..........wakigombana we shika jembe wende shambani wakipatana beba kapu ukavune
Vita vya panzi...................................
Kimaslahi ya kifedha au nafasi ya kutetea wanyonge?Uenyekiti wa ccm mkoa na ubunge kipi bora?
Mgeja Kaa kimya, Wewe hutufai kitu chochote wanashinyanga. Hebu fikiria madini yaliyopo shy, mifugo, pamba na ulinganishe na CCM yako ilivyoifanya shy kuwa, wewe kama mwenyekiti huoni aibu?
Badala yake unashambulia wanaopinga ufisadi??? unataka nini? chama kimekufa shy wewe ukiwa mwenyekiti umesaidiaaje kurejesha chama, kwa kura za utata ubunge shy town ndo msaaada wako kwa chama??
Kama huna uwezo wa kupambana na mafisadi acha wenye uwezo hata kama ni mdogo wafanye hivyo maana mafisadi ni adui wa taifa. Shy ndo imeathirika zaidi, sasa hoja ya kujenga nyumba kahama na masilahi ya nchi wapi na wapi? Kahama wanachagua mwakilishi wa wananchi sio mmliki wa nyumba kahama, ona aibu kuwa na mawazo finyu kama hayo. Unafikiri wanakahama ni wajinga?
Mwenyekiti wa chama na maslahi ya chama, mbunge na masilahi ya wananchi, huoni mbunge ni zaidi yako, wewe subiri kutumwa na chama wanachama 5mil (sensa yake pia ina mashaka makubwa, au wengi wafu) yeye anatumwa na wananchi 40mil.
Unakumbatia ufisadi leo hii utamwambia nani mwenye akili timamu akakuelewa, eti wanadandia sera ya CHADEMA, hiyo ni sera ya taifa kama huelewi. Ina maana ccm sera yao kuhusu ufisadi ni KUULINDA?
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amevunja ukimya kwa kumtaka Mbunge wa Kahama James Lembele (CCM), kutogeuka Mbwa mzee asiye na meno kwa kutafuta umaarufu kupitia jina lake huku akimuonya kwa kumwambia hana mamlaka ya kumngoa katika nafasi hiyo bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Alisema kutokana na kujiita kamanda mpambanaji wa ufisadi nchini yeye na kundi lake wamekuwa wakidandia hoja za CHADEMA hali inayoweza kukichimbia kaburi Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika harakati za kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Mgeja alisema katika kipindi cha miaka Saba mfululizo Mbunge huyo wa Kahama, amekuwa akijenga chuki dhidi yake kutokana na kukosa uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 alipotangaza Baraza lake la Mawaziri na jina lake kukosekana.
Mwenyekiti huyo, alisema kutokana na hali hiyo Lembeli, alijenga chuki dhidi yake na kupitia wapambe wake wa karibu, kumwambia chanzo cha kukosa nafasi ya uwaziri imesababisha na Mgeja.
Katika kipindi cha miaka Saba, sasa Lembeli amekuwa na chuki dhidi yangu na kisa kikubwa ni kukosa nafasi ya Uwaziri kutokana na nafasi ya yangu kama Mwenyekiti, niliweza kumshauri kuhusu kujenga mji Kahama, na sio kufikia Gesti kama anavyofanya hivi sasa.
Lakini ushauri wangu kama kiongozi wa chama alihisi nina mfuatafuata, nami kama kiongozi sijachoka kufanya kazi yangu, ila muda wote pamoja na kusema maneno yake ya hovyo kupitia vyombo vya habari dhidi yangu sasa nami nasema hapana.
Ikiwa anakujibu kifedhuli basi nawe unatakiwa kumjibu hivyo hivyo na leo ninavunja ukimya dhidi yake, ninamuambia nadai sasa yupo tayari kuacha Ubunge ili aniondoe Mgeja katika nafasi hii ya Uenyekiti, namkaribisha kwa moyo mkunjuvu bila kinyongo chochote. Ila atambue nafasi ya Uenyekiti wa CCM Shinyanga Mgeja, ataondolewa na wanachama waliompa madaraka haya na sio yeye.
Ikiwa wakati umefika wa kuondoka na wenye chama chao mkoa wa Shinyanga wakisema Mgeja pumzika ni sahihi. Kwa kauli yake hii Lembeli, inaonyesha wazi uwezo wake ni mdogo katika kuchambua mambo haya.
Nipo tayari kumpa bingo ya Sh. milioni 50, ikiwa Lembeli, atanionyesha mji wake, aliojenga Kahama, familia yake akiwemo mke wake na watoto wake na shule walisoma.
Kwa muda mwingi harakati zake za kutaka kuwania nafsi hii amekuwa akiihusisha familia yangu akiwemo mke wangu, hii si haki hapa kama anahitaji mapambano na Mgeja apambane nami lakini sio vinginevyo. Kwa anavyotaka kufanya sasa ni kutaka kubaka mamlaka ya wanachama wa CCM ambao ndiyo wenye kauli ya mwisho ya kusema nani mwenyekiti wao wa mkoa, alisema Mgeja.
Suala la kuwa na Nyumba Kahama mjini siyo issue sana kama ninavyojua mimi sababu makazi ya Mheshimiwa Lembeli akiwa jimboni kwake ni Bulungwa sehemu aliyozaliwa ambapo anazo nyumba zaidi ya mbili na kwa Makazi ya Lembeli yapo Bulungwa Mseki sehemu aliyozaliwa ambapo ana nyumba zaidi ya mbili kwa waliofika Bulungwa wanazifahamu. Jimbo la Kahama siyo hapo Kahama mjini peke yake jimbo ni kubwa. Issue ingekuwa nyumba basi Mheshimiwa anazo nyumba nyingi zikiwapo za Kunduchi Dar Es salaam na Arusha.
Ni vyema basi mlete hoja zenye mashiko zinazohusiana na Kazi yake ya uwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kahama na kamwe Nyumba ya Mbunge hakiwezi kuwa kipaumbele.
Hivi wewe mgeja umesoma hadi kiwango gan?