Kumbe Katibu Mkuu CCM analipwa Mil11 kwa mwezi

hahaha...hawa watu ni WAPUMBAVU kupita kiasi! Ivi wanaweza kuwa viongozi wetu?
 
Hao wavimba macho tu, kwanza dk. Slaa kwa kazi aifanyayo nahisi anapunjwa, angepata zaid km anavyostahili!
 
Jamani,

Ninavyojua mimi katibu mkuu wa ccm haingii bungeni kwa wadhifa wake. Makamba aliingia baada ya kuteuliwa na JK kama mbunge. Hivyo Mukama kwa sasa hawezi kuingia mjengoni kwa kofia ya U-katibu wa ccm. Labda tena amwombe JK amteue kwenye zile nafasi 7 zilizobakia.
 
Si Kweli! Katibu Mkuu wa CCM wa sasa sio MBUNGE na haingii Bungeni. Mzee Makamba aliweza kuingia Bungeni baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge na Rais kupitia viti 10. Mzee Mukama hana uteuzi huo na hivyo hana stahili zozote za ubunge.
 
Je kuna uthibitisho juu ya hii Millioni 11 ya Mukama au Millioni 12 ya Slaa? Njia moja ya kupata uhakika ni kufanya mapitio ya fomu za maadili. Je tumefanya hivyo? No research no right to speak!
 
Kuna kitu muhimu sana ambacho watanzania tumekisahau baada ya Dk Slaa kuhojiwa na mwandishi mmoja wa habari mwaka jana baada kupinga mishahara mikubwa ya wabunge.

Mwandishi huyo (Jina lake silikumbuki) alimmuuza Dk Slaa, 'Kama unaona mshahara wa wabunge ni mkubwa mbona bado na wewe unaupokea?'. Dk Slaa alijibu kwa ufasaha kabisa kwamba yeye anaupokea mshahara ule kwa kuwa ndio anaoutumia kuzunguka nchi nzima kuwataja mafisadi. Kazi ambayo hakika bado anaifanya hadi leo licha ya kuwa nje ya bunge.

Mi binafsi sioni nongwa kwa Slaa kulipwa huo mshahara kwa kazi kubwa anayoifanya. Lakini swali la kujiuliza, Wilson Mukama analipwa Milioni 11 kwa kukaa tu ofisini, je hii ni sawa?

Maana hata katika puyanga wanayoifanya kina Nape Nnauye huko mikoani yeye simuoni kabisa.

Mi nasisitiza Dk Slaa angozewe mshahara kwa kuwa kazi anayoifanya ni kubwa. Kutaja mafisadi tena na ushahidi juu na wahusika wakikwama kwenda mahakamani si kazi rahisi.

Slaa, Big up my President!
Kweli ndugu mimi nafikiri mshahara wa Dr. ni kidogo sana ukilinganisha na kazi anayoifanya nafikiri ni bora akaongezewa. Kwani hayo manyagau yanalipwa shilingi ngapi? nani aliwahi kuwahoji kuhusu mishahara ndani ya chama chao cha magamaba? Waache kutufanya watz kama wajinga tusiejua nani mkweli na nani mwongo.
 
Kuna kitu muhimu sana ambacho watanzania tumekisahau baada ya Dk Slaa kuhojiwa na mwandishi mmoja wa habari mwaka jana baada kupinga mishahara mikubwa ya wabunge.

Mwandishi huyo (Jina lake silikumbuki) alimmuuza Dk Slaa, 'Kama unaona mshahara wa wabunge ni mkubwa mbona bado na wewe unaupokea?'. Dk Slaa alijibu kwa ufasaha kabisa kwamba yeye anaupokea mshahara ule kwa kuwa ndio anaoutumia kuzunguka nchi nzima kuwataja mafisadi. Kazi ambayo hakika bado anaifanya hadi leo licha ya kuwa nje ya bunge.

Mi binafsi sioni nongwa kwa Slaa kulipwa huo mshahara kwa kazi kubwa anayoifanya. Lakini swali la kujiuliza, Wilson Mukama analipwa Milioni 11 kwa kukaa tu ofisini, je hii ni sawa?

