barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,858
Kwanza, ninaomba kutangaza "Conflict of Interest" katika jambo hili. Ninaandika haya baada ya kuwa mimi ni sehemu ya waathirika wa mfumo wa elimu unaotolewa na Chuo cha Ustawi wa Jamii.
Nilikuwa nina watoto watatu ambao nimekuwa nikiwasaidia kupata elimu hapo. Hawa ni watoto wa washirika na jamaa zangu waliotangulia mbele za haki. Ninapoangalia makaburi yao, marumaru, na nukuu za Biblia zilizoandikwa katika kuta za makaburi hayo, ninakumbuka ujana wetu wa pamoja na hisia za ujamaa. Ninaona deni langu kwao kutokana na maisha tuliyoishi.
Kwa kufuata ushauri wa wataalamu, nilipeleka watoto kusoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, ambacho kipo chini ya Wizara ya mdogo wangu, Dkt. Gwajima D .
Mmoja alijikita katika shahada ya kwanza ya Mahusiano Kazini na Utawala wa Umma, ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama "Industrial Relations". Mwingine alisoma elimu ya awali (Chekechea) na baadaye cheti cha ustawi wa jamii. Kwa bahati mbaya, mmoja wao alilazimika kuacha masomo na sasa yupo VETA akijifunza kupaka rangi.
Bahati mbaya, mwenye shahada ya "Labour Relations and Public Management" ameshindwa kupata ajira rasmi serikalini kwa sababu shahada hiyo haitambuliki katika "Scheme of Service". Licha ya serikali kumiliki Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama na kutoa mikopo na idhibati ya elimu, mifumo yake haiitambui shahada hiyo. Hii inawafanya wahitimu wasiajirike serikalini.
Kwa Mama Gwajima, kama msimamizi wa wizara husika, na kwa Waziri wa Elimu, naomba mshughulikie suala hili kwa pamoja ili kuwasaidia vijana hawa. Kwa nini serikali moja inakuwa na lugha gongana? Ninaandika kama mmoja wa waathirika wa mfumo huu.
Masikitiko yangu kwa chuo hiki pia ni mashaka ya ubora wa elimu. Mmoja wa watoto alikosa sifa za kuendelea na chuo kwa sababu GPA yake ilikuwa chini ya 2.0. Nilijiandaa kumpeleka VETA, lakini alinijulisha kuwa chuoni kwao, usipofikisha GPA unapewa mtihani maalumu ili ku-boost GPA na unaendelea na masomo. Je, huu ni utaratibu unaoruhusiwa?
Idara ya elimu inaonekana kuwa na matatizo. Wanafunzi wanadekezwa na management, na wakuu wa idara wanaogopa kujibu maswali kuhusu GPA ndogo na kufeli. Hii ni hatari kwa mustakabali wa elimu ya watoto na taifa kwa ujumla.
Ninaamini Waziri mwenye dhamana anapaswa kuangalia chuo hiki, kuanzia utawala hadi ofisi za wanataaluma, ili kuboresha ubora wa elimu na uhusiano kati ya kozi zinazotolewa na mfumo wa ajira wa serikali.
Ninayaandika haya kwa ajili ya wazazi wengine ambao wanapanga kupeleka watoto wao katika chuo hiki. Wajue kuwa kuna changamoto ambazo tumezipitia.
Ni matumaini yangu, Waziri husika atalifanyia kazi jambo hili.