Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,571
- 21,119
Na huu ndiyo Ujinga mkubwa tulio nao Waafrika wengi, kwani unafikiri Katiba ni nini? Si karatasi tu, sasa unafikiri Karatasi inawezaje kumzuia mtu mbaya kufanya mabaya?
Wakenya wana Katiba mpya, ambayo imezuia yote hayo na kupunguza madaraka ya Raisi, sasa imewasaidia nini? Angalia wanavyolia sasa hivi na wizi na rushwa iliyopitiliza, upendeleo watu wanapewa vyeo na kulindwa kwa kuwa tu wanaukaribu na Raisi sasa hiyo Katiba imesaidia nini?
Acheni Ujinga Waafrika, cha muhimu ni kupigania kuondoa umaskini kwanza kwa kuwekeza kwenye Elimu tukifanikiwa hapo mengine yote yatafuatia yenyewe tu, watu walioeleimika na wasio masikini hawawezi kuchagua kiongozi mbaya kuwaongoza lkn kama watu wanabakia kuwa masikini na hawana Elimu hata ukichukuwa Katiba ya Japani au sijui Kanada bado Raisi kama ni mbaya ataharibu tu nchi kwa kuikandamiza katiba hiyo hiyo!
Huu ni ujinga uliopindukia! Katiba ya nchi kuita karatasi?!!
Kwani noti si karatasi tu? ! Mbona nchi zinayumbishwa!!