Duuh lakini huyo jamaa ni bendera fata upepo cha msingi atulize akili, kwanini asifunguke kwa wazazi wa demu,kama vipi akache ndoa kwanza mpaka atakapo jiweka pouwa, kwani hapo kalazimishwa na niwangapi wanavalishwa pete na wanaachana hata kabla hawajafunga ndoa?
Na atataka kukuuzia boda boda sindio kurudishana nyuma kimaendeleo huyo demu ni zero brain!!
Mwanangu we ni mwanaume mchulie jamaa kama ni ndugu yako....je ungemuacha amuoe huyo binti?Za mida wajumbe?. Kuna friend of mine hapa ananipa mchapo akitaka kujua afanye nini.
Ana binti aliyenaye katika mahusiano kwa miaka kadhaa sasa. Kijana anasoma ila ana gratuate this year. Binti kamkaba jamaa wafunge ndoa jamaa naye kaona ni sawa kwani kaona binti amepass viwango kuwa naye kimaisha ila jamaa anakwama sehemu moja ana ajira somewhere ya mkataba na analipwa 80% ya mshahara kwa mwezi kwa sababu kiwango chake cha elimu hakijafikia lengo la mshahara kamili. Kwa hili binti akamtia moyo kuwa asijali kabisaaa kwani kwao mahari anataja binti na akamhakikishia kuwa haitazidi laki tano ama sita jamaa kwa kuona hivyo na kwa kuzingatia umri wa ampendaye unamtupa mkono akajitosa binti akawakusanya ndugu zake wengi kuwapa taarifa kuwa amepata mchumba in short jamaa anamuuliza binti ampe siri ndg wanataka kiasi gani ili awaelezee washenga watakapo kwenda wajue kiasi binti anamwambia jamaa ajiandaye kwa milioni moja na nusu khe jamaa kasara mbaya ukitegemea ni miezi kama mitano tu imebaki kwao kufunga ndoa. Binti ni form four failure ila anakibarua mkoa mwingine mbali jamaa mawasiliano ni Simu tu. Jamaa akaa kimnya akajikunja kwani wazazi wa binti waligomea hapo hawataki chini ya hapo.
Jamaa amekubali. Sasa wameenda kwenye swara la Pete ya engagement binti anataka ya dhahabu si chini ya gramu mbili jamaa anamsihi amsaidie japo kidogo binti anagoma kwa kusema nini maana ya kuwa engaged?. Anamwambia wanunue Pete ya silver anamwambia ataiweka kwenye kidole cha nani?. Sasa hivi wamebakiza siku chache jamaa akatoe hiyo mahari anamwambia binti amsaidie pesa kidogo za kununulia vitu vya kuwapa wazazi wake kama blanket na kanga binti anawaka ile mbaya kuwa hata kuwa na amani kabisa akiwa ndani ya ndoa akifanya hivyo. Jamaa hana hamu naye ananiomba ushauri hapa kwani kaamkia kwangu asubuhi hii akitaka kuniuzia boda boda yake ama niichikue bond. Ushauri tafadhari Wajumbe. Mnisamehe kwa uandishi sio mzuri.
Heee anataka binti ampe hela? Ili akajichumbie????
Huyo rafiki yako nae, anajijua uwezo hana kwa sasa kwa nini apelekeshwe?
Unamaanisha ampe demu kibuti au?.
Mshikaji alitaka kumwona Baba mtu binti akagoma akisema kuwa baba yake hausiki anayehusika ni baba yake Mkubwa naye ndiye mtoa maamuzi yote. Pia unamaanisha nini kusema bendera fuata upepo?. Ila binti ndio kabadilika sana hasa kipindi an achoona ndoa iko mlangoni demand zinakuwa nyingi ka anaolewa na riz moko.
jamaa anataka kuangukia pua
Unamaanisha ampe demu kibuti au?.