Kumbe Dk Hamisi Kigwangalla ana CV ya kutisha!

Mambo ya kizamani kulinganisha CV,
hapa Wote ni wabunge hebu linganisha utendaji wao...
Mbona maccm kibao maprof lakini ni bure kabisa, anaza na Kapuya

Cha muhimu tulinganishe utendaji wao

Mnyika mpaka sasa anaongoza kwa kila kitu bungeni, kuchangia, kupeleka hoja binafsi, kuuliza maswali, kuhudhuria bungeni, kutoa michango, hakuna hata mmoja ambalo Kigwangala kamzidi, hapa CV inasaidia nini?

Mwambia akamsaidie baba yake kwanza, laana inamtafuna.

Safi sana Mkuu, 1795618_296102933877339_653044208_n.jpg
 
Na wewe wataje unaowamini towa cv zao. Mbowe na slaa kama watu awapasuki kwa kucheka
 
Mi nataka kujua huo mtaji wa kuanzisha kampuni yake yenye mzunguko wa hela Tshs billioni kumi na kuajiri watu 400 kama alivyoeleza aliutoa wapi, na hakika hakuzaliwa nao yaani kurithi au wa familia, hizo ni struggle zake, tutonye basi na sis ivijana wenzio ulivyoibuka!
 
kawaida sana,kuna watanzania waliosomea havard chuo bora kabisa duniani

Chenge ni mmojawapo!Unaweza kupima mchango wako mwenyewe huenda itakufanya ufikirie zaidi ya hapo

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Imeandikwa kwenye Ukurasa wa FB wa hii kitu https://www.facebook.com/pages/Citizens-For-Kigwangalla/370119756463712

Wasifu Mfupi wa Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB).

Dr. Hamisi Kigwangalla, MB, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, alizaliwa Mwaka 1975, Mwezi Agosti, Tarehe 7 katika Hospitali ya Maweni, Kigoma. Akiwa ni mtoto wa kwanza wa Bwana Mahampa Kigwangalla na bibi Bagaile Lumola. Baba yake ni Mkimbu kutokea kijiji cha Goweko, Uyui, Tabora na Mama yake ni Mnyamwezi mzaliwa wa Nzega, huko huko Tabora. Wakati anazaliwa Baba yake alikuwa ni mtumishi wa benki ya NBC (ya zamani) na mama alikuwa ni mwalimu wa daraja la A. Alikulia mjini Nzega kwa babu na bibi yake baada ya wazazi wake kutengana.

Amesoma shule ya msingi Kitongo na Mwanzoli, Nzega. Sekondari alisomea Kigoma Secondary School, ambapo alifaulu vizuri masomo ya sayansi na kuchaguliwa kwenda kusoma Shinyanga Secondary School, kombinesheni ya Physics, Chemistry na Biology (PCB), ambapo alifaulu vizuri kwa division I na kuchaguliwa kusomea masomo ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Muhimbili University College of Health Sciences. Mwaka 2004, alihitimu masomo ya Udaktari wa Tiba na kutunukiwa digrii ya 'Doctor of Medicine' ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Alifanya internship katika hospitali ya taifa ya muhimbili na baadaye hospitali ya Mwananyamala. Baada ya hapo alipata fursa ya kusoma Masters of Public Health (MPH) katika Chuo Cha Karolinska Institutet na Master of Business Administration (MBA) akibobea zaidi kwenye Organization and Leadership, katika chuo kikuu cha Blekinge Institute of Technology - vyuo vyote hivi vipo nchini Sweden.

Sasa hivi, Dr. Kigwangalla anamalizia tasnifu yake ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) kwenye Public Health, akibobea zaidi kwenye Health Economics. Anaandika tasnifu yake kuhusiana na haki, usawa na uhalali wa mchakato wa bajeti kwenye sekta ya afya nchini Tanzania.

