Charles Taylor ataendelea kutumikia kifungo chake nchini Uingereza

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Charles Taylor.jpg
Mahakama Maalum ya Umoja wa Mataifa inayosikiliza mashtaka dhidi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor imesema kiongozi huyo wa zamani ataendelea kutumikia kifungo chake nchini Uingereza, na si nchini Liberia kama alivyoomba hapo awali kutokana na kigezo cha usalama.​
Kiongozi huyo wa zamani alikuwa ameomba kutumikia kifungo chake nyumbani nchini Liberia, akitumikia kifungo cha miaka 50 mwaka 2012 kutokana na makosa ya kivita aliyoyatenda akiwa madarakani. Taylor alipatikana na hatia katika kesi iliyotolewa hukumu na Mahakama Maalum kwa Sierra Leone, na amekuwa akitumikia kifungo hicho nchini Uingereza huku maombi yake ya kurudishwa barani Afrika yakikataliwa mara kwa mara na mahakama hiyo kwa kigezo cha usalama.​
Ombi la mwisho alilolitoa Taylor lilikuwa kwa kigezo cha hatari ya afya yake kutokana na mlipuko wa virusi vya corona akidai kuwa gereza la HMS Frankland alipokuwa akishikiliwa lina idadi kubwa ya wafungwa na kuomba kuhamishiwa nchi yoyote "salama barani Afrika." Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague nchini Uholanzi lilikanusha ombi lake lenye zaidi ya kurasa 26 ikisema kuwa ombi lake haliendani na taarifa ya maafisa wa gereza hilo.​
Hakimu wa mahakama hiyo amesema kushindwa kuainishwa kwa nchi hiyo ya Afrika kumechangia kukataliwa kwa ombi hilo, akiongeza kuwa Taylor yupo salama zaidi nchini Uingereza kuliko sehemu yoyote duniani. Jaribio kama hili lilishindwa mwaka 2013 ambapo Taylor alitaka kuhamishiwa nchini Rwanda ambapo wafungwa wote wa mashtaka ya uhalifu wa kivita nchini Liberia wanatumikia vifungo vyao.​
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilidumu kwa muda wa miaka 11 vikigharimu maisha ya zaidi ya watu 50,000 vikiwahusishwa waasi wa Revolutionary United Front (RUF) ambao baadaye walipata uungwaji mkono wa Rais Taylor. Alihukumiwa kwa mashtaka 11 yakiwamo ya kuwaunga mkono waasi.​
 
gereza la HMS Frankland alipokuwa akishikiliwa lina idadi kubwa ya wafungwa na kuomba kuhamishiwa nchi yoyote "salama barani Afrika." Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague nchini Uholanzi lilikanusha ombi lake lenye zaidi ya kurasa 26 ikisema kuwa ombi lake haliendani na taarifa ya maafisa wa gereza
huyu akiletwa segadanse hata wiki hamalizi.

Lakini mleteni, Kuna mwenzake wataungana siku SI nyingi
 
Naomba kuuliza, ni nani huwa mlalamikaji mpka Mh rais anatiwa hatiani?

Na Je wanaohukiwa na hii mahakama ni marais tu au hata viongozi wa ngazi za kawaida?
 
Back
Top Bottom