Kumbe kupinga utekaji ni uchochezi na uhaini!?

Kumbe kupinga utekaji ni uchochezi na uhaini!?

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,745
Reaction score
1,171
Sovereignity state for the freedom of people's imeamua kupambana na wananchi huru wanaopinga uvunjifu wa haki za binadamu.

Nani asiyejua aliyemfunga Paka kengele,kengele imebana shingo ya Paka ,Sasa anatapatapa!

Utekaji umeondoka na kisiwa Cha amani,hata wageni au watalii si salama Tena,kwa kuwa kengele ya Paka imezua taharuki,imejeruhi shingo ya Paka atayekutana naye Cha mtema Kuni atakiona.

Najaribu kufikiri tumefikaje hapa!
Tuna katiba ya Watawala wasiyoiamini au Watawala wameamua ku demonstrate ibara ya 18 ya katiba ya JMT,inayotoa haki ya kutoa habari,kuhoji na kupata habari!

Nini muktadha wa hili jambo,kama kanisa la Ufufuo na uzima limefungwa kwa kuikumbusha serikali,hivyo vyombo vya habari vyenye mamlaka ya kuhabarisha umma vikao salama Kwa kiwango Gani,au wameungana na Paka kuficha uovu wake!

Hizo NGO's zenye dhamana ya kutetea Haki nazo ziko salama au ndiyo wanashiriki tafrija yenye kiu ya wenye damu salama.

Uko wapi usalama wa raia na Mali zake ikiwa wawindwaji wanasakwa na walinzi hao!

Paka kachafukwa,tumtafute wa kumfungua hiyo kengele huenda taharuki ikapungua.
 
Tupo arsenal ground battle to battle,mtawala anachukizwa sana na kuumizwa sana na maneno kuliko utekaji unaoendelea!

Kama Kuna Dola ndani ya Dola serikali iweke wazi,Mwalimu Nyerere alichukizwa na mtu aliyesema serikali yake ameiweka mfukoni,Samia haumozwi na watekaji wanaoonekana wana nguvu kuliko serikali.

Kama wanateka,wanaouwa na serikali Iko Kimya mnataka tuamini kuwa kuteka si kipaumbele chake ili kunyamazisha,wanakushauri nyuma ya pazia wanakung'ong'a kalaghabaho
 
Back
Top Bottom