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali. Daktari daraja la II, Mtafiti na mtaalamu mshauri wa kujitegemea. Pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa makampuni yaliyo wanachama wa MSK Group, na amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Group hii kabla ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega. Kampuni ya MSK Group inaweza kukadiriwa kwa sasa kumiliki mali na madeni kwa kiwango cha TZS 10bn, na inazungusha kwa mwaka mtaji wa takriban TZS 4bn. Inaajiri watanzania wapatao 400 moja kwa moja (katika nyakati mbali mbali za mwaka), na zaidi ya 200,000 indirectly.

Dr. Kigwangalla amewahi kuanzisha na ama kushiriki harakati mbalimbali za kupambana na umaskini, maradhi, ujinga, ukosefu wa ajira kwa vijana, uonevu, utetezi wa wanyonge na wasiojiweza, mapambano dhihi ya VVU/UKIMWI, ulinzi wa raslimali za taifa na kuhakikisha watanzania wanafaidika na urithi wao n.k.

HK amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi kwenye chama chake, CCM (ambacho alijiunga rasmi mwaka 1994); amewahi kuwa chipukizi na kiongozi wa chipukizi wilaya ya Nzega, ameshiriki makambi mbalimbali ya vijana na halaiki, amewahi kuwa kijana wa Green Guard wa CCM, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, tawi la Kigoma Sekondari na Mjumbe, Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sikonge akiwawakilisha vijana. Kwa sasa ni Mjumbe, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Tabora, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nzega na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Hajawahi kujiunga na chama kingine chochote kile cha siasa. Amewahi kushiriki kampeni mbalimbali za uchaguzi na kujitolea kwa hali na mali kujenga chama chake.

Dr. Kigwangalla ni mwandishi mzuri wa vitabu, makala za kisayansi na makala za uchambuzi wa mambo mbali mbali ya kisiasa na kiuchumi kwenye magazeti mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.

Ni mwanamichezo, akipendelea zaidi kucheza soccer, basketball, tennis na Golf. Anapendelea mijadala ya wazi kwenye mitandao ya kijamii na ni mpenzi wa kusoma vitabu. Dr. Kigwangalla ana mke na watoto watatu, Sheila, Hawa na HK Jr.

View attachment 142543

Hii ndi imekushtua , mbona hamfikii Prof Maji Marefu
 
Na wewe wataje unaowamini towa cv zao. Mbowe na slaa kama watu awapasuki kwa kucheka

Huwezi kujenga hoja bila kuwataja Mbowe na Slaa?Kuna mtanzania anaweza kucheka mafanikio ya Mbowe(jinsi anavyo deliver na Achievement yake?) kama haitakuwa wendawazimu ni nini?Unaweza kujiweka mahali pa mp.umb.avu ukacheka CV ya Dr Slaa lakini jiulize wewe baba yako ana CV gani tuijue?maana wewe unayeongea sidhani hata kama una elimu yoyote zaidi ya O level!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Imeandikwa kwenye Ukurasa wa FB wa hii kitu https://www.facebook.com/pages/Citizens-For-Kigwangalla/370119756463712

Wasifu Mfupi wa Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB).

Dr. Hamisi Kigwangalla, MB, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, alizaliwa Mwaka 1975, Mwezi Agosti, Tarehe 7 katika Hospitali ya Maweni, Kigoma. Akiwa ni mtoto wa kwanza wa Bwana Mahampa Kigwangalla na bibi Bagaile Lumola. Baba yake ni Mkimbu kutokea kijiji cha Goweko, Uyui, Tabora na Mama yake ni Mnyamwezi mzaliwa wa Nzega, huko huko Tabora. Wakati anazaliwa Baba yake alikuwa ni mtumishi wa benki ya NBC (ya zamani) na mama alikuwa ni mwalimu wa daraja la A. Alikulia mjini Nzega kwa babu na bibi yake baada ya wazazi wake kutengana.

