Kama ulivyosema, wanga ndio tatizo. Mimi nafanya diet pia, Nina miezi kadhaa, sili wali, ugali, mkate chapati na maandazi na jamii hiyo.
Chakula kikubwa ni maboga, nikibadili na magimbi au ndizi tamu, hiyo ni kutokana na mapenzi yangu. Vitoweo vingine kama samaki au kuku, nakula kama kawaida japo si kwa wingi, mboga za majani na matunda kwa wingi, asali kunenepabadala ya sukari katika chai, sinywi soda yoyote, maji kwa wingi, juisi kidogo. Sifanyi zoezi lolote wala kutumia supplements, nimeshapungua kilo si chini ya 15.