Kumbe Katibu Mkuu CCM analipwa Mil11 kwa mwezi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Naye Mabere Marando alikituhumu CCM kuwa kinamlipa Katibu Mkuu wao Sh 11 milioni kwa mwezi
“CCM wanapigia kelele mshahara wa Dk Slaa, mbona Mukama (Wilson) analipwa Sh11 milioni watu hawasemi? Mbona Rais Jakaya Kikwete analipwa posho mbilimbili, ofisi yake iko Dodoma, lakini akienda huko analipwa posho, akirudi Dar es Salaam analipwa,” alisema Marando.
Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya Marando, Mukama alikataa kutaja mshahara wake akisema kuwa ni siri yake.
“Mimi leo ndiyo natimiza mwezi mmoja tangu niingine ofisini, hata mshahara wenyewe sijauona. Mshahara ni siri yangu mwenyewe, nimeingia hapa baada ya kustaafu kwa hiyo ndiyo hivyo, naomba msiniingize kwenye hizo ‘debate’ (malumbano)” alisema Mukama.
 
..........Chadema imesema Nape ni vuvuzela anayecheza ngoma asiyoijua na mtu asiye na msimamo na kumtaka ajibu mambo ya msingi yakiwemo Katiba mpya na kupanda kwa gharama za maisha.

Marando alisema, CCM imelenga kuhamisha hoja ya ufisadi na kukwepa kujibu hoja za msingi na kwamba, Nape hana hadhi ya kuinyooshea kidole Chadema kwa kuwa si mtu makini mwenye ajenda ya wananchi.

“Tuna ushahidi wa kutosha kuwa Nape ni mmoja wa watu walionufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia kwa (anatajwa mfanyabiashara maarufu) ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya Kamati ya Rais,” alisema Marando na kuongeza:

“Alitumia fedha hizo katika kampeni zake za kusaka uongozi ndani ya chama chake.”

Akizungumzia ununuzi wa magari ya chama kutoka kwa Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Marando alisema, magari hayo si chakavu na hayajawahi kukutwa gereji na wala si ya kubebea mchanga wala kokoto, bali ni mitambo maalumu ya kampeni na kwamba, CCM inawaonea wivu kwa kuwa hawana mitambo hiyo.

Alisema, mitambo hiyo ina nguvu kuliko ilivyo mitambo ya kufua umeme ya Dowans na ilinunuliwa na Mbowe kwa ajili ya biashara zake, lakini kutokana na umuhimu wake, chama kiliazimia kwa nia moja kumuomba yatumike kwa kazi hiyo na alikubali.

Alimtaka Nape aache kusema ana taarifa za siri kuhusu chama hicho kwa kuwa hakuna mwanachama anayelalamika juu ya magari hayo kwani zimo katika taarifa za fedha za chama hicho ambazo kila mjumbe aligawiwa.

Kuhusu tuhuma za mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, Marando alisema hajawahi kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hizo cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyoueleza umma.

Source: Habari leo.
 
Sasa huyu poti (Mukama) anajichanganya mwenyewe... mara ooh sijui nalipwa kiasi, ndio kwanza nina mwezi mmoja... mara oooh mshahara ni siri yangu! Ongea mwanamume si unatoka mkoa wa wanaume?!

Duuh, kwa mshahara wa Dr. Slaa na CDM yake cha mtoto!!! Mukama analipwa kama expatriate/consultant toka South Africa!!!

Halafu akivuliwa gamba, anapewa shangingi kama Makamba senior!!!!
 
Ina maana Mukama kapewa kazi hajui analipwa shilingi ngapi?
kwani yeye ni katibu mkuu wa kwanza katika chama?
yeye naye ni zao la mafisadi
hao ni kina sokwe , RACHEL na Mkono
wamemuweka hapo wa poti kulinda maslahi yao
wao wanaona wamecheza kwamba huyo hatuta shituka ni mtu wao
JK mwenyewe anafanya kazi kwa AMRI za EL na mzee wa kikofia chekundu ndiye
mwanasheria wao wa mambo machafu
KATIBU MKUU WA MAGAMBA= RACHEL=JK=MAMBO BINFSI YA RACHEL & JK= MLINDA UFISADI
 
Mmmhhh wa Obama unajulikana we kwa nini unaficha wako??? Au sababu unaelewa unachopata si haki...
 
Wakuu tukumbuke kuwa Katibu mkuu wa CCM:
1.Hulipwa mshahara wa Ukatibu mkuu na marupurupu mengine ya kichama na hutumia usafiri wa ...Chama.
2.Katibu mkuu wa CCM huingia Bungeni kutokana na cheo chake,ina maana hapo tena hulipwa ...Mshahara kama Mbunge na Posho zote za ...kibunge na mkopo wa usafiri wa wabunge

Ukipiga hesabu hapa ina maana Katibu Mkuu huyu kwa Mwezi huingiza pesa nyingi sana.
 