Maana hata katika puyanga wanayoifanya kina Nape Nnauye huko mikoani yeye simuoni kabisa.

Mi nasisitiza Dk Slaa angozewe mshahara kwa kuwa kazi anayoifanya ni kubwa. Kutaja mafisadi tena na ushahidi juu na wahusika wakikwama kwenda mahakamani si kazi rahisi.

Slaa, Big up my President!

na nimepata habari et dr wakat wote wa ubunge wake hakuwah kuwa na usafiri, na alionao sasa amepewa na chama baada ya uchaguz. Je ni kweli?, au ndo mana alikua akija bungen anaish opposite na bunge (hotel fifty six) kukwepa adha za usafiri?.
 
Haijaandikwa popote, isispokuwa JK alimteua Makamba, pamoja na kwamba kila mtu halijua kuwa hakuna sifa yoyote ya kuwa mbunge. Kwa kipindi chake nakumbuka alichangia mara mara moja tu. Kwa sasa JK bado ana nafazi saba za kuteua wabunge

hiv Makamba alivyoteuliwa kuwa mbunge nini alifanya kwa maslah ya taifa?, au alipelekwa akaendelee kula posho na mshahara?.
 
Lakini akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Nape aliwataka Chadema kutoa ushahidi unaoonyesha kuwa alihusika na ufisadi wa EPA. "Atoe ushahidi hadharani, unajua hawa watu ni waongo, hata Watanzania watawashangaa," alisema Nape.

Kuhusu suala la kuhamia katika chama hicho, Nape alisema: "Tena uandike kabisa, mimi ndiyo ninao ushahidi wa wao kunitaka nikagombee kupitia chama chao nikakataa, kwa sababu siwezi kuhamia kwenye chama cha Wachagga, kile ni chama cha ukoo," alisema Nape.

Lakini akijibu hoja hiyo Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara kulingana na daraja la viongozi na hurekebishwa kama watendaji wengine serikalini.

"Katibu Mkuu wetu analipwa Sh1.5 milioni na hukatwa kodi. Vilevile hulipwa posho isiyokatwa kodi ya Sh300,000. Hayo mengine ya usafiri ni mambo ya kawaida tu. Usafiri anao na hulipiwa umeme wa LUKU na nyumba. Siyo suala la kificho hilo," alisema Nape
 
Wakuu tukumbuke kuwa Katibu mkuu wa CCM:
1.Hulipwa mshahara wa Ukatibu mkuu na marupurupu mengine ya kichama na hutumia usafiri wa ...Chama.
2.Katibu mkuu wa CCM huingia Bungeni kutokana na cheo chake,ina maana hapo tena hulipwa ...Mshahara kama Mbunge na Posho zote za ...kibunge na mkopo wa usafiri wa wabunge

Ukipiga hesabu hapa ina maana Katibu Mkuu huyu kwa Mwezi huingiza pesa nyingi sana.

Fafanua. Makamba aliingia Bungeni 2005 - 2010 kama Mbunge wa Kuteuliwa na Raisi kwenye zile nafasi 10 na si kwa cheo chake. Mkama hajateuliwa mpaka sasa hivyo hawezi kuingia Bungeni kwa cheo chake
 
Kazi ipo kumbe watendaji wote wakuu wa CCM na Chadema ni mafisadi kwa mujibu wa mishahara yao kama kweli kauli zinazotolewa ni sawia
 
Hivi ni wapi ambapo mtu anaanza kazi kabla hajajua mshahara? Hata housegirl ukimwajiri mnakubaliana mshahara ndio anaanza kazi inakuwaje Mkama asijue wa kwake? Kweli huu ndio uhuni. Naye Nape atueleza mpaka leo wilaya kamwaachia nani? Mipango ya maendeleo wilayani kwake anasimamia nani? Kwanini tusimwite mtoro kazini, nakumbuka kuna sheria inasema wafanyakazi waandamizi wa serikali hawaruhusiwi kufungamana na chama cha siasa kwa Nape inakuwaje?
 
