Kumbe huu utapeli bado upo?

Kumbe huu utapeli bado upo?

Moja kwa moja kwenye mada. Kuna dogo wa form three amekuja hapa job kwa kaka yake akamsimulia yaliyo mkuta baada ya kutapeliwa simu pamoja na pesa.

Ilikuwa hivi. Dogo anaseme, ameshuka kituo cha daladala cha stesheni akitokea Mbagala. Baada ya kushuka tu, akatembea kama mita tatu akakutana na dingi mtu mzima fulani miaka 55 hakosi. Akamuuliza amuoneshe mahali Equity bank ilipo. Dogo akamwambia mimi sipajui sio mwenyeji sana na huku town.

Yule dingi akawa kama anamshangaa hivi na kumwambia kweli hupajui unaonekana mjanja mjanja hivi!! Akamwambia basi ngoja tumuulize huyu jamaa inawezekana anapafahamu (huyo jamaa kutokana na maelezo ni mwenzake). Wakamfata then yule dingi akamuuliza yule jamaa. Jamaa akasema yeah, naifahamu ilipo hata nikimuelekeza huyu kijana nadhani atakufikisha kwa maana naona na yeye anaelekea njia hiyo hiyo.

Basi yule jamaa hakumuelekeza tena yule dogo badala yake wakawa wanaongozana sasa. So wakawa watu watatu wanaongozana kuelekea maeneo ya hiyo bank ilipo. Wakiwa njiani, yule dingi akaanzisha story na kusema kuwa yeye ni mganga na kuna mama alimsaidia baada ya kubeba mimba kwa miezi kumi na sita akampatia dawa na kujifungua salama. Kwa hiyo ndio anaenda kwenye hiyo bank kwa ajili ya kwenda kuchukuwa zawadi yake aliyoahidiwa na huyo mama.

Yule jamaa mwingine akamuuliza yule dingi. Vipi kuhusu masuala ya nyota una ujuzi nayo? Dingi akasema yeah, nafahamu. Jamaa akasema hebu niangalizie mimi nyota yangu. Basi yule dingi akamwambia lete mkono wako wako. Then akauangalia na kumbwambia wewe ndugu zako wamekuchezea nyota yako inahitajika kusafishwa.

Kumbuka hapo walikuwa wameshaiona bank. Lakini wakawa wamesimama mahali na kuanza kupiga hizo story. So yule dingi akamwambia na yule dogo ampe mkono nae amuangalie nyota yake. Dogo akakubali then mzee mganga akamwambia wewe una nyota ya biashara ila pia ina hitaji kusafishwa. Na ninaweza kuwasafishia hata sasa hivi. Wote wakakubali.

Dingi akatoa kikaratasi kwenye bahasha aliyokuwa amebeba. Akachana vipande vidogo vidogo viwili na kumpa kila mmoja na kumwambia akitafune. Basi wote wakatafuna. Akawaambia waviteme na kuviangalia. Yule jamaa akatema na kusema amekuta kucha. Ni kweli ameonesha kucha. Yule dogo akatema akasema hajaona kitu. Basi yule dingi akamwambia wewe utakuwa umetafuna vibaya. Akampa kikaratasi kingine. Dogo akakitafuna then akakitema na kukuta kina nywele. Basi akawaambia hivyo vitu mlivyovikuta ndio vinashikilia nyota zenu.

Dingi akawaambia inabidi mkavitupe njia panda. Akawonesha sehemu ya kuvitupa sio mbali sana na walipokuwa. Kumbuka hapo walipo sasa hivi ni sehemu nyingine na walikaa kabisa na kufanya hayo mambo yote. Kwa sababu pale walipokuwa wamesimama kuna mtu (ambaye inasemekana ni mwenzao) alikuwa anawaangalia sana na kupelekea yule dingi kusema hapa tuondoke maana yule kijana anaetuangalia ni mchawi. Dawa zangu zinanionesha yule kijana ana uchawi, so wakahama venue.

Basi safari ya kuelekea njia panda kuvitupa vile vitu ikaanza. Akaanza yule jamaa. Masharti ni kwamba unaacha kila kitu. Basi yule jamaa aliacha wallet na simu pamoja na saa. Akaenda baada ya dakika tano akarudi. Dingi akamuuliza umeona nini? Jamaa akajibu nimekuta pete ina kitu cha pink kwa juu. Dingi akasema hiyo ndio itakayo kusafishia nyota yako. Akamwambia yule dogo kuwa yeye akienda atakuta pete yenye kidude cha blue kwa juu kwa sababu nyota yake ni ya biashara.

