Kumbe bei ya sukari Kenya ni maradufu ya Tanzania

Hiyo labda ni pkt ya 2kg.
Sukari kenya ni 1.0 kg = KES 130.00, inategemea unanunua wapi.
Ingekuwa kilo ya sukari Kenya ni TZS 6000, basi sukari yote ya Tanzania ingeishia kenya kwa magendo?
Yaani hata Mimi nilikuwa naweweseka hapa. Yaani tofauti ya sh.3500 wakati njia za panya za kupita zipo kibao watu wangepiga hela mpaka basi kwa black market, tofauti kubwa sana hiyo kwa nchi zinazopakana hivyo haiwezi kutokea na biashara ikaenda kama kawaida. Labda nchi yenyewe iwe kama North Korea ambayo mipaka inalindwa kwa nyaya za umeme. Mleta mada fanya uchunguzi tena
 
.
kilo moja ya kupima na ile iliyofungwa vizuri haina tofauti, kilo ni kilo tuu.

Lakini hata ukiikokoto hiyo bei ya $1.53 kwa 1.81Kg unapata sawa $0.83 kwa 1kg ambayo ni sawa na Tsh 1992 kwa 1kg ambayo siyo mbaya sana na hasa ukiangalia uchumi wetu ulivyo mdogo.

Kinachofanya bei ya vitu kuwa ndogo Marekani ni pamoja na bei ya mafuta kuwa chini, kwahiyo kufanya gharama za usafirishaji wa bidhaa kuwa chini na hivyo kushusha bei ya vitu mbalimbali.
Kwa hiyo unataka kusema kutengeneza mifuko 50 ya kilo moja moja ni sawa na gharama ya kutengeneza mfuko mmoja wa kilo 50. Pia sukari yetu ubora wake ni wa chini sana kulinganisha na hiyo.......
 
Asante Kiongozi kwa kuleta fact lakini kama kawaida huwezi kukosa wa kupinga Tanzania tuna tatizo la wapinzani kwao ilimradi wao wanaitwa wapinzani basi ni kupinga kila kitu na kufanya kionekane kibaya.

Acha ushamba unakula packages au unakula Sukari? Unashadadia package wakati ukiitoa tu dukani unaiweka kwenye container ya sukari hoja yako ni ya kitoto kama zilivyo nyingi kutoka kwenu.

Hiyo hiyo Sukari ya Tanzania inauzwa mpaka nchi za kiarabu tena hakuna sukari standard kama za Africa ukilinganisha na chemicals stimulated manufactured za most of the western countries.

Alafu hujalazimishwa kununua sukari ya Tanzania kanunue ya Marekani.

Kuwa mzalendo sio kusema uongo......Sukari yetu tu haitutoshi halafu tukauze uarabuni,halafu umasikini wetu ustufanye tuwe tunapewa bidhaa mbovu sokoni.Eti leo hii tunambavu za kubishana na Marekani kwenye viwanda.
 
Bei ya sukari nchini Kenya ni USD 2.5 per kilo sawa na TSh 6,000 kwa kilo.

Source: ITV taarifa ya habari saa 2 usiku leo.

My take: Bei ya sukari hapa kwetu ni TSh 2,500 lakini kuna mijitu imekuwa imekuwa ikitoa mapovu kulalamikia bei hii na kuiona kama ni kick ya kisiasa dhidi ya serikali.
Bei ya kilo ya sugar UK ni mpaka £3, exchange rate ni almost 3,000 TZS. Kwa hiyo kilo kwa UK ni 9,000 za Tanzania
Hapo unasemaje. Its about the economy and purchase power.
 
Bei ya sukari nchini Kenya ni USD 2.5 per kilo sawa na TSh 6,000 kwa kilo.

Source: ITV taarifa ya habari saa 2 usiku leo.

My take: Bei ya sukari hapa kwetu ni TSh 2,500 lakini kuna mijitu imekuwa imekuwa ikitoa mapovu kulalamikia bei hii na kuiona kama ni kick ya kisiasa dhidi ya serikali.
kwaio kama kwao bei na sisi iwe hvo hvo? Stupid
 
Bei ya sukari nchini Kenya ni USD 2.5 per kilo sawa na TSh 6,000 kwa kilo.

Source: ITV taarifa ya habari saa 2 usiku leo.

My take: Bei ya sukari hapa kwetu ni TSh 2,500 lakini kuna mijitu imekuwa imekuwa ikitoa mapovu kulalamikia bei hii na kuiona kama ni kick ya kisiasa dhidi ya serikali.

Sawa kabisa, ngoja tuendelee kujilinganisha na Kenya rais wao anaendesha nchi kwa katiba ya wananchi, mihimili ya utawala inajipambanua.

Tz mahakama na bunge viko mfukoni mwa mtu. Katiba na sheria havieshimiki.

"Kiongozi aliyeapa kuilinda katiba, asipoiheshimu katiba HATUFAI kabisa" mwl. Nyerere
 
Kenya Hawana hata Shamba LA miwa, sukari yao ni imported 100%. Sisi tuna viwanda lukuki vya sukari na bei ilitakiwa kuwa chini ya 2500
 
Hiyo labda ni pkt ya 2kg.
Sukari kenya ni 1.0 kg = KES 130.00, inategemea unanunua wapi.
Ingekuwa kilo ya sukari Kenya ni TZS 6000, basi sukari yote ya Tanzania ingeishia kenya kwa magendo?
...Uko sahihi, juzi nilikuwa maeneo ya Kileo, Mwanga huko Moshi, mpakani kabisa na Kenya (upande wa Kitobo Kenya), nilishuhudia bodaboda nyingi vinapita from Kitobo na madumu ya mafuta ya taa wakielekea Moshi, kwa njia ya panya road. Baada ya kuuliza nikaambiwa Kenya mafuta ni very cheap kiasi kwamba boda boda wanaenda kununua huko na kuhonga mpakani and yet wanapata faida. So kama sukari ingekuwa cheap hivyo wangekuwa wanaipeleka pia.
 
