Kumbe kiranja pinda ni jasiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe kiranja pinda ni jasiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KALABASH, Mar 28, 2011.

 1. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Katika swala la ununuzi wa mashangingi ya bei mbaya kwa ajili ya viongozi sirikali waziri mkuu Pinda alishia kulalama tu. Hakuwa na ujasiri(GUTS/BALLS? kupiga stop. Katika swala la bomoa bomoa ya Waziri Magufuli hahulalamika bali alipiga stop papo kwa hapo. Jasiri kweli kweli huyu kiranja. Au mwasemaje wana JF?
   
 2. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Ujasiri wa kifisadi!
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160

  Jibu zuri, fupi, la uhakika na linajitosheleza.
   
 4. mmzalendo

  mmzalendo Senior Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ana ujasiri wapi kwenye bomoa bomoa watu tumepigwa changa la macho, kisa cha magufuri kupigwa stop ni
  meya wa jiji la ilala kajifisadi JERRY huyo alikwenda kumshitaki magufuri dodoma kwa kiranja pinda na pinda alikuwa anamvutia speed magufuli na chato ndipo mahali alipommalizia yawezekana hana ziara ya pinda ilikuwa imepangwa kwa lengo hilo
  lengo ni kulinda mabango ya outdoor ambayo jerry na mafisadi wenzake wanayatete ili kula posho kama magufuli alivyokuwa
  ana wabeba kitu ambacho labda magufuli na watu wengine hawa mjui jerry ni kwamba huyo mtu ni hatari toka zama na ndumila kuwili tafuta watu waliomaliza PUGU form ya MWAKA 1999 kuna rafiki zake aliwafanya kitu mbaya alikuwa wanamekula naye dili ya mitihani fake jamaa alipoupata akaingia mtini, kwa stress zake akajaribu kuanza form 5 mwezi wa january 2000 badala la JULY 2000 kuwakimbia washikaji zake lakini akakwamishwa na NECTA 2001
  huyo ndiye jerry ambaye magufuli alidhani anacheza na dogo lakini huyo kwa vijiufisadi yuko juu hata huyo meye aliyepita wa ilala nina hakika alizungukwa na dogo kabla ya kujua miguu juu, na jiji la dara wasipokuwa makini watamnufaisha JERRY na watu wake wanaomtuma
  kwa kifupi pinda ni mtu wa kutumiwa tu sidhani kama ni waziri mkuu wa kutumainia
  maana ya yeye mwenyewe kukiri kwamba mafisadi ni watu hatari
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tabu kweli kweli!!!!!!!
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  ndiyo mkuu, maana katika DOWANS alisalimu amri, achana na mnafiki huyu
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hili ndio jibu lake stahili kwani huyu bwana anawaogopa sana mafisadi!!
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  leo alikuwa aongee na waandishi wa habari..je kafanya hivyo
   
 9. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Which ujasari or if I may ask Which Pinda are u referring to? If ur talking about Pinda the Premier, then something is terribly wrong with u or your assessment
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kumbukukeni kauli hii aliyoitoa mwenyewe mjengoni...............namnukuu "MAFISADI WANA NGUVU" sasa tunategemea nini hapo........
   
 11. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kama wewe ni mfuasi wake, basi utakuwa FISADI. Jamaa yako ameshanunuliwa na kuwa fisadi mkuu. Huwezi kuwa na akili timamu ukapewa madaraka ya kusimamia sheria badala yake unaanza kukwepesha sheria. Niambie Serikali ya nchi hapa Duniani ambayo inatawala bila kufuata sheria.

  Hivyo hawa viongozi wetu PINDA na KIKWETE wao wanaona ukifuata sheria unawachafua wao pamoja na Chama Chao. Serikali ya aina ndiyo nawe unaitaka?. Jiulize mara mbili kushabikia watu wa aina ya PINDA na KIKWETE.
   
