Kumbe Azam Energy ni balaa kiasi hiki!?

Kumbe Azam Energy ni balaa kiasi hiki!?

Hii ni hatari wakuu, hii kitu haiwezi kuwa na athari za kiafya hapo baadae kweli?

Hii ni mara ya tatu natumia, mwanzo nilikuwa sijagundua. Nimegundua kuwa siku ninazotumia huwa nafanya kazi usiku kucha huku Mkono bado ukiwa Imara.

Sasa leo nimeendesha gari usiku kucha, Abiria wangu yuko hoi lakini bado mkono wangu uko imara na umenyooka tu! Yaani bado nahitaji kuendelea na safari.

Wakuu hii kitu haiwezi kuleta madhara kweli hapo baadae tukashindwa kabisa kuendesha?
Hyo ni balaa ukichanganya na konyagi alafu upate na supu ya mdudu wa baharini
 
Nahisi toka uzi huu umeanzishwa kwa mkoa ambao una members wengi wa kiume hasa Dar saizi depot nyingi wameshafunga hesabu...chochote chenye kuongeza nguvu wanavyoamini wao na nguvu za kiume kinaongeza,basi na mvua hizi ndiyo balaa zaidi!
 
Ila pia nadhani ni rahisi sana kuwa addicted ukishakizoea. Najitahidi sn kupambana kuiacha.

Njia rahisi ya kuacha nashauri usifanye mbadala wake kuwa maji. Hii ni kwa sababu ubongo umeshauzoesha kitu fulani kitamu kitamu.

Nilivyofanya mimi (and I'm still trying) ili kuacha mazoea ya hyo kitu, nilitafuta sehemu wanapotengeneza juice ya miwa. Nikawa nanunua juice iliyojaa chupa kubwa ya maji ya lita 1.5, nakunywa taratiiibu mpk inaisha.

With time, najiona kabisa naisahau Azam Energy.
 
Sababu ya mambo haya vijana wa leo ambao ndo wazee wa kesho mitarimbo yao itakuwa ishalala doro zamaanii kabla jua halijazama dadeki...

Ila endeleeni tu hakuna aijuae kesho hahaha
 
Yes hizi energy drinks zote zina side effects mbaya sana,kama ni dereva unaendesha masafa marefu epuka fatique,kila baada ya masaa mawili simamisha gari ,park sehemu safe toka nje na jinyoshe,kimbia kimbia,kunywa maji,fungua vioo ili fresh air iingie ndani ya gari,then endelea na safari ukiona umechoka park gari na lala,hivi vinywaji vyenye caffine sio vizuri.
Hahaaha mkuu una umri gani?
 
Ilitaka kuniulia usingizini nilikua nimechoka sana nilifanya kazi usiku kucha nikawa nimechoka sana nikasema ngoja nishtue kamoja kupunguza uchovu baada ya kama nusu saa nikajipumzisha usingizi ukanipitia l, Kilicho niamsha ni kupaliwa kwa dam, nilishtuka nimepaliwa dam zinatoka puani godoro lote chepe chepe damu utadhani mbuzi kachinjiwa hapo. Sina ham na hiyo kitu, ila nilipo uliza tatizo ndo nika ambiwa ni hiyo kitu. Ni kwamba msukumo wa dam ulifanya kazi mara mbili ya kawaida kwahiyo mishipa midogo ilipasuka kwa kuzidiwa na presha ile. Hata Red Bol iko hivyo
 
Ila pia nadhani ni rahisi sana kuwa addicted ukishakizoea. Najitahidi sn kupambana kuiacha.

Njia rahisi ya kuacha nashauri usifanye mbadala wake kuwa maji. Hii ni kwa sababu ubongo umeshauzoesha kitu fulani kitamu kitamu.

Nilivyofanya mimi (and I'm still trying) ili kuacha mazoea ya hyo kitu, nilitafuta sehemu wanapotengeneza juice ya miwa. Nikawa nanunua juice iliyojaa chupa kubwa ya maji ya lita 1.5, nakunywa taratiiibu mpk inaisha.

With time, najiona kabisa naisahau Azam Energy.
Sasa mkuu ulikua unatumia ili iweje? Au una Lindo mahali?
 
Back
Top Bottom