Kumbe hizi ndizo nguvu za Serikali

Kumbe hizi ndizo nguvu za Serikali

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,385
Reaction score
2,587
Nianze kwa kusema kwamba ndugu zangu Watanzania tunachanganya sana mambo.

Frikra za Watanzania walio wengi juu ya serikali ni kwamba serikali ni lijitu lenye manguvu makubwa sana. Na ili kuonyesha manguvu yake basi litanyanganya watu ardhi pasipo fidia inayostahili, litapiga viongozi wa upinzani, litafanya mambo pasipo kushirikisha wananchi, litaingilia maamuzi ya mahakama, litaingilia maamuzi ya taasisi nyingine, yaani nguvu zake hazina mipaka.

Kumbe hizo tajwa sio nguvu za serikali bali ni nguvu uchwara, batili, za kijinga.

Sasa kwa maneno machache nitabainisha nguvu halisi za serikali.

- Kuweza kukusanya kodi kutoka kwa wazalishaji wote walio ndani ya mipaka yake pasipo kubagua.

- Kuweza kujenga, kusimamia na kuendesha miundombinu muhimu; barabara, umeme, maji

- Kutoa huduma za kijamii bora; mashule, hospitali, mafao, nk

Kwa misingi hiyo tajwa serikali ionyeshe mabavu yake sasa, kama late Nyerere alivyosema maadui ambao serikali yapaswa kupigana nao ni Ujinga, Umaskini na Maradhi.

Je, serikali ya Tanzania ina mbavuu kweli?
 
Serikali Haina uwezo wa kunyanganya Ardhi mwananchi
 
Back
Top Bottom