Kumbe huu utapeli bado upo?

Kumbe huu utapeli bado upo?

Moja kwa moja kwenye mada. Kuna dogo wa form three amekuja hapa job kwa kaka yake akamsimulia yaliyo mkuta baada ya kutapeliwa simu pamoja na pesa.

Ilikuwa hivi. Dogo anaseme, ameshuka kituo cha daladala cha stesheni akitokea Mbagala. Baada ya kushuka tu, akatembea kama mita tatu akakutana na dingi mtu mzima fulani miaka 55 hakosi. Akamuuliza amuoneshe mahali Equity bank ilipo. Dogo akamwambia mimi sipajui sio mwenyeji sana na huku town.

Yule dingi akawa kama anamshangaa hivi na kumwambia kweli hupajui unaonekana mjanja mjanja hivi!! Akamwambia basi ngoja tumuulize huyu jamaa inawezekana anapafahamu (huyo jamaa kutokana na maelezo ni mwenzake). Wakamfata then yule dingi akamuuliza yule jamaa. Jamaa akasema yeah, naifahamu ilipo hata nikimuelekeza huyu kijana nadhani atakufikisha kwa maana naona na yeye anaelekea njia hiyo hiyo.

Basi yule jamaa hakumuelekeza tena yule dogo badala yake wakawa wanaongozana sasa. So wakawa watu watatu wanaongozana kuelekea maeneo ya hiyo bank ilipo. Wakiwa njiani, yule dingi akaanzisha story na kusema kuwa yeye ni mganga na kuna mama alimsaidia baada ya kubeba mimba kwa miezi kumi na sita akampatia dawa na kujifungua salama. Kwa hiyo ndio anaenda kwenye hiyo bank kwa ajili ya kwenda kuchukuwa zawadi yake aliyoahidiwa na huyo mama.

Yule jamaa mwingine akamuuliza yule dingi. Vipi kuhusu masuala ya nyota una ujuzi nayo? Dingi akasema yeah, nafahamu. Jamaa akasema hebu niangalizie mimi nyota yangu. Basi yule dingi akamwambia lete mkono wako wako. Then akauangalia na kumbwambia wewe ndugu zako wamekuchezea nyota yako inahitajika kusafishwa.

Kumbuka hapo walikuwa wameshaiona bank. Lakini wakawa wamesimama mahali na kuanza kupiga hizo story. So yule dingi akamwambia na yule dogo ampe mkono nae amuangalie nyota yake. Dogo akakubali then mzee mganga akamwambia wewe una nyota ya biashara ila pia ina hitaji kusafishwa. Na ninaweza kuwasafishia hata sasa hivi. Wote wakakubali.

Dingi akatoa kikaratasi kwenye bahasha aliyokuwa amebeba. Akachana vipande vidogo vidogo viwili na kumpa kila mmoja na kumwambia akitafune. Basi wote wakatafuna. Akawaambia waviteme na kuviangalia. Yule jamaa akatema na kusema amekuta kucha. Ni kweli ameonesha kucha. Yule dogo akatema akasema hajaona kitu. Basi yule dingi akamwambia wewe utakuwa umetafuna vibaya. Akampa kikaratasi kingine. Dogo akakitafuna then akakitema na kukuta kina nywele. Basi akawaambia hivyo vitu mlivyovikuta ndio vinashikilia nyota zenu.

Dingi akawaambia inabidi mkavitupe njia panda. Akawonesha sehemu ya kuvitupa sio mbali sana na walipokuwa. Kumbuka hapo walipo sasa hivi ni sehemu nyingine na walikaa kabisa na kufanya hayo mambo yote. Kwa sababu pale walipokuwa wamesimama kuna mtu (ambaye inasemekana ni mwenzao) alikuwa anawaangalia sana na kupelekea yule dingi kusema hapa tuondoke maana yule kijana anaetuangalia ni mchawi. Dawa zangu zinanionesha yule kijana ana uchawi, so wakahama venue.

