Kumbe Lembeli anaishi gesti hana nyumba Kahama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Lembeli anaishi gesti hana nyumba Kahama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kikulacho, Apr 12, 2012.

 1. K

  Kikulacho Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [FONT=&quot] MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amevunja ukimya kwa kumtaka Mbunge wa Kahama James Lembele (CCM), kutogeuka ‘Mbwa mzee asiye na meno’ kwa kutafuta umaarufu kupitia jina lake huku akimuonya kwa kumwambia hana mamlaka ya kumng’oa katika nafasi hiyo bila kufuata utaratibu wa kisheria.[/FONT]

  [FONT=&quot]Alisema kutokana na kujiita kamanda mpambanaji wa ufisadi nchini yeye na kundi lake wamekuwa wakidandia hoja za CHADEMA hali inayoweza kukichimbia kaburi Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika harakati za kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015.[/FONT]
  [FONT=&quot]Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Mgeja alisema katika kipindi cha miaka Saba mfululizo Mbunge huyo wa Kahama, amekuwa akijenga chuki dhidi yake kutokana na kukosa uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 alipotangaza Baraza lake la Mawaziri na jina lake kukosekana.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mwenyekiti huyo, alisema kutokana na hali hiyo Lembeli, alijenga chuki dhidi yake na kupitia wapambe wake wa karibu, kumwambia chanzo cha kukosa nafasi ya uwaziri imesababisha na Mgeja.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Katika kipindi cha miaka Saba, sasa Lembeli amekuwa na chuki dhidi yangu na kisa kikubwa ni kukosa nafasi ya Uwaziri kutokana na nafasi ya yangu kama Mwenyekiti, niliweza kumshauri kuhusu kujenga mji Kahama, na sio kufikia Gesti kama anavyofanya hivi sasa.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Lakini ushauri wangu kama kiongozi wa chama alihisi nina mfuatafuata, nami kama kiongozi sijachoka kufanya kazi yangu, ila muda wote pamoja na kusema maneno yake ya hovyo kupitia vyombo vya habari dhidi yangu sasa nami nasema hapana.[/FONT]

  [FONT=&quot]“Ikiwa anakujibu kifedhuli basi nawe unatakiwa kumjibu hivyo hivyo na leo ninavunja ukimya dhidi yake, ninamuambia nadai sasa yupo tayari kuacha Ubunge ili aniondoe Mgeja katika nafasi hii ya Uenyekiti, namkaribisha kwa moyo mkunjuvu bila kinyongo chochote. Ila atambue nafasi ya Uenyekiti wa CCM Shinyanga Mgeja, ataondolewa na wanachama waliompa madaraka haya na sio yeye.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Ikiwa wakati umefika wa kuondoka na wenye chama chao mkoa wa Shinyanga wakisema Mgeja pumzika ni sahihi. Kwa kauli yake hii Lembeli, inaonyesha wazi uwezo wake ni mdogo katika kuchambua mambo haya.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Nipo tayari kumpa bingo ya Sh. milioni 50, ikiwa Lembeli, atanionyesha mji wake, aliojenga Kahama, familia yake akiwemo mke wake na watoto wake na shule walisoma.[/FONT]
  [FONT=&quot]“Kwa muda mwingi harakati zake za kutaka kuwania nafsi hii amekuwa akiihusisha familia yangu akiwemo mke wangu, hii si haki hapa kama anahitaji mapambano na Mgeja apambane nami lakini sio vinginevyo. Kwa anavyotaka kufanya sasa ni kutaka kubaka mamlaka ya wanachama wa CCM ambao ndiyo wenye kauli ya mwisho ya kusema nani mwenyekiti wao wa mkoa,” alisema Mgeja. [/FONT]
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  kazi kweli kweli.madaraka yanapiganiwa kwa kila namna,nimejifunza mtu akikuchokoza kaa kimya,kimya ni busara.mtu mkorofi atajulikana tu hata huhitaji kuwaambia watu wasikie ama waone coz watasikia na kuona wenyewe.kisa uenyekiti wa chama mkoa watu wanashushiana maneno mazito,nadhani wazee ni sehem muhimu ya kuchota busara sasa kwa mwendo huu wanakatisha tamaa japo ni magamba na kwenu madaraka ni mhm kuliko utu nawapeni pole bwa.james lembeli na mwenyekiti wako wa chama mkoa wa shinyanga.
   
 3. O

  Original JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Vita vya panzi...................................
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ..........wakigombana we shika jembe wende shambani wakipatana beba kapu ukavune
   
 5. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Uenyekiti wa ccm mkoa na ubunge kipi bora?
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,605
  Likes Received: 5,780
  Trophy Points: 280
  Waacheni wafu wazike wafu wao
  topic closed
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu Mgeja Mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga ndiye anayetumiwa na mafisadi kwenye NEC kuwasemea hoja za kuwatetea kwa ujira maalun; in other words they pay him to defend their interests in this party organ! Huyu ni mamluki.
   