 12. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jasiri kwa masilahi yake.
   
 13. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 288
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Umezipata wapi Data zako. Nawafahamu A1 wanaweza kufanya huo mchezo. Lakini kumtumia mtu mdogo kama JERRY sifikirii ungeniambia Mzee Makamba ningekubali
   
 14. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Yes I mean PINDA the Premier. If you read between the lines you will note that I am as contemptuos of his UJASIRI as you are. He was not courageous enough to put a stop on the buying of costly vehicles but at a stroke he put a stop to Magufuli's "bomoa bomoa" and publically humilliated his own teamplayer.
   
 15. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Na lilipokuja suala la albino aliishia kumwaga chock badala ya kumfuta kazi wazuri wa mambo ya ndani kwa kushindwa kuwachulia hatua wauwaji wa albino! Hata agizo la kuandikisha waua albino pia limeshia hewani! Kweli ni jasiri sana!
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MHESHIWA PINDA CHINI YA RADAR YA ALIYEWAHI KUMUAMINI: UWEZO TUNAO

  Eti umesema Mhe Peter Kayanza Mizengo Pinda aka Mtoto wa Mkulima niliyewahi kumpenda na kumuamini ni JAAAAASIRI??? Ni ujasiri gani tena huo, huyu mtoto wa mkulima nisioifahamu mie???

  Nakuambia mimi huyu mtoto wa mkulima siku hizi simuelewi kabisa juu ya lolote lile!! Na kwa kukuthibitishia hilo mwenzenu tayari nimekua nikijihesabia KUMPOTEZA KIPENZI sawa sawa na ninsi nilivyowahi kujihesabia huko nyuma nikiwa sekondari huku nikion CCM ikinilazimisha kumpoteza KIPENZI CHA ROHO YANGU KISIASA MHE AUGUSTINO LYATONGA WA MREMA (the bureaucratic rule arch-rival charismatic leader) na hivi majuzi tena nikalazimishwa KUMPOTEZA KIPENZI MWINGINE JOHN POMBE MAGUFULI kwa kukataliwa kuzingatia sheria mstari kwa mstari kwenye utendaji wake.

  Nakuuliza mwenzangu ni ujasiri gani huo ulioigundua kwa huyu aliyewahi kuwa Mtoto wa Mkulima huko nyuma na sasa hivi kabakia tu kuwa Mtoto wa walima bustani ya mchicha Mto Msimbazi Dar es Salaam??

  Hakika ili niweze kumtendea haki katika kuanza kwangu kumkataa kule kwanza kulitokea azimio nzito sana katika kikao cha kukata na shoka ambapo wahudhuriaji walikua ni akina (1) Uwezo Tunao mwenye Kupenda, (2) Uwezo Tunao akili na fikra pamoja na (3) Uwezo Tunao jicho la walalahoi. Mkutano huu wa zaidi ya wiki ulikua mkali kweli kweli tena wenye futa nikuvute mkubwa mno.

  Lakini labda nianze kwa kuwashukuru sana tena sana ndugu zangu wengine hawa (Uwezo Tunao family) kwa kuafiki mapendekeza ya huyo mjumbe wa pili hapo juu ya kwamba kwanza tufanye utafiti utakaotuelekeza kama kweli bado kuna matumaini yamebakia ndani ya Baba huyu 'Mtoto wa Mkulima' hadi hapa tulipofikia au laa. Katika kutekeleza azima hiyo sote watatu tulichagua kujipa siku 90 kumsoma juu ya kauli zake na kwa kiasi gani zinavyokubaliana na matendo yake katika jamii yetu hii.

  Kiukweli kabisa, japo MATOKEO YA UTAFITI WA UWEZO TUNAO FAMILI NA HATIMA YA MHESHIMIWA PINDA A.K.A MTOTO WA MKULIMA utakamilika hapo Aprili 23, hata hivyo dalili za awali hazimpendelei saaana huyu kipenzi changu ambaye nasikitika kuelekea kumpoza hivi karibuni katika kitabu changu cha Wanasiasa ninaowaamini nchini.