Sasa kusoma kuna faida gani!

Kama unamkuta mtu mwenye elimu yake, ameajiriwa halafu hajui Mshahara wake ni kiasi gani, je kuna sababu ya kusoma kweli!

Kama mpaka Kibarua anajua Stahili yake, leo hii mtu mwenye ajira inayoeleweka, yenye kukatwa kodi, NSSF, n.k hajui anacholipwa!

Kweli hili ni Zuzu! Sasa atawasaidiaje Wananchi kupata haki zao kama hata Stahili zake mwenyewe hazijui!

Kweli hili nalo ni GAMBA!
 
hahaha,niguse bahati mbaya nikupige makusudi!
sasa nape kaona m7 kubwa kumbwe mwenzake anapewa m11 duh,...
 
CCM warejeshe viwanja vyetu - Kirumba, Jamhuri (Moro), Jamhuri (Dom), Sokoine (Mbeya), Ali Mwinyi (Tabora) etc etc
 
ccm wazee wa magamba hamuiwezi ngoma ya Chadema mlianzisha kelele kuwa mnajua mbona mmesepa,mshahara wa kiongozi kuwa ni siri ya mtu hapo patakuwa na tatizo(ufisadi)wakati sisi tunalalamika huku mitaani juu ya ugumu wa maisha nyie kazi yenu kutuibia wananchi
 
Naye Mabere Marando alikituhumu CCM kuwa kinamlipa Katibu Mkuu wao Sh 11 milioni kwa mwezi
Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya Marando, Mukama alikataa kutaja mshahara wake akisema kuwa ni siri yake.

Jamani honestly speaking mimi ninafikiri mtu ukiwa mwana CCM basi hata uwezo wa kufikiri unapotea. I can conclude that CCM IS A MENTAL DISEASE. Eti Mukama hajui mshahara wake kwakuwa hajapokea (SIC).

Hivi jamani ni mtu gani unaweza kuanza/kuajiriwa kazi bila kuambiwa/kuuliza mshahara wako ni kiasi gani? Huyu Mukama anafikiri watanzania wote hatujawahi kuaajiriwa?

Mimi house girl wangu kabla ya kuanza kazi aliniuliza boss utanilipa sh ngapi kwa mwezi? nikamwambia Tsh 60,000/= @ month. Ndipo akaanza kazi. Kama huyo binti wa STD VII aliweza kuniuliza mshahara wake kabla ya kuanza kazi leo Mukama eti ameanza kazi hata mshahara wake haufahamu?! Jamani nchii hii ina vituko. Je huyu ndiyo kweli katibu mkuu ambaye CCM wanategemea awaongoze kwenye karne hii teknohama?

Kama alishindwa kuuliza mshahara wake, je hata job description yake kweli anaifahamu? Ama kweli la kuvunda halina ubani.
 
kwa mafisadi hao wa ccm imeaandikwa wapi kwamba wanauhusa ya kutuibia?
kila kilicho kwenye fikra za MWENYEKITI wa chama ni sahihi kwa ccm
hicho ni chama kisichofuata maandishi ila ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI

Wakuu tukumbuke kuwa Katibu mkuu wa CCM:
1.Hulipwa mshahara wa Ukatibu mkuu na marupurupu mengine ya kichama na hutumia usafiri wa ...Chama.
2.Katibu mkuu wa CCM huingia Bungeni kutokana na cheo chake,ina maana hapo tena hulipwa ...Mshahara kama Mbunge na Posho zote za ...kibunge na mkopo wa usafiri wa wabunge

Ukipiga hesabu hapa ina maana Katibu Mkuu huyu kwa Mwezi huingiza pesa nyingi sana.

Heee ni wapi imeandikwa kwamba katibu mkuu huingia bungeni kwa cheo chake? Huenda una hoja kwa kuwa umetoa angalizo kwa wekundu. Tusaidie hoja hapa au Mukama naye anandaliwa kuteuliwa kuwa Mbunge? Hivi JK hajamaliza zile nafasi zake kumi za akina Nahodha, Meghji na Mbarawa?
 
Back
Top Bottom