Basi safari ya kuelekea njia panda kuvitupa vile vitu ikaanza. Akaanza yule jamaa. Masharti ni kwamba unaacha kila kitu. Basi yule jamaa aliacha wallet na simu pamoja na saa. Akaenda baada ya dakika tano akarudi. Dingi akamuuliza umeona nini? Jamaa akajibu nimekuta pete ina kitu cha pink kwa juu. Dingi akasema hiyo ndio itakayo kusafishia nyota yako. Akamwambia yule dogo kuwa yeye akienda atakuta pete yenye kidude cha blue kwa juu kwa sababu nyota yake ni ya biashara.

Basi dogo kama ilivyoada na kwa kufata masharti ya kuacha kila kitu. Akaenda. Sasa anasema kupiga hatua kama tano hivi akili ikamjia na kujisemea mbona kama natapeliwa hivi. Basi kweli bwana hajafika hata hapo njia panda, akarudi. Kurudi anakuta kweupe hakuna mtu. Dogo anasema aliwaachia smartphone Samsung hajasema aina gani, na hela elfu kumi na tano na saa.

Dogo analalamika anasema ameibiwa kiboya sana. Yeye anasisitiza kuwa jamaa wanatumia dawa kwa sababu ni vitu ambavyo anavisikia kwenye story zikipigwa na watu mbali mbali lakini yeye amenasa.

Basi wakuu story ndio ilikuwa hiyo. Inawezekana ikawa ni style ya zamani ya kutapeliwa but kuna mtu hana uzoefu nayo. Na akiisoma hapa pia inaweza ikamsaidia asitapeliwe kipuuzi namna hii.

Nawatakia siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mijinga minga mingine ilitaka kuniingiza chaka hv karibuni wanadai wana safisha dollar pia wana black money wana dublicate elf10 wakatoa bluck m mbili kaweka noti ya 10elf ktkt ya zile bluck baada ya hapo kaminya sijui dawa gani kaanza kuscratch kama vocha kweli 10elf ikazaa 20 ikawa jumla 30elf baada ya hapo wanataka niwe na mtaji around 10m ili itoke 20m jumla ziwe 30m 2kazozana na maswali ya hapa na pale akadai 10m kama cna nitafute hata 5m ili jumla zje kua 15m yeye achukue 5m kama faida ya kazi yake mm nibaki na 10m kama mtaji na faida nikamsubirisha kama cku mbili nikaanza kuwasaka mdogo mdogo nilicho kuja kubaini hao watu sio mkate wa kurumangia hata kwa supu ya mbwa! Ukikutana nao huwezi dhania kabisa
 
Moja kwa moja kwenye mada. Kuna dogo wa form three amekuja hapa job kwa kaka yake akamsimulia yaliyo mkuta baada ya kutapeliwa simu pamoja na pesa.

Ilikuwa hivi. Dogo anaseme, ameshuka kituo cha daladala cha stesheni akitokea Mbagala. Baada ya kushuka tu, akatembea kama mita tatu akakutana na dingi mtu mzima fulani miaka 55 hakosi. Akamuuliza amuoneshe mahali Equity bank ilipo. Dogo akamwambia mimi sipajui sio mwenyeji sana na huku town.

Yule dingi akawa kama anamshangaa hivi na kumwambia kweli hupajui unaonekana mjanja mjanja hivi!! Akamwambia basi ngoja tumuulize huyu jamaa inawezekana anapafahamu (huyo jamaa kutokana na maelezo ni mwenzake). Wakamfata then yule dingi akamuuliza yule jamaa. Jamaa akasema yeah, naifahamu ilipo hata nikimuelekeza huyu kijana nadhani atakufikisha kwa maana naona na yeye anaelekea njia hiyo hiyo.

Basi yule jamaa hakumuelekeza tena yule dogo badala yake wakawa wanaongozana sasa. So wakawa watu watatu wanaongozana kuelekea maeneo ya hiyo bank ilipo. Wakiwa njiani, yule dingi akaanzisha story na kusema kuwa yeye ni mganga na kuna mama alimsaidia baada ya kubeba mimba kwa miezi kumi na sita akampatia dawa na kujifungua salama. Kwa hiyo ndio anaenda kwenye hiyo bank kwa ajili ya kwenda kuchukuwa zawadi yake aliyoahidiwa na huyo mama.

