Kumbe Ben Mkapa naye anaweza kufungwa...?

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Afrika imeshuhudia maajabu.

Waliokuwa marais wa Nchi mbili tofauti Bw HOSNI MUBARA wa Misri na Bw CHARLES TAYLOR wa Liberia kutumikia vifungo vya maisha kwa makosa ya mauaji, hapa kwetu Tanzania chini ya uongozi wa Mkapa Nchi iliwahi kushuhudia mauaji huko zanzibar, ingawa ilipita kimya kimya lkn kumbe baada ya urais kuna maisha mengine .

Sijui Mkapa na wenzake wanatambua hili....?
 
2015 ccm ikipigwa chini,jk na mkapa watapishana kwenye lango kuu la segerea na babu seya's
 
Nitafurahi sana nikimuona Che Nkapa akiwa amevaa lile kaptura la rangi ya chungwa.Damu za wapemba aliowachinja na wakina mama kubakwa na mapolisi wake zingali zikimlilia toka kaburini mpaka siku na yeye atakapohukumiwa kwa udhalimu wake
 
Ndio anaweza kufungwa au kuachiwa na Mahakama, kama itathibitisha hana cha kujibu katika shutma na tuhuma zinazomkabili mpaka dakika hii.
Kwa kisingizio sahihi kuwa Katiba inampa Kinga hilo limeshindikana lakini
KATIBA hiyo hiyo imewapa WABUNGE utaratibu wa kuliwezesha hilo la kumfikisha Mahakamani. Kwa vile Wabunge wetu wamekosa MAKODO ya ujasiri hiki Kitendawili kitaendelea kusubiri jibu..............nasi tuwe tayari kusubiri jibu, sio Mji.
 
Hawa wawili wa mwisho - wameua mno jamani! bora wanasheria walisimamie hili iwe fundisho kwa maraisi tutakaowachagua mbeleni
 
Tenda wema nenda zako, marais wanatakiwa kutenda hivyo lakini wakifika kwenye kile kiti cha enzi wanabadilika kabisa wanageuka Miungu watu sasa dawa yake ni Okampo..
 
Tuweke maoni katika kurekebisha katiba, kwani kwa katiba ya sasa huwezi kufanya jambo hili.

Tubadilishe Katiba kwanza kisha kila kitu kinawezekana hata kuwafungulia mashitaka mapya mafisadi.

Na pia ieleweke kuwa hata JK, sidhani kama atatoka katiak hilo tundu la ICC.




MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Tuweke maoni katika kurekebisha katiba, kwani kwa katiba ya sasa huwezi kufanya jambo hili.

Tubadilishe Katiba kwanza kisha kila kitu kinawezekana hata kuwafungulia mashitaka mapya mafisadi.

Na pia ieleweke kuwa hata JK, sidhani kama atatoka katiak hilo tundu la ICC.




MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
Mkuu usitegemee hata siku moja kuwa Mkapa au Kikwete anaweza kufikishwa ICC. Hawa wamewawezesha sana hao mabwana zao kwa raslimali zetu. Sioni kama tunaweza kushindwa kuwabana kwa sheria zetu kwani kama ambavyo tumekuwa tukisikia, hata sheria ya sasa haiwalindi kutoshtakiwa kwa makosa ambayo hayahusiani na majukumu ya urais.
 
Hizi sheria ZInazotungwa kwa msaada mkubwa wa Chenge Fisadi kuangalia inampendelea mkuu hakuna wa kuwapeleka lupango
 
Back
Top Bottom