Amesoma shule ya msingi Kitongo na Mwanzoli, Nzega. Sekondari alisomea Kigoma Secondary School, ambapo alifaulu vizuri masomo ya sayansi na kuchaguliwa kwenda kusoma Shinyanga Secondary School, kombinesheni ya Physics, Chemistry na Biology (PCB), ambapo alifaulu vizuri kwa division I na kuchaguliwa kusomea masomo ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Muhimbili University College of Health Sciences. Mwaka 2004, alihitimu masomo ya Udaktari wa Tiba na kutunukiwa digrii ya 'Doctor of Medicine' ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Alifanya internship katika hospitali ya taifa ya muhimbili na baadaye hospitali ya Mwananyamala. Baada ya hapo alipata fursa ya kusoma Masters of Public Health (MPH) katika Chuo Cha Karolinska Institutet na Master of Business Administration (MBA) akibobea zaidi kwenye Organization and Leadership, katika chuo kikuu cha Blekinge Institute of Technology - vyuo vyote hivi vipo nchini Sweden.

Sasa hivi, Dr. Kigwangalla anamalizia tasnifu yake ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) kwenye Public Health, akibobea zaidi kwenye Health Economics. Anaandika tasnifu yake kuhusiana na haki, usawa na uhalali wa mchakato wa bajeti kwenye sekta ya afya nchini Tanzania.

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali. Daktari daraja la II, Mtafiti na mtaalamu mshauri wa kujitegemea. Pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa makampuni yaliyo wanachama wa MSK Group, na amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Group hii kabla ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega. Kampuni ya MSK Group inaweza kukadiriwa kwa sasa kumiliki mali na madeni kwa kiwango cha TZS 10bn, na inazungusha kwa mwaka mtaji wa takriban TZS 4bn. Inaajiri watanzania wapatao 400 moja kwa moja (katika nyakati mbali mbali za mwaka), na zaidi ya 200,000 indirectly.

Dr. Kigwangalla amewahi kuanzisha na ama kushiriki harakati mbalimbali za kupambana na umaskini, maradhi, ujinga, ukosefu wa ajira kwa vijana, uonevu, utetezi wa wanyonge na wasiojiweza, mapambano dhihi ya VVU/UKIMWI, ulinzi wa raslimali za taifa na kuhakikisha watanzania wanafaidika na urithi wao n.k.

HK amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi kwenye chama chake, CCM (ambacho alijiunga rasmi mwaka 1994); amewahi kuwa chipukizi na kiongozi wa chipukizi wilaya ya Nzega, ameshiriki makambi mbalimbali ya vijana na halaiki, amewahi kuwa kijana wa Green Guard wa CCM, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, tawi la Kigoma Sekondari na Mjumbe, Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sikonge akiwawakilisha vijana. Kwa sasa ni Mjumbe, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Tabora, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nzega na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Hajawahi kujiunga na chama kingine chochote kile cha siasa. Amewahi kushiriki kampeni mbalimbali za uchaguzi na kujitolea kwa hali na mali kujenga chama chake.

Dr. Kigwangalla ni mwandishi mzuri wa vitabu, makala za kisayansi na makala za uchambuzi wa mambo mbali mbali ya kisiasa na kiuchumi kwenye magazeti mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.

Ni mwanamichezo, akipendelea zaidi kucheza soccer, basketball, tennis na Golf. Anapendelea mijadala ya wazi kwenye mitandao ya kijamii na ni mpenzi wa kusoma vitabu. Dr. Kigwangalla ana mke na watoto watatu, Sheila, Hawa na HK Jr.

View attachment 142543

kuna mambo mwandishi kasahau. nasikia kuna kigwangala FEKI na ORIGINAL. Sasa huyu ni yupi?Feki anatumia jina la original baada ya kuchemsha elimu ya msingi.
 