Basi dogo kama ilivyoada na kwa kufata masharti ya kuacha kila kitu. Akaenda. Sasa anasema kupiga hatua kama tano hivi akili ikamjia na kujisemea mbona kama natapeliwa hivi. Basi kweli bwana hajafika hata hapo njia panda, akarudi. Kurudi anakuta kweupe hakuna mtu. Dogo anasema aliwaachia smartphone Samsung hajasema aina gani, na hela elfu kumi na tano na saa.

Dogo analalamika anasema ameibiwa kiboya sana. Yeye anasisitiza kuwa jamaa wanatumia dawa kwa sababu ni vitu ambavyo anavisikia kwenye story zikipigwa na watu mbali mbali lakini yeye amenasa.

Basi wakuu story ndio ilikuwa hiyo. Inawezekana ikawa ni style ya zamani ya kutapeliwa but kuna mtu hana uzoefu nayo. Na akiisoma hapa pia inaweza ikamsaidia asitapeliwe kipuuzi namna hii.

Nawatakia siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, huyo dogo poyoyo sn. Huo utapeli wa kizamani mno.
 
Aisee umenikumbusha!

Siku moja majira ya saa mbili usiku. Ilikua jumapili nakumbuka. Nimefika zangu mqkumbusho nasubiri gari la kwenda mbagala. Mgongoni nina begi lililotuna

Wakati nimesimama pale magari ya mbagala yanapoingilia (mkabala na mesuma plus), akaja mzee mmoja akaniuliza wapi ilipo bank ili akafanye exchange ya $ to madafu (tshs) Akawa anasema katoka kulipwa na wasomali ujira wake wa miaka 3. Akatoa ka-kitita hivi akanionyesha.

Na nukuu machache " Nsaidie mdogo angu, siku hizi watu ni matapeli. Nisaidie unipeleke nitakupatia hela ya maji"

Nkamwambia leo ni jumapili alafu sasa hivi ni ni usiku, ni ngumu kupata msaada hadi kesho (jumatatu yaani)

Wakati naendelea kumsikiliza akaja kijana mmoja kavaa casual (kama mtu flani hivi anaejiheshimu). Nikajua nae anasubiri daladala, akatuuliza kuna nini, nikamweleza kwa niaba ya yule mzee.

Akasema, "kuna mtu anamfahamu anashughulika na mambo hayo, ngoja nimpigie nimuulize yuko wapi atusaidie"

Akapiga, nikaongea na huyo mzee (wa bureau exchange) ili nijiridhishe maana machale yalishanicheza. Jamaa akasema twende, tutamkuta BIASHARA COMPLEX. nikakubali kuongozana nao though nlikua nasitasita. Sasa yule mzee mwenye madola akaomba tumlipie nauli afu akishachange hela atatukatia chetu. Nikasema sio kesi.

Tukaenda hadi biashara complex kwa bahati nzuri nauli hatukulipa (nahisi konda alisahau). Sasa pale tukamkuta yule jamaa kwenye gari. Kijana mtanashati akasema tuingie kwenye gari ili tubadilishiwe hela.

Asee Roho ilikataa katakata. Nikawaambia badilisheni mtanikuta nje. Yule mzee mwenye dola akashuka na kunifuata (maanq alishaingia kwenye gari). Akaanza kunchombeza "mimi nakuamini wewe na blah blah " . Nikamwambia umetaka uonyeshwe na tayari umeonyeshwa.

Hapo akarudi kwenye ile gari (kama crown hivi) wakaondoka wote. Nikawa najiuliza watu muonane leo afu muaminiane kiasi kwamba muondoke wote kwenye gari moja !

Nilipona kwa staili hiyo.

NILICHOJIFUNZA: Ni muhimu kuwa na hela , kama ningekua mweupe (sina hela) ningekua na tamaa ya kupata pesa. UMASKINI MBAYA SANA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilishawahi kunitokea Kariakoo mtaa wa mkunguni 2006.
Nilikuwa natoka kwenye duka la vifaa vya umeme kununua socket switch,ghafla Mzee mmoja wa makamo hivi umri ni kama miaka 55 ana mvi kidogo kichwani.Akanisalimia akaniuliza kama nalifahamu duka la Maria Stopps, nikamjibu silifahamu.Akajitambulisha yeye ni mgeni ametokea Sumbawanga,na wamepaki gari yao Big Bon Petro station pale Msimbazi."Wewe unaonekana ni mwenyeji huwezi kunisaidia kwani mtaa wa Living Stone ndio upi?" Nikamjibu mitaa mingi siijui majina yake.

