Msigazi Mkulu
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 4,184
- 3,421
Huyo akikupenda atakuja mwenyewe, huwa hawana longolongo kuna rafiki yangu tulienda wote field maeneo ya HAI, tulipokuwa tunaishi jirani palikuwepo kabinti kazuri kumbe ni bubu na hasikii pia, sasa alipotuona akawa anakuja kututembelea na akamchagua mmoja wetu tulikuwa watatu ndo wakawa wanawasiliana kwa ishara japo na huyo mwenzetu alikuwa hajui alichofanya alimuonesha ishara ya mapenzi kwa kuweka mkono wake kifuani na kuinama kidogo. Binti huyo alifurahi ndo akamukaribisha chumbani na siku hiyo hiyo akala mzigo. Iliendelea kila siku akituona tunatoka job na yeye anakuja. Kimbembe kilikuwa atamuagaje siku akiondoka maana huyo binti kiziwi alizimika sana, ilibidi tutorokea saa 11 alfajiri. Pamoja na hayo mama yake alikuja kugundua kwamba mmoja wetu anakula mzigo na alimfuata akamwambia tafadhari usimpe mimba maana akizaa atahangaika na mtoto.