Kumbe Lembeli anaishi gesti hana nyumba Kahama

Mbunge wetu Kyela Dr Mwakyembe kama anataka kuongelea matatizo ye Kyela yeye huwaita waandishi wa habari nyumbani kwake Kunduchi-Dar!

Dr Mwakyembe pia HANA NYUMBA Kyela isipokuwa nyumba ya wazazi wake Mpiki-Mwangupili-Ngonga!
 
Mnara wa babeli.Na hawa wanaobishana ndan ya magamba wanaupromote ufisadi wako sawa na walikuwa wanamjarbu mungu maana magamba wanapingana na ukweli wataumbuka kabla ya 2015 na chadema itachukua nchi kiulainiii kama inanawa.Watu wanaichukia ccm sana watz kwa sababu ya uongo na ufisad unaosababsha maisha magumu kwa wananch wake.Tunataka mabadiliko ccm tuh
 
Ndo maana analilia posho ziongezwe ili alale guest nzuri muheshimiwa Lembeli
 
Mgeja Kaa kimya, Wewe hutufai kitu chochote wanashinyanga. Hebu fikiria madini yaliyopo shy, mifugo, pamba na ulinganishe na CCM yako ilivyoifanya shy kuwa, wewe kama mwenyekiti huoni aibu?

Badala yake unashambulia wanaopinga ufisadi??? unataka nini? chama kimekufa shy wewe ukiwa mwenyekiti umesaidiaaje kurejesha chama, kwa kura za utata ubunge shy town ndo msaaada wako kwa chama??

Kama huna uwezo wa kupambana na mafisadi acha wenye uwezo hata kama ni mdogo wafanye hivyo maana mafisadi ni adui wa taifa. Shy ndo imeathirika zaidi, sasa hoja ya kujenga nyumba kahama na masilahi ya nchi wapi na wapi? Kahama wanachagua mwakilishi wa wananchi sio mmliki wa nyumba kahama, ona aibu kuwa na mawazo finyu kama hayo. Unafikiri wanakahama ni wajinga?

Mwenyekiti wa chama na maslahi ya chama, mbunge na masilahi ya wananchi, huoni mbunge ni zaidi yako, wewe subiri kutumwa na chama wanachama 5mil (sensa yake pia ina mashaka makubwa, au wengi wafu) yeye anatumwa na wananchi 40mil.

Unakumbatia ufisadi leo hii utamwambia nani mwenye akili timamu akakuelewa, eti wanadandia sera ya CHADEMA, hiyo ni sera ya taifa kama huelewi. Ina maana ccm sera yao kuhusu ufisadi ni KUULINDA?

Hizi ndizo gharama za ufisadi,tusubiri 2015 tutajua mengi.
 
Tuwaache magamba wapalulane sie tujenge cdm yetu.Hongera magamba hiyo ndiyo kasi na nguvu zaidi mliyowaahidi watanzania!!
 
Hata Kanumba alikuwa amepanga! inaonekana hizo ni chuki binafsi,kama huyo mwenyekiti anajiamini kwa nini analalama jukwaani si asuburi wapambane kwa hoja!tatizo mtu yeyote akiwa chama cha magamba mfumo wa kufikiri hubadilika kwa kuwa anapata mfumo mwingine wa kufikiri kuliko ule wa kawaida
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amevunja ukimya kwa kumtaka Mbunge wa Kahama James Lembele (CCM), kutogeuka ‘Mbwa mzee asiye na meno’ kwa kutafuta umaarufu kupitia jina lake huku akimuonya kwa kumwambia hana mamlaka ya kumng’oa katika nafasi hiyo bila kufuata utaratibu wa kisheria.

Alisema kutokana na kujiita kamanda mpambanaji wa ufisadi nchini yeye na kundi lake wamekuwa wakidandia hoja za CHADEMA hali inayoweza kukichimbia kaburi Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika harakati za kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Mgeja alisema katika kipindi cha miaka Saba mfululizo Mbunge huyo wa Kahama, amekuwa akijenga chuki dhidi yake kutokana na kukosa uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 alipotangaza Baraza lake la Mawaziri na jina lake kukosekana.
Mwenyekiti huyo, alisema kutokana na hali hiyo Lembeli, alijenga chuki dhidi yake na kupitia wapambe wake wa karibu, kumwambia chanzo cha kukosa nafasi ya uwaziri imesababisha na Mgeja.
“Katika kipindi cha miaka Saba, sasa Lembeli amekuwa na chuki dhidi yangu na kisa kikubwa ni kukosa nafasi ya Uwaziri kutokana na nafasi ya yangu kama Mwenyekiti, niliweza kumshauri kuhusu kujenga mji Kahama, na sio kufikia Gesti kama anavyofanya hivi sasa.
“Lakini ushauri wangu kama kiongozi wa chama alihisi nina mfuatafuata, nami kama kiongozi sijachoka kufanya kazi yangu, ila muda wote pamoja na kusema maneno yake ya hovyo kupitia vyombo vya habari dhidi yangu sasa nami nasema hapana.

