV.

Kwenye post iliyotangulia, nimepinga suala la udaku la kusema sijui fulani mchumba wake sijui wameachana amemchukua sijui nani. Huu ni udaku pure na unawafaa watu wenye akili za wastani.

Sasa naomba unieleweshe post yako ina-respond hoja ipi?

Nitashukuru.

ZOTE MBILI!

Kwanza ulisema HAYATUHUSU, lakini ghafla ukasahau, na kuanza kusema Tanzania bila Ukimwi ina....!

Huoni kuwa wewe ni..Nataka..Sitaki?

Hujajigundua?

Huh!..
 
ZOTE MBILI!

Kwanza ulisema HAYATUHUSU, lakini ghafla ukasahau, na kuanza kusema Tanzania bila Ukimwi ina....!

Huoni kuwa wewe ni..Nataka..Sitaki?

Hujajigundua?

Huh!..

Una tatizo la msingi la uelewa na nachelea nitaumiza vidole vyangu kwenye keyboard kuendelea kuchochea moto kwenye kuni mbichi.

Wasalam.
 
Una tatizo la msingi la uelewa na nachelea nitaumiza vidole vyangu kwenye keyboard kuendelea kuchochea moto kwenye kuni mbichi.

Wasalam.

Your SIGNATURE speaks it all for you, dont get troubled to puke all that stinking shit here!
....Peace...
 
Your SIGNATURE speaks it all for you, dont get troubled to puke all that stinking shit here!
....Peace...

Tena umenikumbusha aisee..Umeingia rasmi ktk list yangu ya watu wasio na input. Kusoma michango ya watu kama wewe ni kuumiza macho yangu na kupoteza muda wangu wa kuishi bila sababu.

Hongera!
 
Tena umenikumbusha aisee..Umeingia rasmi ktk list yangu ya watu wasio na input. Kusoma michango ya watu kama wewe ni kuumiza macho yangu na kupoteza muda wangu wa kuishi bila sababu.

Hongera!

I knew a cheap person of this calibre wouldnt afford my posts!...Too Classic for dogs!
 
Of course siwezi ku-afford post za mtu kichwapanzi, asiyeelewa hata anachokirespond..bua ha ha ha..

Pig-2115.jpg
 
Hawa mbwa-watu siku moja inabidi mtu awapige lawsuit ya $ 5m wafilisiwe vizuri tu ndiyo watatia akili.

Kamata five Blueray, watu design hii wanatakiwa unawakimbiza pale kisutu chapchap unakamata $ 5m unatupa kwenye charity.., wamekosa habari ya msingi zakuandika...upuuzi sana.
 
Magazeti mengine bwana! Tena bongo hawalindwi na freedom of speech kama marekani, kweli inabidi kuwe na lawsuits ndo watajirekebisha.

Tena kwa kuangalia hiyo ramani jamaa ameunganika na mademu watano cha ajabu nini sasa?
 
aaaaaaaaargh! gazeti la udaku lina watu wke bana, mtu mzima mwenye mawazo na hesabu nyingi hawezi kuumizwa kichwa na mambo ya kiswazi
 
kuna haja ya kuwa na madanguro kama ulaya, serikali itapata kodi kuliko sasa hivi kuna madanguro mengi yasiyo rasmi na ambayo hayana leseni na hivyo hawalipi kodi.

Mtake msitake madanguro rasmi yatapunguza kuongezeka kwa ukimwi maana wanafuata taratiibu zote

Kuhusu gazeti dawa ni kumpeleka mahakamani tu anatajirika kwa kdhalilisha watu yeye alikuwepo woote hao wakitiana?

Tatizo la mastaa uchwara wa bongo nao wamezidi kutangaza mahusiano yao wakati wanajua hawana mapenzi ya dhati. Wao wanaona ngono ndo dili.

YAP TZ bila ukimwi inawezekana
 
Back
Top Bottom