  Hizo dalili za awali zisizompendelea huyu 'rafiki wa roho yangu, mara baada ya kumsogeza kwa karibu zaidi chini ya drubini yangu kwenye maabara binafsi ya siasa nchini (microscope) kumebainika mambo kadhaa wa kadhaa juu yake huyu mwenzetu. Na endapo dlili hizi zenye gizo totoro hazioonekana kupona kitu basi nawahakikishieni kwamba sitochelewa kupendekeza hapa JF na kote nchini kwamba hicho cheo cha heshima cha 'Mtoto wa Mkulima' nacho tukamnyang'anye kabisa kwa kutoitendea haki ipasavyo.

  Kwa mwenzetu, ndugu yetu na Baba yetu wa Taifa Mwalimu Nyerere cheo kile cha heshima toka kwetu wananchi aliendelea kukitumikia hadi dakika ya mwisho aliposema maneno mawili mtatu kwa Mzee Rashidi Simba wa Vita pembeni mwa kitanda chake hospitalini kule Uingereza hivyo hata akaendelea kustahili kubakia nayo hata baada ya safari ya kurudi kwa muumba wake ilipowadia.

  Mapungufu mazito tuliyoyaona ni haya na ni bora akayafanyia kazi kwa haraka kabla hatujafunga faili na kuikabidhisha kwa wapiga kura kumpima nayo zaidi pamoja na kwamba keshaahidi kurudi kupumzika nyumbani mara baada ya utumishi wake kama Waziri Mkuu, Mheshimiwa Pinda ni:

  1. Kiongozi anayeogopa sana LAWAMA:

  Hii tabia imegeuka kuwa jela yake binafsi anayotembea nayo kila mahali kama mfungwa wa hiari. Kwa kukuthibitishia madai yangu haya utagundua kwamba Mhe Pinda siku zote hajawahi kuonyesha OWN INITIATED ACTION BALI NI MZEE WA REACTIONS tu. Nasema akome kukimbizana na upepo kwa mtindo wa zimamoto kwa kila atendalo.

  2. Mtaalam wa Kukasimu Madaraka, Mchovu wa Kufuatilia:

  Delegating power is a very good sign of a leader who has confidence in colleagues and teamwork spirit. Lakini kama huna muda wa kufuatilia ulioyakasimu, wala uwezo wa kuhakikisha kwamba kweli ulioyakasimu yanaleta matunda ya kugusika kwa mikono na kuonekana kwa macho basi mwenzetu ukae ukijua kwamba wengi huku nje wanajiuliza kiti hicho unachokalia unakiachia wazi lini???

  Uthibitisho wa madai yangu; Mzee Pinda alijichagulia kuparamia swala nyeti la Madai ya Katiba nchini na kwa kuelewa kwamba anayo GOODWILL kwetu sie walalahoi tulio wengi basi akaona vema kuchangamkia tenda hiyo.

  Lakini, kwa bahati mbaya sana 'Wa Mkulima ' hajagundua siri kwamba goodwill ni goodwill tu na inayo ukomo wake na kwamba kitendo cha kuuchukua swala la katiba na kujirithisha kuuficha ndani ya mfuko wake wa suruali ya nyloni ni jambo la hatari kuliko angeliacha tu swala hili bila kuahidi kulishughulikia kabisa.

  Katika hili nasema Mhe Pinda usiombe mtu na au kundi la watu waliyokumini pindi wanapogeuka na kukosa imani kwako - mungalie Ndugu yetu Mhe Kikwete na jinsi alivyotuchukulia for granted imani yote kwake na kura zote katika kipindi chake cha kwanza mpaka akafika mahala na kuona kwamba tuliomuamini baada ya kutusaliti basi ni bora akatumie njia ya mkato KUTUIBIA KABISA KARU nadhani lengo likiwa ni kupata SECOND CHANCE kurekebisha mambo lakini ndio hivyo maji ya kunywa yakishamwagika bora ukayapigie tu deki.

