Kumbe kesi ya DOWANS nyanya tu ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe kesi ya DOWANS nyanya tu !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tarita, Jan 25, 2011.

 1. t

  tarita Senior Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nawaza hivi, kama anayetajwa kuwa mmiliki wa KAMPUNI YA KITAPELI ya RICHMOND, anashitakiwa na serikali kwa kuitapeli na kuisababishia hasara kubwa-Mohammed Gire, je imekuwaje Gire kusaini mkataba halali na Dowans uliyoiwezesha Dowans kuwa halali kibiashara hapa nchini?!!
  Kumbe kweli serikali hii hatari. Aibu tupu.Hii kesi alishindaje DOWANS? Je mwanasheria Mkuu wa serikali anaelewa kwamba anamshitaki Mohammed Gire kwa utapeli? Sasa inakuwaje hata RICHMOND INA MGAO wa hizo fedha, je hizo fedha atapewa nani ? Je ni Mohammed Gire ndiye atakayelipwa?!
  Nchi hii kweli ni ya wadanganyika. To hell with you Rostam.SIJAPATA KUJISIKIA VIBAYA KAMA LEO LILIPONIIJIA WAZO HILI.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hawajali kwa sababu wana msemo ule kwamba watanzania ni watu wakusema sema sema tuu,watasema halafu watasahau,kwani wewe umeona kesi ya GIRE pale kisutu imetajwa tena jiulize mwenyewe na huku tunasema tunainvestigative journalist ni manyanya pia si mpaka sasa wangesha tafiti hiyo connection kinyaa kabisa puu nchi imeliwa hii
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana, usiwaze sana. elewa hawa ndo aina ya viongozi tulionao, Kumbuka kwamba kwenye haya mambo, including lile sakata la radar, walitumiwa wanasheria wakuu hawa hawa ku-make sure kwamba iki-back fire, haiwezi kuwarudia, wanakuwa wamefanya utafiti wa kisheria na ku-analyze way out.......hata kama sio sahihi sana, kwa vile wapo kwenye power hiyo alternative route ndo inatumika.

  Hili ndilo lililotokea kwa Richmond. Ndilo litakalotokea kwa Rdar as well. Hili Linchi ni muozo kabisa.
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,717
  Trophy Points: 280
  grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Give me a break kiongozi anaonyesha njia hawa ni watawala wamepora dhamana ya wananchi kwa ajili ya maslahi yao. Labda tujichunguze; kweli hatuna uwezo wa kuzuia huu upumbavu?
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  utakufa na pressure bure kaka angu, ukianza kufikiria uozo wa nchi hii. we tafuta chako kula n life goes on
   
 7. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Ni vyema umeamka ingawa na hasira zisizokuwa na muhimu hapa. Na sijui kwa nini tunahangaika na mjadala huu. Wenye dhamana ya serikali wakiamua kuliibia taifa, si rahisi kuwadhibiti kwa kutumia taratibu za kawaida - wao ndio wenye madaraka ya kutumia mifumo ya serikali, sheria na taratibu zake. Hili la Dowans, tunaibiwa na serikali yetu kwa dhamana tuliyowapa viongozi wetu - sio watu wa nje kama tunavyojidanganya. Sakata la rada, SFO walitufungua macho: serikali yetu haina maslahi na mkwanja BAE Systems waliokubali kuturudishia. Husikii (toka serikalini) mdadi wa kudai wala ahueni ya kurejeshewa chetu. Hata kwa Dowans unawaona wanavyohaha jinsi ya kujikabidhi mkwanja huo bila kulaumiwa. Tusipokuwa na namna ya kuwaondosha madarakani, tusipoteze muda kujadili wanavyojichana kwa rasilimali zetu bila hiyana.
   
 8. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  You are right Carmel. Lakini wakulu hawa wanapenda sana kuisikia kauli ya aina hiyo inayowatuliza wa-Tanzania wasidanganyike kufikiri kuna namna mbadala; wasisikilize mtu au chama chochote kinachowaambia kuna uwezekano wa kubadilisha hali toka kwenye uozo uliopo. Waendelee kuchangamkia fursa za kifisadi hata kama wanaambulia punje za karanga. Ndio maana Sophia Simba alidiriki kusema ndani ya CCM hakuna msafi. Lakini tusijidanganye, ipo siku tutalazimika kubadili hali hii hata kwa vilio kwa sababu si endelevu.
   
 9. minda

  minda JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ukiwaza sana nguruwe kala nini au kafanyaje, amin huli kiti moto!

  i will pretend nothing happened. god bless tanzania.
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kesi ya Gire hata bado haijaisha lakini ya Dowans imepita kwa supersonic speed...
   
 11. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,081
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hufikirii kuhusu kizazi kijacho cha watanganyika? Wajukuu wako watarithi nini? "Tafuta chako kula"?? kipi hicho? kuna raha gani kushiba wakati mamilioni ya waliokuzunguka wanakufa njaa? "Life goes on"? What life? You mean this one without electricity,bidhaa bei juu, trafic jam,ufisadi na karaha zote hizi? Bora kufa kwa pressure lakini ufumbuzi upatikane kuliko kukubali kuwa mnyonge eti life goes on.
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bongo si mchezo, kwenye ulaji watu hawalazi damu, mabadiliko ni muhimu kabla hawajamaliza kila kitu!!!!!
   
 13. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  hizi ndo fikra chafu tusizozitaka...kama kila mmoja akiwa na dhamira kama yako kweli tutajikwamua kutoka kwa hawa mafisadi?
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Me natoa angalizo tuu kwa huyu RA kuwa na ulinzi la sivyo mtamkuta kalala kwa gari hapo kwa traffic Rights ipo siku na tunako kwenda au kuburuzwa kama wasomali walivyo watenda wa America kwa Somali land ndio itakvyotokea kwa RA siku za mbeleni wananchi watachoka sasa kwa hizi habari jinsi muda unavyo kwenda kwa kasi ndio serikali inachemka na kushindwa kuwawajibisha wahusika na kuiacha nchi ikiingia kwa janga la ajabu hii hali twaiongea sasa ni inakuja tena mbaya sana ila ikitufikia ndio tutaijua vyema na kuheshimu madaraka na utawala kwa wananchi tunao watawala na kuwa na machungu na nchi yetu

   
 15. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  M just curious!:shock:
   
 16. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena wahandishi wetu si lolote hawana utafiti wa kina kabisa wanakurupuka tu
   
Loading...