Njowepo
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 9,710
- 2,233
Mhitimu mwanzilishi 1961 afunika mahafali UDSM
Mwananchi Sunday, 28 November 2010 20:59
Jackson Odoyo
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam kimeadhimisha mahafali ya 40 kwa staili ya aina yake, baada ya kumwalika aliyekuwa mwanafunzi wa kwanza kumaliza katika chuo hicho kati ya 16 waliohitimu masomo yao mwaka 1961, Gerald Kakuba.
Kakuba, raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 72, alikuwa kivutio kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambako zilifanyika sherehe hizo, baada ya kutambulishwa na Makamu Mkuu wa Udsm, Profesa Rwekaza Mkandara.
"Mahafali ya 40 yanafanyika huku kukiwa na bahati ya kuhudhuriwa na mwanafunzi wa kwanza kuhitimu chuo hiki kati ya 16 waliomaliza hapa," alisema Profesa Mkandala.
Baada ya wahitimu hao kusikia historia fupi ya Kakuba, waliripuka kwa shangwe na vigelele ukumbi mzima, huku wale waliokuwa mbali na eneo alilokaa mwanafunzi huyo wakijaribu kusimama kumuona na kumpungia mkono.
Kakuba ni kati wanafunzi 16 waliomaliza chuoni hapo Kitivo cha Sheria, ni miongoni mwa wanafunzi sita walio hai.
Akizungumza na Mwananchi juzi, Kakuba alisema kitu kikubwa ambacho anakikumbuka ni msingi imara waliojengewa wakati wa masomo chuoni hapo.
Kakuba ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea nchini Uganda, na mwanasheria wa kwanza katika Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977, alisema anajivunia elimu aliyopa chuoni hapo.
"Kikubwa ambacho ninajivunia mpaka hivi sasa katika maisha yangu, ni elimu ya sheria niliyopata chuoni hapa, ambayo imenisaidia katika maisha yangu tangu nikiwa kijana mpaka sasa nimekuwa mzee," alisema Kikuba.
Alisema chuo hicho bado kinaongoza kwa ubora katika Kitivo cha Sheria Afrika Mashariki na Kati.
Akitaja baadhi ya wanafunzi wenzake sita walio hai mpaka sasa kati ya 16 waliomaliza chuoni hapo mwaka 1961, Kakuba alisema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya, Samuel Kivuitu.
"Ninakumbuka tulimaliza na Samuel Kivuitu, raia wa Kenya, Jully Manning (Mtanzania), Mussa Kwikima (Mtanzania), John Haminwa (Mkenya) na James Miruka (Mkenya) na hawa wote bado wako hai.
Alisema kila wakati wanaposikia chuo hicho kinafanya mahafali, wanakumbuka kwa kutumiana ujumbe mbalimbali, huku wakijiona sehemu ya wahitimu wa wakati huo na kwamba, amefurahishwa na hatua ya uongozi wa chuo kumwita kushuhudia tukio la historia.