2015 sukari ilikua 1800 tsh/kg, mwaka 2017 ni 2600tsh/kg. Halafu unasema Rais anafanya vizuri?

Bei ilikuwa ndogo kwasababu ya rushwa ya ukwepaji kodi, mheshimiwa katibua tibua dili za watu kwahiyo bado kuna mkorogo wa maji na tope. Mpe muda Mh. Rais, tope likitua utaona maji yalivyo safim bei za bidhaa zitashuka na uchumi kupaa.
 
Kwa hiyo unataka kusema kutengeneza mifuko 50 ya kilo moja moja ni sawa na gharama ya kutengeneza mfuko mmoja wa kilo 50. Pia sukari yetu ubora wake ni wa chini sana kulinganisha na hiyo.......

Inawezekana kabisa kama kuna automated system ya kujaza hiyo mifuko kwa haraka na ufanisi, gharama itapungua.

Pia sukari yetu ubora wake ni wa chini sana kulinganisha na hiyo.......
.
Siyo kila kitu cha Marekani ni bora kuliko Tanzania, kwa mfano nyama, kuku, maziwa, mboga za majani na hata matunda huwa hayana ubora kama vile vya Tanzania (hata ukionja tuu utaona). Ukitaka vyakula bora fresh (kama vya bongo) kwa mfano ni lazima ununue vile vinavyoitwa organic ila bei yake ni zaidi ya mara tatu hata nne vile vya kawaida.
 
Inawezekana kabisa kama kuna automated system ya kujaza hiyo mifuko kwa haraka na ufanisi, gharama itapungua.

.
Siyo kila kitu cha Marekani ni bora kuliko Tanzania, kwa mfano nyama, kuku, maziwa, mboga za majani na hata matunda huwa hayana ubora kama vile vya Tanzania (hata ukionja tuu utaona). Ukitaka vyakula bora fresh (kama vya bongo) kwa mfano ni lazima ununue vile vinavyoitwa organic ila bei yake ni zaidi ya mara tatu hata nne vile vya kawaida.

Najua kuna machine ya kufanya hivyo ila gharama ya kuwekeza kwenye machine ya aina hiyo ni gharama......pia hata sukari yetu inajazwa na mashine. Kwenye hili la sukari wametuzidi kwa kila kitu tukae na kukubali tu.

Marekani na nchi zilizoendelea wanajua changamoto ya kulisha dunia, hivyo kulima kwa kienyeji kama bongo ni changamoto kubwa sana. Jaribu kufikiria 90% wanatumia maziwa kila siku sasa kukidhi mahitaji inabidi wafanye ukulima huo.
 
Kila kitu kinategemea na uchumi wa nchi husika, mfano ukiuza kilo ya Sukari uingereza kwa Tsh 8,000 watasema ni fake. Kikombe cha kahawa Ulaya kinaenda hadi Tsh 7000, wakati hapa kwentu hakizidi 1000
 
Bei ya sukari nchini Kenya ni USD 2.5 per kilo sawa na TSh 6,000 kwa kilo.

Source: ITV taarifa ya habari saa 2 usiku leo.

My take: Bei ya sukari hapa kwetu ni TSh 2,500 lakini kuna mijitu imekuwa imekuwa ikitoa mapovu kulalamikia bei hii na kuiona kama ni kick ya kisiasa dhidi ya serikali.
Usikurupuke wewe! Ni sh. 2600 kwa kilo mbili, Kenya bidhaa zao huwa wanafungasha kilo mbili mbili.
 
dc52477c27e7805edb308ec85132ecd4.jpg
 
Kumbe wewe hujawahi kuishi vijijini ambako aslimia 80% ya watanzania ndiko wanakoishi? Kwao sukari is none of their buisiness. Wanaishi kwa natural diet na hivyo magonjwa kama ya kisukari, ma high blood pressure na vidole tumbo (appendicitis) hayawasumbui. Na hawa ndiyo wenye maamuzi ya nani au chama gani kitawale kwani ndiyo wenye kura nyingi. Hivyo kick ya bei ya sukari kwao ni irrelevant. Wanachohitaji ni maji, huduma bora za afya, barabara na bei nzuri ya mazao yao ya kilimo na kutobuguziwa na kodi za ovyo ovyo za mazao yao ya kilimo na mifugo yao.
Mh, nimekuelewa ingawa unafikiri kinyumenyume. Waliwahi kukwambia kwamba hawahitaji sukari? uliwahi kuwapelekea sukari wakaikataa? kesho pia utasema hawahitaji kula nyama kwa sababu wanakula kisamvu natural! That is weird.
 
Kuna chama kwenye kampeni yao kipao mbele cha kwanza hadi cha tatu ni Elim,nazidi amini kumbe waliona mbali,

Mode mawazo kama haya muwe mnafuta ,

Asanteni
 
Back
Top Bottom