Huwa ninamkubali kielimu pamoja na michango yake bungeni katika wale uccm sana hayupo mara nyingi yuko neutral ingawa kuna muda naona wanamkeme arudi kundini ila rai yangu kwake kwa sasa Tanzania tulipofika hatuitaji mtu mwenye ma PHD mengi ila tunataka kiongozi wakuzionea uchungu rasilimali zetu, wakutusemeha wananchi matatizo yetu, kuona gep kubwa walionacho na wasio nacho, na kuweka maslahi ya taifa mbele na sio matumbo yao yuho ndio wakutunukiwa PHD lakini hata kama umesoma ukapitiliza kama elimu yako uitumii kwa maslahi ya watu nothing wewe ujasoma, taaluma yako ya afya iko hoi bin taaban bado wewe unasema Dr tena kiongozi tunaona watu wanaleta miswada mbalimbali ya sheria ktk taaluma zao wameguswa!!!! JE WEWE Unajadili posho zaidi, pigania taaluma yako utakuwa ni sadaka moja wapo utaokoa watoto, wanawake, wazee, vilema na maskini ambao ndio wanaitaji mmsaada mkubwa.
kila la kheri
 
Nini kinachotisha kwenye hiyo CV?,unaleta ushabiki hapa!!!
 
Vipi matatizo yeye na mshua wake ameyamaliza? - maana kuna wakati mshua alisema mwanaye huyu anabana sana mpunga kiasi inamfanya mshua wake aishi maisha kama ya digidigi - yaani ya kubahatisha - lishe shida, matibabu ya shida!
 
Hivi kwanini madaktari (MD) huwa wanakimbia fani ya utabibu na kwenda kwenye arts? Mfano mzuri ni huyu jamaa.
 
Labda inatisha wasiojua!

Lakini kwa wanaojua kuwa huyo bwana ni mwizi wa maandiko ya wengine wala hawatishwi.

Kwani CV ndo nini bana? Si maandishi tu hayo.

Kilichomo kichwani mwa mtu kwangu ndo cha muhimu zaidi.

Hivyo, hata uwe na mi PhD mia, lakini kama una tabia ya kuigilizia kazi za watu na kujifanya kuwa ni zako wewe kwangu ni bure tu!

Mkuu, tutupie hapa ile ya kwako ambayo ninzuri zaid isiyochanganya maandiko yaw engine.

Tanzania ukitaka maisha bora ingia kwenye siasa. Haijalishi umesoma kiasi gani au hujasoma.

Ndiyo maana hata Ma Prof wanaacha kazi za kufundisha vyuoni wanakimbilia kwenye siasa hasa CCM ili walale masikini na kuamka tajiri. Sishangai kwa CV iliyoko hapo juu.
 
huyu jamaa alitakiwa awepo hospitali kufanya kazi yake sasa huko bungeni si atasahau kufanya operesheni kwa wagonjwa? sasa sijui maana ya kusomea udaktari nini hapo.
 
Nadhani ni namna tu ilivyoandikwa, otherwise haina kitu cha ajabu kama title ya thread ilivyo.
 
weka performance CV yake na sio longolongo hizo. Kuwa nashule inachangiwa na fursa na uwezo wa wazazi na sio uelewa binafsi wa mhusika.
 
Imeandikwa kwenye Ukurasa wa FB wa hii kitu https://www.facebook.com/pages/Citizens-For-Kigwangalla/370119756463712

Wasifu Mfupi wa Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB).

Dr. Hamisi Kigwangalla, MB, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, alizaliwa Mwaka 1975, Mwezi Agosti, Tarehe 7 katika Hospitali ya Maweni, Kigoma. Akiwa ni mtoto wa kwanza wa Bwana Mahampa Kigwangalla na bibi Bagaile Lumola. Baba yake ni Mkimbu kutokea kijiji cha Goweko, Uyui, Tabora na Mama yake ni Mnyamwezi mzaliwa wa Nzega, huko huko Tabora. Wakati anazaliwa Baba yake alikuwa ni mtumishi wa benki ya NBC (ya zamani) na mama alikuwa ni mwalimu wa daraja la A. Alikulia mjini Nzega kwa babu na bibi yake baada ya wazazi wake kutengana.

