Mbochong'a
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 770
- 1,315
Moja kwa moja kwenye mada. Kuna dogo wa form three amekuja hapa job kwa kaka yake akamsimulia yaliyo mkuta baada ya kutapeliwa simu pamoja na pesa.
Ilikuwa hivi. Dogo anaseme, ameshuka kituo cha daladala cha stesheni akitokea Mbagala. Baada ya kushuka tu, akatembea kama mita tatu akakutana na dingi mtu mzima fulani miaka 55 hakosi. Akamuuliza amuoneshe mahali Equity bank ilipo. Dogo akamwambia mimi sipajui sio mwenyeji sana na huku town.
Yule dingi akawa kama anamshangaa hivi na kumwambia kweli hupajui unaonekana mjanja mjanja hivi!! Akamwambia basi ngoja tumuulize huyu jamaa inawezekana anapafahamu (huyo jamaa kutokana na maelezo ni mwenzake). Wakamfata then yule dingi akamuuliza yule jamaa. Jamaa akasema yeah, naifahamu ilipo hata nikimuelekeza huyu kijana nadhani atakufikisha kwa maana naona na yeye anaelekea njia hiyo hiyo.
Basi yule jamaa hakumuelekeza tena yule dogo badala yake wakawa wanaongozana sasa. So wakawa watu watatu wanaongozana kuelekea maeneo ya hiyo bank ilipo. Wakiwa njiani, yule dingi akaanzisha story na kusema kuwa yeye ni mganga na kuna mama alimsaidia baada ya kubeba mimba kwa miezi kumi na sita akampatia dawa na kujifungua salama. Kwa hiyo ndio anaenda kwenye hiyo bank kwa ajili ya kwenda kuchukuwa zawadi yake aliyoahidiwa na huyo mama.
Yule jamaa mwingine akamuuliza yule dingi. Vipi kuhusu masuala ya nyota una ujuzi nayo? Dingi akasema yeah, nafahamu. Jamaa akasema hebu niangalizie mimi nyota yangu. Basi yule dingi akamwambia lete mkono wako wako. Then akauangalia na kumbwambia wewe ndugu zako wamekuchezea nyota yako inahitajika kusafishwa.
Kumbuka hapo walikuwa wameshaiona bank. Lakini wakawa wamesimama mahali na kuanza kupiga hizo story. So yule dingi akamwambia na yule dogo ampe mkono nae amuangalie nyota yake. Dogo akakubali then mzee mganga akamwambia wewe una nyota ya biashara ila pia ina hitaji kusafishwa. Na ninaweza kuwasafishia hata sasa hivi. Wote wakakubali.
Dingi akatoa kikaratasi kwenye bahasha aliyokuwa amebeba. Akachana vipande vidogo vidogo viwili na kumpa kila mmoja na kumwambia akitafune. Basi wote wakatafuna. Akawaambia waviteme na kuviangalia. Yule jamaa akatema na kusema amekuta kucha. Ni kweli ameonesha kucha. Yule dogo akatema akasema hajaona kitu. Basi yule dingi akamwambia wewe utakuwa umetafuna vibaya. Akampa kikaratasi kingine. Dogo akakitafuna then akakitema na kukuta kina nywele. Basi akawaambia hivyo vitu mlivyovikuta ndio vinashikilia nyota zenu.
Dingi akawaambia inabidi mkavitupe njia panda. Akawonesha sehemu ya kuvitupa sio mbali sana na walipokuwa. Kumbuka hapo walipo sasa hivi ni sehemu nyingine na walikaa kabisa na kufanya hayo mambo yote. Kwa sababu pale walipokuwa wamesimama kuna mtu (ambaye inasemekana ni mwenzao) alikuwa anawaangalia sana na kupelekea yule dingi kusema hapa tuondoke maana yule kijana anaetuangalia ni mchawi. Dawa zangu zinanionesha yule kijana ana uchawi, so wakahama venue.
Basi safari ya kuelekea njia panda kuvitupa vile vitu ikaanza. Akaanza yule jamaa. Masharti ni kwamba unaacha kila kitu. Basi yule jamaa aliacha wallet na simu pamoja na saa. Akaenda baada ya dakika tano akarudi. Dingi akamuuliza umeona nini? Jamaa akajibu nimekuta pete ina kitu cha pink kwa juu. Dingi akasema hiyo ndio itakayo kusafishia nyota yako. Akamwambia yule dogo kuwa yeye akienda atakuta pete yenye kidude cha blue kwa juu kwa sababu nyota yake ni ya biashara.
Basi dogo kama ilivyoada na kwa kufata masharti ya kuacha kila kitu. Akaenda. Sasa anasema kupiga hatua kama tano hivi akili ikamjia na kujisemea mbona kama natapeliwa hivi. Basi kweli bwana hajafika hata hapo njia panda, akarudi. Kurudi anakuta kweupe hakuna mtu. Dogo anasema aliwaachia smartphone Samsung hajasema aina gani, na hela elfu kumi na tano na saa.
Dogo analalamika anasema ameibiwa kiboya sana. Yeye anasisitiza kuwa jamaa wanatumia dawa kwa sababu ni vitu ambavyo anavisikia kwenye story zikipigwa na watu mbali mbali lakini yeye amenasa.
Basi wakuu story ndio ilikuwa hiyo. Inawezekana ikawa ni style ya zamani ya kutapeliwa but kuna mtu hana uzoefu nayo. Na akiisoma hapa pia inaweza ikamsaidia asitapeliwe kipuuzi namna hii.
Nawatakia siku njema.
Sent using Jamii Forums mobile app