Ghafla tukamkuta kijana mmoja kasimama akasema ngoja tumuulize,akaniuliza duka la Maria Stopps liko wapi?Akajibu lipo jengo la umoja wa vijana(CCM).Akasema naomba mnisaidie kunipeleka nitawapa hela ya chai.Hapo tunakaribia barabara ya Lumumba maana Mimi nilikuwa naelekea mtaa wa Kisutu.Akaanza kujieleza kwamba yeye ni mganga wa kienyeji.Na huyo anaemfuata ni mteja wake(mwanamke) ambaye alimtibu baada ya kurogwa na mke mwenzake alikuwa na mimba ya miezi 18.

Pia ni tajiri anamiliki hayo maduka ya Maria Stops,hapo hapo kengele ikagonga kichwani Kwa kuwa nafahamu Maria Stops ni taasisi ya kidini inayoshughulikia maswala ya uzazi.Tulipofika tu Lumumba nikamwambia huyo kijana atakufikisha mimi nina shughuli zangu nyingine.Hivyo ndivyo tulivoachana.

Niligutuka baada ya kusema huyo mama ni mmiliki wa Maria Stops ndipo walipokosea.

Umesahau ulitoka Narungombe ukaingia Livingstone ulipofika Mtaa wa Mahiwa ukaleta ujanja wako huo nikaponyoka kukutapeli, Siku hizi umekuwa mjanja heee
 
Aisee umenikumbusha!

Siku moja majira ya saa mbili usiku. Ilikua jumapili nakumbuka. Nimefika zangu mqkumbusho nasubiri gari la kwenda mbagala. Mgongoni nina begi lililotuna

Wakati nimesimama pale magari ya mbagala yanapoingilia (mkabala na mesuma plus), akaja mzee mmoja akaniuliza wapi ilipo bank ili akafanye exchange ya $ to madafu (tshs) Akawa anasema katoka kulipwa na wasomali ujira wake wa miaka 3. Akatoa ka-kitita hivi akanionyesha.

Na nukuu machache " Nsaidie mdogo angu, siku hizi watu ni matapeli. Nisaidie unipeleke nitakupatia hela ya maji"

Nkamwambia leo ni jumapili alafu sasa hivi ni ni usiku, ni ngumu kupata msaada hadi kesho (jumatatu yaani)

Wakati naendelea kumsikiliza akaja kijana mmoja kavaa casual (kama mtu flani hivi anaejiheshimu). Nikajua nae anasubiri daladala, akatuuliza kuna nini, nikamweleza kwa niaba ya yule mzee.

Akasema, "kuna mtu anamfahamu anashughulika na mambo hayo, ngoja nimpigie nimuulize yuko wapi atusaidie"

Akapiga, nikaongea na huyo mzee (wa bureau exchange) ili nijiridhishe maana machale yalishanicheza. Jamaa akasema twende, tutamkuta BIASHARA COMPLEX. nikakubali kuongozana nao though nlikua nasitasita. Sasa yule mzee mwenye madola akaomba tumlipie nauli afu akishachange hela atatukatia chetu. Nikasema sio kesi.

Tukaenda hadi biashara complex kwa bahati nzuri nauli hatukulipa (nahisi konda alisahau). Sasa pale tukamkuta yule jamaa kwenye gari. Kijana mtanashati akasema tuingie kwenye gari ili tubadilishiwe hela.

Asee Roho ilikataa katakata. Nikawaambia badilisheni mtanikuta nje. Yule mzee mwenye dola akashuka na kunifuata (maanq alishaingia kwenye gari). Akaanza kunchombeza "mimi nakuamini wewe na blah blah " . Nikamwambia umetaka uonyeshwe na tayari umeonyeshwa.

Hapo akarudi kwenye ile gari (kama crown hivi) wakaondoka wote. Nikawa najiuliza watu muonane leo afu muaminiane kiasi kwamba muondoke wote kwenye gari moja !