Wakuu tukumbuke Makamba alivyokuwa Bungeni alipewa Mkopo wa Gari kama wabunge wengine na Baada ya kuachia Ukatibu mkuu bado kapewa usafiri(Shangingi) jipya kama asante.Na imani bado kachukua kiinua mgongo cha ubunge wa kuteuliwa na Raisi na Bado kachukua kiinua mgongo cha ukatibu mkuu.
 
Nadhani sasa CDM na wananchi kwa ujumla tuwaforce CCM nao waanike hesabu zao, wao wanadandia tu vya wenzao badala ya kuweka comparison. Kama wanaona Slaa analipwa sana basi waseme viongozi wao wanalipwa kiasi gani?

Halafu huyu Mnauye bila shaka anaendelea kupokea mshahara wa mkuu wa wilaya wakati hayupo kituo cha kazi, huu sio tu Ufisadi bali pia ni Utapeli na ni kosa la Jinai. CDM/wanaharakati can follow-up ili ashitakiwe kwa kuiibia serekali.
 
ahahah mimi na furahi sana napo waona ccm wanajichanganya wenyewe au wanafanya jambo alafu lina warudia wenyewe
 
Kuna kitu muhimu sana ambacho watanzania tumekisahau baada ya Dk Slaa kuhojiwa na mwandishi mmoja wa habari mwaka jana baada kupinga mishahara mikubwa ya wabunge.

Mwandishi huyo (Jina lake silikumbuki) alimmuuza Dk Slaa, 'Kama unaona mshahara wa wabunge ni mkubwa mbona bado na wewe unaupokea?'. Dk Slaa alijibu kwa ufasaha kabisa kwamba yeye anaupokea mshahara ule kwa kuwa ndio anaoutumia kuzunguka nchi nzima kuwataja mafisadi. Kazi ambayo hakika bado anaifanya hadi leo licha ya kuwa nje ya bunge.

Mi binafsi sioni nongwa kwa Slaa kulipwa huo mshahara kwa kazi kubwa anayoifanya. Lakini swali la kujiuliza, Wilson Mukama analipwa Milioni 11 kwa kukaa tu ofisini, je hii ni sawa?

Maana hata katika puyanga wanayoifanya kina Nape Nnauye huko mikoani yeye simuoni kabisa.

Mi nasisitiza Dk Slaa angozewe mshahara kwa kuwa kazi anayoifanya ni kubwa. Kutaja mafisadi tena na ushahidi juu na wahusika wakikwama kwenda mahakamani si kazi rahisi.

Slaa, Big up my President!
 
Mukama ameomba kutoingizwa katika 'debate' zetu. Mshahara wenyewe hajauona na kaingia pale baada ya 'KUSTAAFU'
Kustaafu bongo ni nini jamani?
 
Wakuu tukumbuke kuwa Katibu mkuu wa CCM:
1.Hulipwa mshahara wa Ukatibu mkuu na marupurupu mengine ya kichama na hutumia usafiri wa ...Chama.
2.Katibu mkuu wa CCM huingia Bungeni kutokana na cheo chake,ina maana hapo tena hulipwa ...Mshahara kama Mbunge na Posho zote za ...kibunge na mkopo wa usafiri wa wabunge

Ukipiga hesabu hapa ina maana Katibu Mkuu huyu kwa Mwezi huingiza pesa nyingi sana.

Heee ni wapi imeandikwa kwamba katibu mkuu huingia bungeni kwa cheo chake? Huenda una hoja kwa kuwa umetoa angalizo kwa wekundu. Tusaidie hoja hapa au Mukama naye anandaliwa kuteuliwa kuwa Mbunge? Hivi JK hajamaliza zile nafasi zake kumi za akina Nahodha, Meghji na Mbarawa?
 
Ni kweli bwana MKAMA analipwa m11 Kwa Mwezi,ni mtu mmojawapo mwenye dhuruma na mali za watanzania
 
Heee ni wapi imeandikwa kwamba katibu mkuu huingia bungeni kwa cheo chake? Huenda una hoja kwa kuwa umetoa angalizo kwa wekundu. Tusaidie hoja hapa au Mukama naye anandaliwa kuteuliwa kuwa Mbunge? Hivi JK hajamaliza zile nafasi zake kumi za akina Nahodha, Meghji na Mbarawa?

Haijaandikwa popote, isispokuwa JK alimteua Makamba, pamoja na kwamba kila mtu halijua kuwa hakuna sifa yoyote ya kuwa mbunge. Kwa kipindi chake nakumbuka alichangia mara mara moja tu. Kwa sasa JK bado ana nafazi saba za kuteua wabunge
 
Back
Top Bottom