 8. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Dah! Magamba bwana yameamua kutoana povu kisa madaraka!!
   
 9. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  ngoja kidogo tu utasikia mmojawapo sio raia so aculiwe madaraka
   
 10. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Wanazidiana kwa viwango vya kutoa rushwa. wote wametoa rushwa za aina tofauti kupata ujumbe wa NEC!
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Lembeli in limbo. Huyu mzee yuko after kitu kidogo . Anaibana barrick ila tangu achaguliwe na bunge kwenda north mara kufanya uchunguzi wa uharibifu wa mazingira na Barrick wakawa wanampa 300,000 kwa siku on top of posho za bunge amekaa kimia mwanaharumu huyu na hajakohoa tena kuhusu Barrick. Nwele zake nyeupe si ishara ya busara but utapeli.
   
 12. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mgeja Kaa kimya, Wewe hutufai kitu chochote wanashinyanga. Hebu fikiria madini yaliyopo shy, mifugo, pamba na ulinganishe na CCM yako ilivyoifanya shy kuwa, wewe kama mwenyekiti huoni aibu?

  Badala yake unashambulia wanaopinga ufisadi??? unataka nini? chama kimekufa shy wewe ukiwa mwenyekiti umesaidiaaje kurejesha chama, kwa kura za utata ubunge shy town ndo msaaada wako kwa chama??

  Kama huna uwezo wa kupambana na mafisadi acha wenye uwezo hata kama ni mdogo wafanye hivyo maana mafisadi ni adui wa taifa. Shy ndo imeathirika zaidi, sasa hoja ya kujenga nyumba kahama na masilahi ya nchi wapi na wapi? Kahama wanachagua mwakilishi wa wananchi sio mmliki wa nyumba kahama, ona aibu kuwa na mawazo finyu kama hayo. Unafikiri wanakahama ni wajinga?

  Mwenyekiti wa chama na maslahi ya chama, mbunge na masilahi ya wananchi, huoni mbunge ni zaidi yako, wewe subiri kutumwa na chama wanachama 5mil (sensa yake pia ina mashaka makubwa, au wengi wafu) yeye anatumwa na wananchi 40mil.

  Unakumbatia ufisadi leo hii utamwambia nani mwenye akili timamu akakuelewa, eti wanadandia sera ya CHADEMA, hiyo ni sera ya taifa kama huelewi. Ina maana ccm sera yao kuhusu ufisadi ni KUULINDA?
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni wao na chama chao!
   
 14. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 533
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Heheeeee!
  Na bado, hii ndiyo siri ya laana ya chama kinachokufa.
  Watafarakana na kuanikana kabla ya kuzikana!
   
 15. M

  MGOME Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Suala la kuwa na Nyumba Kahama mjini siyo issue sana kama ninavyojua mimi sababu makazi ya Mheshimiwa Lembeli akiwa jimboni kwake ni Bulungwa sehemu aliyozaliwa ambapo anazo nyumba zaidi ya mbili na kwa Makazi ya Lembeli yapo Bulungwa Mseki sehemu aliyozaliwa ambapo ana nyumba zaidi ya mbili kwa waliofika Bulungwa wanazifahamu. Jimbo la Kahama siyo hapo Kahama mjini peke yake jimbo ni kubwa. Issue ingekuwa nyumba basi Mheshimiwa anazo nyumba nyingi zikiwapo za Kunduchi Dar Es salaam na Arusha.

  Ni vyema basi mlete hoja zenye mashiko zinazohusiana na Kazi yake ya uwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kahama na kamwe Nyumba ya Mbunge hakiwezi kuwa kipaumbele.
   
 16. d

  dguyana JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ule mnara ulioandikwa katika bible ule watu waliokuwa wanaujenga huku wakiongea lugha tofauti unaitwaje vile?
   
 17. M

  Murukulazo JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 576
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mnara wa Babeli.....
   
 18. e

  evoddy JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Imeandikwa acha wafu wazike wafu wao ,CCM wote ni wezi na wala rushwa na watoa rushwa wakubwa ispokuwa wanazidiana viwango,
   
 19. m

  mwanantwe New Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Busara kubwa inahitajika kwa Kiongozi. Watu wanapaswa watofautishe maneno yanayotolewa na Kiongozi. Hata hivyo kutumia vyombo vya habari katika kushambuliana sio njia muafaka ya kumaliza tatizo
   
 20. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hah hah hah hah a new day has come
   
Loading...