Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,045
- 33,528
Kitendo cha Sheikh Khalifa Khamisi kusema kwamba waislamu waliisaidia CCM kwenye uchaguzi wa Mwaka jana kwa kuitoa "ICU" kinafuta kebehi zote alizotupiwa mwanasiasa Pekee Mkongwe aliyepo hai mpaka sasa Mzee Kingunge Ngombare Mwiru, kwamba alikosea aliposema kwenye uchaguzi huo kuwa CCM imekata pumzi.
Kama Sheikh Khamis anaona kwamba CCM ilikuwa chumba cha wagonjwa mahututi kwenye uchaguzi wa Mwaka jana, basi ni lazima iwepo sababu iliyoiipeleka CCM "ICU". Bila ya shaka CCM ilipokata pumzi mojawapo ya hewa ya Oksejeni iliyowekewa ni msaada toka kwa viongozi wa dini ya Kiislamu iliyoisadia CCM kupata kura toka kwa waumini kwa kiislamu.
Ningeshangaa sana kama Mzee Kingunge na uzowefu wake wote wa kisiasa alio nao aseme kitu ambacho hakina ukweli ama mantiki. Kwa jicho la tatu Gwiji hilo la siasa liliona CCM imekata pumzi. Kumbe udhaifu ulikuwa ni kwa UKAWA kushindwa kuizuia CCM isipelekwe ICU kwenye kuwekewa Oksjeni na kina Sheikh Khalifa!!
Mzee Kingunge, Umetisha!!