Yule jamaa mwingine akamuuliza yule dingi. Vipi kuhusu masuala ya nyota una ujuzi nayo? Dingi akasema yeah, nafahamu. Jamaa akasema hebu niangalizie mimi nyota yangu. Basi yule dingi akamwambia lete mkono wako wako. Then akauangalia na kumbwambia wewe ndugu zako wamekuchezea nyota yako inahitajika kusafishwa.

Kumbuka hapo walikuwa wameshaiona bank. Lakini wakawa wamesimama mahali na kuanza kupiga hizo story. So yule dingi akamwambia na yule dogo ampe mkono nae amuangalie nyota yake. Dogo akakubali then mzee mganga akamwambia wewe una nyota ya biashara ila pia ina hitaji kusafishwa. Na ninaweza kuwasafishia hata sasa hivi. Wote wakakubali.

Dingi akatoa kikaratasi kwenye bahasha aliyokuwa amebeba. Akachana vipande vidogo vidogo viwili na kumpa kila mmoja na kumwambia akitafune. Basi wote wakatafuna. Akawaambia waviteme na kuviangalia. Yule jamaa akatema na kusema amekuta kucha. Ni kweli ameonesha kucha. Yule dogo akatema akasema hajaona kitu. Basi yule dingi akamwambia wewe utakuwa umetafuna vibaya. Akampa kikaratasi kingine. Dogo akakitafuna then akakitema na kukuta kina nywele. Basi akawaambia hivyo vitu mlivyovikuta ndio vinashikilia nyota zenu.

Dingi akawaambia inabidi mkavitupe njia panda. Akawonesha sehemu ya kuvitupa sio mbali sana na walipokuwa. Kumbuka hapo walipo sasa hivi ni sehemu nyingine na walikaa kabisa na kufanya hayo mambo yote. Kwa sababu pale walipokuwa wamesimama kuna mtu (ambaye inasemekana ni mwenzao) alikuwa anawaangalia sana na kupelekea yule dingi kusema hapa tuondoke maana yule kijana anaetuangalia ni mchawi. Dawa zangu zinanionesha yule kijana ana uchawi, so wakahama venue.

Basi safari ya kuelekea njia panda kuvitupa vile vitu ikaanza. Akaanza yule jamaa. Masharti ni kwamba unaacha kila kitu. Basi yule jamaa aliacha wallet na simu pamoja na saa. Akaenda baada ya dakika tano akarudi. Dingi akamuuliza umeona nini? Jamaa akajibu nimekuta pete ina kitu cha pink kwa juu. Dingi akasema hiyo ndio itakayo kusafishia nyota yako. Akamwambia yule dogo kuwa yeye akienda atakuta pete yenye kidude cha blue kwa juu kwa sababu nyota yake ni ya biashara.

Basi dogo kama ilivyoada na kwa kufata masharti ya kuacha kila kitu. Akaenda. Sasa anasema kupiga hatua kama tano hivi akili ikamjia na kujisemea mbona kama natapeliwa hivi. Basi kweli bwana hajafika hata hapo njia panda, akarudi. Kurudi anakuta kweupe hakuna mtu. Dogo anasema aliwaachia smartphone Samsung hajasema aina gani, na hela elfu kumi na tano na saa.

Dogo analalamika anasema ameibiwa kiboya sana. Yeye anasisitiza kuwa jamaa wanatumia dawa kwa sababu ni vitu ambavyo anavisikia kwenye story zikipigwa na watu mbali mbali lakini yeye amenasa.

Basi wakuu story ndio ilikuwa hiyo. Inawezekana ikawa ni style ya zamani ya kutapeliwa but kuna mtu hana uzoefu nayo. Na akiisoma hapa pia inaweza ikamsaidia asitapeliwe kipuuzi namna hii.

Nawatakia siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii tabia iko sana msamvu morogoro kuna Dogo mmoja wa mzumbe alishawahi kupigwa changa hivi hivi
 
Mimi nilitapeliwa hivyo kitambo sana nikiwa form2. Sasa hv akinifuata na maneno hayo namtapeli yy
Mkuu hela ya tapeli hailiwi huwa ni chambo, sana sana utaishia kutapeliwa kwa staili nyingine.
 
