Kumbe Makongoro anaongea kama baba yake?

Kumbe Makongoro anaongea kama baba yake?

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,349
Reaction score
36,300
Sentensi kumi za Makongoro Nyerere kuhusu yeye na wanawake, ulevi na kutangaza nia (Sauti)..

makongoro_charles-1764x700.jpg

Headlines zenye stori za Siasa zimeendelea kutawala. Makongoro Nyerere ni Mbunge anaewakilisha TZ kwenye Bunge la Afrika Mashariki, nae alikuwa nyumbani kwao Butiama, hapa nimenukuu sehemu ya kile aichokisema akiwa huko.

"Nina nia ya kutangaza nia lakini bado sijatangaza nia… kwanza tuzungumze kuhusu utaratibu wa CCM. Mkutano Mkuu utakaa tarehe 11 na 12 June ili kuisikia Rasimu ya Chama, kuithibitsha na kuipitisha… Sizuki na kuanza kuzungumza kabla ya ilani ya Uchaguzi.. Wanaoamua nani awe kiongozi sio huku kwenye Chama, ni Watanzania…" Makongoro Nyerere.

Kwenye sentensi nyingine akasema hivi kuhusu wale wanaomzungumzia "Huyo mtoto wa Nyerere huyo ni mlevi kweli… mmewashtukia au vipi??. Huyo mtoto wa Nyerere huyo anapenda wanawake kweli.. sasa mlitaka nipende wanaume? Nawapenda kweli na mimi nashukuru MUNGU mnanipenda kweli" Makongoro Nyerere.

Makongoro Nyerere akamalizia hivi "CCM sio chama cha vibaka, ni chama cha walio wengi.. wakulima na wafanyakazi.. turudishieni chama chetu, mnaenda nacho wapi? Kufanya nacho nini? Alafu sisi mtuache wapi?"

Utamsikiliza kwa urefu zaidi kila alichokisema kwenye sauti hii (hapo chini) mtu wangu;

View attachment Makongoro.mp3

Chanzo: Millardayo.com
 
somehow!/

mle mle/ but

intunation ya baba kufanana na mtoto ni sawa kabisa / tatizo marithishano / ya serikali za kiafrica baba> mtoto >mjukuu
 
somehow!/

mle mle/ but

intunation ya baba kufanana na mtoto ni sawa kabisa / tatizo marithishano / ya serikali za kiafrica baba> mtoto >mjukuu
Kulithishana sio mbaya kama anaweza kukemea mafisi maji. Ila ndani ya CCM sidhani kama atweza. Pia Babake alikuwa ni mtu wa kusoma vitabu so, huyu atategemea ushauri kutoka kwa makanjanja, watamwingiza town, tutarudi kuleeeeeeeeee.
 
Hata kucheka kwa mbaaali kama baba yake.
 
somehow!/

mle mle/ but

intunation ya baba kufanana na mtoto ni sawa kabisa / tatizo marithishano / ya serikali za kiafrica baba> mtoto >mjukuu

mkuu nadhani hufuatilii haya mambo duniani, unaweza chukua mfano wa Taifa la Marekani tu sasa hao nao wanarithishana..acha kupotosha watu wewe na uache uvivu wa KUFIKIRI.
 
Hatuwezi kumpa Nchi Mlevi na mgoni ipo siku tutamkuta ambiance akivizia machangu.
 
So what???????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
 
Yule msani wa bongo movie kamzidi kwa mbali san huyu mako hajaweza kuiga vizuri!!!
 
Kwa jc nnavyo ona ccm itampitisha huyu wale vikingwe wanaojua nyerere bado mzma wampigie kura wakidhani ni yy

Hawa watamburuza Mama Maria kila kona bila kujali afya yake mpaka kieleweke!
 
Makongoro ndiye atapeperusha bendera ya CCM
Team lowassa tujipange kwakweli
 
tatiza sio mtu, ni je anaweza kukidhi haja za watanzania, hata akiwa baba na mjukuu...
 
ila sijaona ambacho ameonngea zaidi ya pumba na ushabiki shabiki tu . badla ya kujadili hoja yeye anajadili watu. angeenda kujiuza na si kuwapiga madongo wenzake. kiukweli anaonekana ni mhuni mhuni tu hana uwezo wowote basi tu.

labda ccm iamue kumbeba.... na hata angefanana na nyerere bado si sifa tunayoitaka.,kama sautu inafanana na nyerer sisi inatusaidia nini? kwan sisi tunataka mwigizaji wa sehemu ya kuongea nyerere wenye movie? aende zake huko ...mhuni mhuni tu chapombe na hajaonge hoja yoyote zaidi ya kufanya ucomedy.
 
Kwa jambo hili mfano wa marekani ni sahihi kabisa kwa watu wenye fikra mgando kwa watoto wa viongozi wastaafu kugombea. Je ukiwa mtoto wa mhandisi ni dhambi kurithi kazi ya mzazi kama una sifa? Tuache ukenge..hivi mwanaume gani lijari ambaye hapendi wanawake? Msitufundishe ushoga..p.
 
Back
Top Bottom