Kumbe Kivuitu ni mmoja wa wahitimu wa kwanza UDSM way back 1961

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Mhitimu mwanzilishi 1961 afunika mahafali UDSM


Mwananchi Sunday, 28 November 2010 20:59

Jackson Odoyo
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam kimeadhimisha mahafali ya 40 kwa staili ya aina yake, baada ya kumwalika aliyekuwa mwanafunzi wa kwanza kumaliza katika chuo hicho kati ya 16 waliohitimu masomo yao mwaka 1961, Gerald Kakuba.
Kakuba, raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 72, alikuwa kivutio kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambako zilifanyika sherehe hizo, baada ya kutambulishwa na Makamu Mkuu wa Udsm, Profesa Rwekaza Mkandara.

"Mahafali ya 40 yanafanyika huku kukiwa na bahati ya kuhudhuriwa na mwanafunzi wa kwanza kuhitimu chuo hiki kati ya 16 waliomaliza hapa," alisema Profesa Mkandala.

Baada ya wahitimu hao kusikia historia fupi ya Kakuba, waliripuka kwa shangwe na vigelele ukumbi mzima, huku wale waliokuwa mbali na eneo alilokaa mwanafunzi huyo wakijaribu kusimama kumuona na kumpungia mkono.
Kakuba ni kati wanafunzi 16 waliomaliza chuoni hapo Kitivo cha Sheria, ni miongoni mwa wanafunzi sita walio hai.
Akizungumza na Mwananchi juzi, Kakuba alisema kitu kikubwa ambacho anakikumbuka ni msingi imara waliojengewa wakati wa masomo chuoni hapo.

Kakuba ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea nchini Uganda, na mwanasheria wa kwanza katika Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977, alisema anajivunia elimu aliyopa chuoni hapo.

"Kikubwa ambacho ninajivunia mpaka hivi sasa katika maisha yangu, ni elimu ya sheria niliyopata chuoni hapa, ambayo imenisaidia katika maisha yangu tangu nikiwa kijana mpaka sasa nimekuwa mzee," alisema Kikuba.
Alisema chuo hicho bado kinaongoza kwa ubora katika Kitivo cha Sheria Afrika Mashariki na Kati.

Akitaja baadhi ya wanafunzi wenzake sita walio hai mpaka sasa kati ya 16 waliomaliza chuoni hapo mwaka 1961, Kakuba alisema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya, Samuel Kivuitu.
"Ninakumbuka tulimaliza na Samuel Kivuitu, raia wa Kenya, Jully Manning (Mtanzania), Mussa Kwikima (Mtanzania), John Haminwa (Mkenya) na James Miruka (Mkenya) na hawa wote bado wako hai.

Alisema kila wakati wanaposikia chuo hicho kinafanya mahafali, wanakumbuka kwa kutumiana ujumbe mbalimbali, huku wakijiona sehemu ya wahitimu wa wakati huo na kwamba, amefurahishwa na hatua ya uongozi wa chuo kumwita kushuhudia tukio la historia.
 
"Akitaja baadhi ya wanafunzi wenzake sita walio hai mpaka sasa kati ya 16 waliomaliza chuoni hapo mwaka 1961, Kakuba alisema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya, Samuel Kivuitu.
"Ninakumbuka tulimaliza na Samuel Kivuitu, raia wa Kenya, Jully Manning (Mtanzania), Mussa Kwikima (Mtanzania), John Haminwa (Mkenya) na James Miruka (Mkenya) na hawa wote bado wako hai"

hivi udsm wanatufundishaje uzalendo huyu Bwana Kwikima kwanini nayeye asingelialikwa kwenye mahafali hayo tena yupo karibu tu Tabora pale kwa wanyamwezi au ndo mambo ya Siasa kwa kuwa yule bwana toka enzi na enzi ni mpingaji mkuu wa CCM?

kwa maoni yangu wangemwalika na yeye kwani kama ni uanasheria hata yeye ni lawyer pia tena ni mtoto wa kwetu
mnaonaje wanajamii wenzangu?????????????
 