Siku hizi wanyamwezi huko znz wanafanya sana hayo...
Juzi tu hapa katepeliwa mtu ..laki nne mkononi ..simu na saa...na kwenye ATM wakamtoa 1m.
 
Aisee umenikumbusha!

Siku moja majira ya saa mbili usiku. Ilikua jumapili nakumbuka. Nimefika zangu mqkumbusho nasubiri gari la kwenda mbagala. Mgongoni nina begi lililotuna

Wakati nimesimama pale magari ya mbagala yanapoingilia (mkabala na mesuma plus), akaja mzee mmoja akaniuliza wapi ilipo bank ili akafanye exchange ya $ to madafu (tshs) Akawa anasema katoka kulipwa na wasomali ujira wake wa miaka 3. Akatoa ka-kitita hivi akanionyesha.

Na nukuu machache " Nsaidie mdogo angu, siku hizi watu ni matapeli. Nisaidie unipeleke nitakupatia hela ya maji"

Nkamwambia leo ni jumapili alafu sasa hivi ni ni usiku, ni ngumu kupata msaada hadi kesho (jumatatu yaani)

Wakati naendelea kumsikiliza akaja kijana mmoja kavaa casual (kama mtu flani hivi anaejiheshimu). Nikajua nae anasubiri daladala, akatuuliza kuna nini, nikamweleza kwa niaba ya yule mzee.

Akasema, "kuna mtu anamfahamu anashughulika na mambo hayo, ngoja nimpigie nimuulize yuko wapi atusaidie"

Akapiga, nikaongea na huyo mzee (wa bureau exchange) ili nijiridhishe maana machale yalishanicheza. Jamaa akasema twende, tutamkuta BIASHARA COMPLEX. nikakubali kuongozana nao though nlikua nasitasita. Sasa yule mzee mwenye madola akaomba tumlipie nauli afu akishachange hela atatukatia chetu. Nikasema sio kesi.

Tukaenda hadi biashara complex kwa bahati nzuri nauli hatukulipa (nahisi konda alisahau). Sasa pale tukamkuta yule jamaa kwenye gari. Kijana mtanashati akasema tuingie kwenye gari ili tubadilishiwe hela.

Asee Roho ilikataa katakata. Nikawaambia badilisheni mtanikuta nje. Yule mzee mwenye dola akashuka na kunifuata (maanq alishaingia kwenye gari). Akaanza kunchombeza "mimi nakuamini wewe na blah blah " . Nikamwambia umetaka uonyeshwe na tayari umeonyeshwa.

Hapo akarudi kwenye ile gari (kama crown hivi) wakaondoka wote. Nikawa najiuliza watu muonane leo afu muaminiane kiasi kwamba muondoke wote kwenye gari moja !

Nilipona kwa staili hiyo.

NILICHOJIFUNZA: Ni muhimu kuwa na hela , kama ningekua mweupe (sina hela) ningekua na tamaa ya kupata pesa. UMASKINI MBAYA SANA

Sent using Jamii Forums mobile app
wangekufanya kitu kibaya sana

Kweli umasikini mbayaa
 
duh yani uyu dogo wala simcheki mimi nilishawai kulizwa nakumbuka nilikuwa nipo form 3 Enzi hizo nilikuwa natoka zangu bunju naenda chuo kikuu UDSM nampelekea bro vijisenti vya kula sasa ile nashuka tu mwenge pale stendi kabla haijaamishwa basi jamaa wa kwanza akaja sijakaa vizuri akaja mwingine yani dah wale washenzi waliniuliza hospitali ya mwenge yani walinisemesha nilijikuta napoteza mawazo tena ya kwenda udsm yani walinitembeza mpak kule bamaga around maeneo ya taasisi ya mitiani necta maeneo hayo waliniibia vijisenti vyangu baati nzuri mfuko mwingine wa suruali nilikuwa na kama mia tano by that time nauli ilikuwa shilingi hamsini ila dah aya mambo sio ya kumcheka mtu
 