  Mheshimiwa Pinda kwa taarifa tu ni kwamba 'Nguvu ya Umma' tunasubiri kwa hamu kuona endapo tena utaipigia danadana swala la Katiba Mpya na Mtume huru za Uchaguzi; Bara na Visiwa hata isipitishwe kwenye bunge hili la mnamo mwezi huu wa April 2011!!!!

  3. Group Thinking

  Mheshimiwa Pinda ni muumini mkubwa wa kanisa au msikiti wa maamuzi ya kikundi kundi hivi. Hili jambo linampa shida sana kwa kuwa kila mara anakosa ORIGINALITY katika msururu wa mambo ya kutekeleza hivyo jambo linapoenda kombo anashindwa kulitafutia lango la pili kwa kuwa he is NOT never married to the original idea either.

  Kwa mtindo huu 'Wa Mkulima' ni kwamba utajikuta siku zote unageuka kuwa MTUMWA WA FIKRA ZA WASHAURI ambao pindi mambo yanapoharibika wao hucheka mtindo wa Jino-Pembe kwa kuwa siri yote wanayo kwamba wewe hauna input yoyote mle na kwamba hata zile perspective mikanganyiko walizokupa washauri mbali mbali wala haukuweza hata kujitengea muda wa peke yako with a BRUTALLY CRITICAL MIND.

  Kama uliwahi kusikia Mheshimiwa Mwl Nyerere, Mkapa, Dr Shein na Dr Magufuli walipata kuheshimika sana ni kule katika wao kujitengea muda usioingiliwa hata na mama watoto pale nyumbani ili AKALIFIKIRIE TAIFA LAKE KWA UDHATI KABISA NA MOYO WA KIZALENDO ili ku-Question, kuomba ufafanuzi zaidi, uthibitisho wa maelezo na hata kule kufanya SUPRISE SELF-FACT FINDING MISSION bila kuwa pompus anda embarrassing to others kama Vijikamati Vya Bunge tunavyovishuhudia hivi leo viki-play both Police and Court roles together on their subordinate line ministries and related institutions whereas the costitution ONLY asks the to Oversee and Advise.

  Wakati bado utafiti wetu juu ya Mtoto-wa-Mkulima na hasa kwa kumpima zaidi atakavyoshugulikia jambo la msingi zaidi kwa taifa (an immediate People-Centred Constitutional Overhaul call) au kuyaacha kwenye mikono ya wachache akina Oliver Mhaiki na Celina Kombani au atawaita wadau wote kuliweka sawa kabla ya kutinga nayo bungeni Aprili, mambo mengine yatakayoendelea kuangaliwa kwake ni pamoja na:

  a. Pinda Leadership style and frame (Theories X and Y tools).

  b. Whether Pinda is already at the Plateaue of his performance or not (Goal-setting & Abraham Maslow's Theory of Needs)

  c. Jibu kama Mhe Pinda ni Innovative, Proactive or not

  ... na mjadala wa Uwezo Tunao family bado unaendelea juu ya kiongozi huyu kabla ya kuingia kwenye kuwachambu with a brutally critical mind mtu yeyote ambaye amewahi kutajwa kutamani kuwa kiongozi wetu ama wa kisiasa au technocrat kinamna fulani hivi.

  Nyote mnakaribishwa kwenye huu mkutano endelevu wenye lengo la kukosoa hadi wale tunaowapenda ndani ya CHADEMA chenyewe ili kila mmoja aweze kupata marejesho jinsi tunavyomuona na mambo gani yafanyike huruka vihunzi kadhaa kuelekea kwenye mafanikio maridhawa kwa Wa-Tanzania tulio wengi.
   
Loading...