"Akitaja baadhi ya wanafunzi wenzake sita walio hai mpaka sasa kati ya 16 waliomaliza chuoni hapo mwaka 1961, Kakuba alisema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya, Samuel Kivuitu.
"Ninakumbuka tulimaliza na Samuel Kivuitu, raia wa Kenya, Jully Manning (Mtanzania), Mussa Kwikima (Mtanzania), John Haminwa (Mkenya) na James Miruka (Mkenya) na hawa wote bado wako hai"

hivi udsm wanatufundishaje uzalendo huyu Bwana Kwikima kwanini nayeye asingelialikwa kwenye mahafali hayo tena yupo karibu tu Tabora pale kwa wanyamwezi au ndo mambo ya Siasa kwa kuwa yule bwana toka enzi na enzi ni mpingaji mkuu wa CCM?

kwa maoni yangu wangemwalika na yeye kwani kama ni uanasheria hata yeye ni lawyer pia tena ni mtoto wa kwetu
mnaonaje wanajamii wenzangu?????????????

Si unajua nabii hakubaliki kwao


Nyote mko sawa kabisa
 
jamani tusiharibu historia ya chuo kikuu cha dar es salaam. kwanza kabisa, chuo cha dsm hakikuanza kutoa wahitimu wake wa kwanza 1961. mwaka huo ndio tulipata uhuru. wanafunzi wa kwanza kuingia chuo hicho ni wale walio maliza darasa la 14 mwaka 1960, kina Mussa kwikima, Zahor El-kindy na nadhani Anrnold Kilewo na Peter Bakilana. Huyo Muganda kama alimaliza degree yake 1961, haikuwa kutoka chuo kipya cha dar es salaam.

Wakati chuo kinaanzishwa chuo kilikua ni sehemu ya chuo kikuu cha london Pamoja na Makerere na Nairobi mpaka kilipoanziwsa chuo kikuu cha africa mashriki ambacho wahitimu wa kwanza wa chuo cha afrika mashariki ilikuwa 1966.

Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilanza kwenye miaka ya 70, kwa hiyo chuo hiki wala hakijafikisha miaka hiyo 50 ambayo Prof mkuu wa chuo anataka watu wote duniaqni waamini,

macinkus
 
Umenikumbusha uchaguzi wa kenya,

huyu kivuitu alichakachua kura za raila odinga na alilazimishwa na kibaki amtangaze kuwa ni mshindi kupitia Television ya nchi hiyo KBC lakini alipohojiwa na kituo cha KTN na Aljazeera kama ana uhakika kama kibaki kashinda uchaguzi alisema kwa kujiamini kuwa HATA YEYE HAJUI.

Hii kaulio yake imetengenzewa na tanagzzo huko kenya

huyo ndiye kivuitu hivyo ukinulisha kuwa alisomea hapa bongo naanza kufikiria mengine
 
"Akitaja baadhi ya wanafunzi wenzake sita walio hai mpaka sasa kati ya 16 waliomaliza chuoni hapo mwaka 1961, Kakuba alisema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya, Samuel Kivuitu."Ninakumbuka tulimaliza na Samuel Kivuitu, raia wa Kenya, Jully Manning (Mtanzania), Mussa Kwikima (Mtanzania), John Haminwa (Mkenya) na James Miruka (Mkenya) na hawa wote bado wako hai"hivi udsm wanatufundishaje uzalendo huyu Bwana Kwikima kwanini nayeye asingelialikwa kwenye mahafali hayo tena yupo karibu tu Tabora pale kwa wanyamwezi au ndo mambo ya Siasa kwa kuwa yule bwana toka enzi na enzi ni mpingaji mkuu wa CCM?kwa maoni yangu wangemwalika na yeye kwani kama ni uanasheria hata yeye ni lawyer pia tena ni mtoto wa kwetumnaonaje wanajamii wenzangu?????????????
Ni wazi siasa imeingizwa hapo.Inafahamika mzee Kwikima ni chama pinzani na ndicho kicho mgharimu! Hapo tunaona mapungufu ya Prf Mukandara anapoingiza siasa kwenye taaluma!
 
Back
Top Bottom