Kabisaa mkuu sio miaka hiyoo tu hata leo kuna watu wanaibiwaa kwa style hii
 
imewahi kunitokea kariakoo hiyo 2012 ila nikashtuka hapo kwenye kuacha simu nikasepa mbio wachawi wale wapumbavu na mimi nilitafuna zikatoka nywele.nilisali sana siku hiyo nikajua labda nitadhurika hahaaa na sikuwahi kumwambiaga mtu hiyo issue
 
Huu ulishanikuta moshi maeneo ya mjini pale, mwanzoni niliwaona wema ila baada ya wao kuanza kupiga story za nyota nilipatwa na wasiwasi nikajeuka, nilivyokua narudi tu nakukatana na mama anakuja nyuma yangu akaniuliza hawajakutapeli ? Kumbe mama yule anawafahamu na akajua hawatoniacha salama, yule mama alikua ameita polisi kabisa, wakati narudi stand niliwaona wanaingizwa pale central wakiwa wamepigwa bangili za polisi, siku hiyo ilikua jumapili na nna elfu 30 mfukoni, na home niliaga naenda kanisani mi nikaenda town nikanunue simu used pale stand ya moshi chini ya mwembe!!! Nilichogundua hawa watu hawatumii dawa ila wamejipanga tu neno juu ya neno hawakuachii ufikirie, mimi nilikua form two ila mpaka leo hata kama uwe vipi siwezi kukupa direction kwa kwenda nawewe labda uwe mdada murembo sana !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nishapigwa kitambo hiyo 2008 ilikuwa inafanana naiyo maeneo ya Tandika
 
Enzi hizo wanafunzi waliibiwa sana pesa za ada.
Nikiwa form two mwaka 1998 nilinunuliwa buti Fulani Kali,sasa naenda zangu shule Minaki nipo maeneo ya around about ya shule Uhuru pale kuna shoe shine jamaa akaniambia dogo viatu vyako vizuri lakini huna dawa mzuri ya kuvishine Mimi ninayo hapa ngoja nikupigie ukiipenda nitakuuzia. Mimi machale yakanicheza,nikamuambia sawa. Jamaa akaniambia via viatu basi,nikamuambia piga vikiwa mguuni. Jamaa kapiga brush kama nne kisha akaniambia dogo kila brush moja mia tano. Nikamuambia husinitanie Mimi mtoto wa Kinondoni Moscow kule mateja wanaiba mpaka vijiko alafu wewe unajaribu kuniibia kiboyo hivi,nikaondoka zangu jamaa wakawa wanacheka tu.
 
Huu ulishanikuta moshi maeneo ya mjini pale, mwanzoni niliwaona wema ila baada ya wao kuanza kupiga story za nyota nilipatwa na wasiwasi nikajeuka, nilivyokua narudi tu nakukatana na mama anakuja nyuma yangu akaniuliza hawajakutapeli ? Kumbe mama yule anawafahamu na akajua hawatoniacha salama, yule mama alikua ameita polisi kabisa, wakati narudi stand niliwaona wanaingizwa pale central wakiwa wamepigwa bangili za polisi, siku hiyo ilikua jumapili na nna elfu 30 mfukoni, na home niliaga naenda kanisani mi nikaenda town nikanunue simu used pale stand ya moshi chini ya mwembe!!! Nilichogundua hawa watu hawatumii dawa ila wamejipanga tu neno juu ya neno hawakuachii ufikirie, mimi nilikua form two ila mpaka leo hata kama uwe vipi siwezi kukupa direction kwa kwenda nawewe labda uwe mdada murembo sana !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Walinikumba YMCA wakaenda kunipiga kazi Coffee Curing njia panda ya Njoro. Situation ilikuwa the same mpaka kesho sihitaji mtu aniulize usenge nikiwa njiani.
 
Shida hamna cha kufanya,mnatembeatembea tu bila ratiba mjini.

Kama una miadi yako,sioni ukimpa attention mtu baki tu kwa muda wote huo unaamrishwa kama zuzu.

Unaanzaje kwanza kutafuna makaratasi umepewa na stranger tu njiani?

IMG_20200703_205649.jpg
 
Sikujui hunijiui
Yanini nikusikilize??
Hata salamu yako siitikii...Nakausha tu
 
Back
Top Bottom