“Ikiwa anakujibu kifedhuli basi nawe unatakiwa kumjibu hivyo hivyo na leo ninavunja ukimya dhidi yake, ninamuambia nadai sasa yupo tayari kuacha Ubunge ili aniondoe Mgeja katika nafasi hii ya Uenyekiti, namkaribisha kwa moyo mkunjuvu bila kinyongo chochote. Ila atambue nafasi ya Uenyekiti wa CCM Shinyanga Mgeja, ataondolewa na wanachama waliompa madaraka haya na sio yeye.
“Ikiwa wakati umefika wa kuondoka na wenye chama chao mkoa wa Shinyanga wakisema Mgeja pumzika ni sahihi. Kwa kauli yake hii Lembeli, inaonyesha wazi uwezo wake ni mdogo katika kuchambua mambo haya.
“Nipo tayari kumpa bingo ya Sh. milioni 50, ikiwa Lembeli, atanionyesha mji wake, aliojenga Kahama, familia yake akiwemo mke wake na watoto wake na shule walisoma.
“Kwa muda mwingi harakati zake za kutaka kuwania nafsi hii amekuwa akiihusisha familia yangu akiwemo mke wangu, hii si haki hapa kama anahitaji mapambano na Mgeja apambane nami lakini sio vinginevyo. Kwa anavyotaka kufanya sasa ni kutaka kubaka mamlaka ya wanachama wa CCM ambao ndiyo wenye kauli ya mwisho ya kusema nani mwenyekiti wao wa mkoa,” alisema Mgeja.

Hivi wewe mgeja umesoma hadi kiwango gan?
 
Tatizo Mgeja shule ni std seven sifa kubwa aliyonayo ni fitina ndio maana ameweza hata kupata umweyekiti wa magamba mkoa. Lembeli ana nyumba kijiji achozaliwa yeye anataka awe na nyumba Kahama mjini si lazima kwani ya kijijini ipo mjini ni option kama atataka
 
Suala la kuwa na Nyumba Kahama mjini siyo issue sana kama ninavyojua mimi sababu makazi ya Mheshimiwa Lembeli akiwa jimboni kwake ni Bulungwa sehemu aliyozaliwa ambapo anazo nyumba zaidi ya mbili na kwa Makazi ya Lembeli yapo Bulungwa Mseki sehemu aliyozaliwa ambapo ana nyumba zaidi ya mbili kwa waliofika Bulungwa wanazifahamu. Jimbo la Kahama siyo hapo Kahama mjini peke yake jimbo ni kubwa. Issue ingekuwa nyumba basi Mheshimiwa anazo nyumba nyingi zikiwapo za Kunduchi Dar Es salaam na Arusha.

Ni vyema basi mlete hoja zenye mashiko zinazohusiana na Kazi yake ya uwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kahama na kamwe Nyumba ya Mbunge hakiwezi kuwa kipaumbele.

Mgome, nahisi wewe ndiye Lembeli mwenyewe na kama siye nahisi ni mwanaye au mtu aliyetumwa na Lembeli kujibu hii thread. Nasema hivyo kwa kuwa umetoa majibu ya ndani kabisa ya raslimali anazomiliki mlalamikiwa yakiwa na usahihi wa hali ya juu. Hata hivyo nakupongeza kwa kuwa mwana JF.
 
Waache watoane meno lakini Kahama wala hatuihitaji CCM,sisi ni waathirikua wakubwa wa ufisadi wa CCM katika sekta ya madini. Akina Nape,Mgeja na CCM yao wamewapa hawa MATAPELI -Barrick wanaowaita wawekezaji ardhi yetu na sasa wanapora dhahabu yetu. Kahama mjini tulishaanza nao,tulikula hela zao 2010 lakini kwenye sanduku la kura hatukukosea tulichagua CDM kata zote kwa kiti cha udiwani.Lembeli kama ni mpambanaji wa kweli ahamie CHADEMA aachane na Mgeja wala hana lolote, kipindi kile alikuwa mwenyekiti wa halimashauri ya w/Kahama hakuna alichofanya zaidi ya kudhoofisha maendeleo yetu.
 
Hivi wewe mgeja umesoma hadi kiwango gan?

Mgeja kichwa kwelikweli alijitahidi kupiga kitabu mpaka akamaliza darasa la saba. Ni kiongozi wa kupigiwa mfano kwa bidii ya kujiendeleza kielimu. Pamoja na elimu hiyo ya juu, amehudhuria semina nyingi za ccm na kutunukiwa vyeti vya mahudhurio.
 
Back
Top Bottom