Amesoma shule ya msingi Kitongo na Mwanzoli, Nzega. Sekondari alisomea Kigoma Secondary School, ambapo alifaulu vizuri masomo ya sayansi na kuchaguliwa kwenda kusoma Shinyanga Secondary School, kombinesheni ya Physics, Chemistry na Biology (PCB), ambapo alifaulu vizuri kwa division I na kuchaguliwa kusomea masomo ya Udaktari katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Muhimbili University College of Health Sciences. Mwaka 2004, alihitimu masomo ya Udaktari wa Tiba na kutunukiwa digrii ya 'Doctor of Medicine' ya chuo kikuu cha Dar es salaam. Alifanya internship katika hospitali ya taifa ya muhimbili na baadaye hospitali ya Mwananyamala. Baada ya hapo alipata fursa ya kusoma Masters of Public Health (MPH) katika Chuo Cha Karolinska Institutet na Master of Business Administration (MBA) akibobea zaidi kwenye Organization and Leadership, katika chuo kikuu cha Blekinge Institute of Technology - vyuo vyote hivi vipo nchini Sweden.

Sasa hivi, Dr. Kigwangalla anamalizia tasnifu yake ya shahada ya uzamivu (Ph.D.) kwenye Public Health, akibobea zaidi kwenye Health Economics. Anaandika tasnifu yake kuhusiana na haki, usawa na uhalali wa mchakato wa bajeti kwenye sekta ya afya nchini Tanzania.

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali. Daktari daraja la II, Mtafiti na mtaalamu mshauri wa kujitegemea. Pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa makampuni yaliyo wanachama wa MSK Group, na amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Group hii kabla ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega. Kampuni ya MSK Group inaweza kukadiriwa kwa sasa kumiliki mali na madeni kwa kiwango cha TZS 10bn, na inazungusha kwa mwaka mtaji wa takriban TZS 4bn. Inaajiri watanzania wapatao 400 moja kwa moja (katika nyakati mbali mbali za mwaka), na zaidi ya 200,000 indirectly.

Dr. Kigwangalla amewahi kuanzisha na ama kushiriki harakati mbalimbali za kupambana na umaskini, maradhi, ujinga, ukosefu wa ajira kwa vijana, uonevu, utetezi wa wanyonge na wasiojiweza, mapambano dhihi ya VVU/UKIMWI, ulinzi wa raslimali za taifa na kuhakikisha watanzania wanafaidika na urithi wao n.k.

HK amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi kwenye chama chake, CCM (ambacho alijiunga rasmi mwaka 1994); amewahi kuwa chipukizi na kiongozi wa chipukizi wilaya ya Nzega, ameshiriki makambi mbalimbali ya vijana na halaiki, amewahi kuwa kijana wa Green Guard wa CCM, amewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, tawi la Kigoma Sekondari na Mjumbe, Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Sikonge akiwawakilisha vijana. Kwa sasa ni Mjumbe, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM, Mkoa wa Tabora, Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nzega na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Hajawahi kujiunga na chama kingine chochote kile cha siasa. Amewahi kushiriki kampeni mbalimbali za uchaguzi na kujitolea kwa hali na mali kujenga chama chake.

Dr. Kigwangalla ni mwandishi mzuri wa vitabu, makala za kisayansi na makala za uchambuzi wa mambo mbali mbali ya kisiasa na kiuchumi kwenye magazeti mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.

Ni mwanamichezo, akipendelea zaidi kucheza soccer, basketball, tennis na Golf. Anapendelea mijadala ya wazi kwenye mitandao ya kijamii na ni mpenzi wa kusoma vitabu. Dr. Kigwangalla ana mke na watoto watatu, Sheila, Hawa na HK Jr.

View attachment 142543
So what?!
 
Anyway sijui lakini hii ni CV ya kawaida sana; ungebahatika kona maCV mengine naamini ungezimia na baada ya kuzinduka ungesema hii ya HK kumbe ni cha mtoto mchanga! Bahati mbaya wenye maCV kama hayo hayatangazwi na pia wao wenyewe hawajitangazi. Tuibue hoja za maana siyo kuzungumzia watu humu JF jamani!
 
Back
Top Bottom