Nilipona kwa staili hiyo.

NILICHOJIFUNZA: Ni muhimu kuwa na hela , kama ningekua mweupe (sina hela) ningekua na tamaa ya kupata pesa. UMASKINI MBAYA SANA

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiponea Uzi na sindano

Wewe ulibakiza kidogo tu wakutapeli na pengine wangekupeka chaka wakakuulia huko. Ulifanya kosa kubwa sana kufuatana na watu usiowafahau. Jiulize, dunia ya leo mtu hakujui kwanini akuamini kiasi hicho? Somo la kwanza: ukikutana na mtu yeyote ambaye humjui na ukaone anakuchangamkia usimchekee. Kuwa serious kabisa na vaa sura ya hasira kali. Akijifanya kuelezea mambo ambayo kwa hali ya kawaida mtu mgeni hapaswi kukuelezea, mfukuze.
 
Kuna jirani yetu alipigwa style hii nikiwa primary, nimefika form two natoka mchikidown kucheki ratiba nashuka Tandika nikakutana nao wakaniimbisha but nikawastukia nikawa nawaza jinsi ya kuwatoka pindi wapo busy kuniimbisha mie sipo kabisa pale kimawazo. Ikafika time ya kuacha vitu kwa mwenzio jamaa akaenda kanipa wallet ile anapotea tu nikamwona mmama anapita kwa mbali nikamwambia mganga huku natoka nduki kwamba naenda kumuita mama yangu yule anapita aje asikie matatizo niliyonayo ndiyo kimoja hiyo
 
Suala la msingi ni kuacha tamaa na shortcut. Wanaotapeliwa ni wenye nacho, huwezi tapeliwa kama huna kitu. Kuwa na hela sio suluhisho la kutotapeliwa maana wewe ndio mlengwa wa kutapeliwa. Muhimu ni kuridhika na ulichonacho. Never trust a stranger.
 
Wewe ulibakiza kidogo tu wakutapeli na pengine wangekupeka chaka wakakuulia huko. Ulifanya kosa kubwa sana kufuatana na watu usiowafahau. Jiulize, dunia ya leo mtu hakujui kwanini akuamini kiasi hicho? Somo la kwanza: ukikutana na mtu yeyote ambaye humjui na ukaone anakuchangamkia usimchekee. Kuwa serious kabisa na vaa sura ya hasira kali. Akijifanya kuelezea mambo ambayo kwa hali ya kawaida mtu mgeni hapaswi kukuelezea, mfukuze.
Umeongea mambo ya msingi. Watu wafuate ushauri huu.
 
Hii ya pochi mjomba wangu ambaye sasa ni marehemu aliwahi kutapeliwa mjini Moshi mwaka 1970! Imagine mpaka sasa bado mtindo unatumika.
Hii ilinikuta makambako miaka ya 2006-2007 hivi. Alipita jamaa na baiskeli yupo nduki mara nikaona bunda kubwa la noti la sh.500 hivi limedondoka. Mara ghafla akapita mtu toka nyuma yangu akawahi lile bunda kuokota akawa anashangaa kwa sauti, akaona mimi sina time kabisa wala sijawehuka na lile bunda basi akaondoka zake. Kama ningeonyesha kuwehuka angesema twende tukagawane, halafu huko wangenikaba na kuiba kila kilicho changu.

Nilishtuka mapema kwasababu nilishawahi simuliwa story kama hii siku za nyuma. Mwenyezi MUNGU alinipa wasaa wa kuepuka utapeli ule.
 
Kuna jirani yetu alipigwa style hii nikiwa primary, nimefika form two natoka mchikidown kucheki ratiba nashuka Tandika nikakutana nao wakaniimbisha but nikawastukia nikawa nawaza jinsi ya kuwatoka pindi wapo busy kuniimbisha mie sipo kabisa pale kimawazo. Ikafika time ya kuacha vitu kwa mwenzio jamaa akaenda kanipa wallet ile anapotea tu nikamwona mmama anapita kwa mbali nikamwambia mganga huku natoka nduki kwamba naenda kumuita mama yangu yule anapita aje asikie matatizo niliyonayo ndiyo kimoja hiyo
Wewe ulikuwa unaibiwa huku unajua kuwa unaibiwa, tatizo lako ulikuwa muoga, ulishindwa kujiamini.
 
Back
Top Bottom