Kumbe Azam Energy ni balaa kiasi hiki!?

Kumbe Azam Energy ni balaa kiasi hiki!?

Duh kunawanaume hawawezi kupiga mzigo bila hayo makitu?
 
HAYA NDIO MADHARA YA AZAM ENERGY DRINK IKITUMIKA VIBAYA..


Watanzania wamekipokea na wanakitumia sana, kifupi kinauzika, huu ndio ukweli. Na mimi pia siku moja nilijaribu kukionja kutaka kujua kina ladha gani kinywaji hiki? Kinywaji hiki kinaitwa ENERGYDRINK

Je, ni wangapi tumeshawahi kusoma maelekezo yaliyoandikwa kwenye kopo la kinywaji hiki?

Baada ya kufungua na kuonja kwa mara ya kwanza kilinishinda kurudia fundo la pili, nikajua labda huenda ni gesi ngoja nikiache kwa muda kidogo, lakini hata baada ya kukirudia tena bado kilinishinda.

Nikajikuta navutiwa kusoma kimeungwa kwa kutumia viungio gani (ingredients). Hiki nilichokiona ndicho kilichonifanya niandike haya.

Malengo sio kuharibu biashara yako la!, ni kuwajuza Watanzania ambao wengi wetu lugha iliyotumika hapa ni changamoto kuijua, lakini pia wengi wetu huwa hatuna utamaduni wa kusoma hivi vibandiko kabla ya kutumia.

NI NINI NILICHOKIONA NA KIKANISTUA? HIKI HAPA!

1. INGREDIENTS (VIUNGIO)
Water sugar, Carbondioxide, Citric acid (E330), Taurine, Acidity Regulator Sodiumcitrates E331, Colour plain, Caramel E150a, CAFFEINE, Inositol, Preservative Potassium Sorbate E 202, Flavouring, Niacin, Pantothenic Acid, Vitamin B6, B12
Baada ya kuandikwa hivi viungia ukiangalia katika chupa hii kilichofatiwa ni muda wa matumizi na mahali kinapozalishwa. Lakini bado sikupata mantiki kwanini kimekuwa kikali mno, kwanini!!

Ghafla katika kudadisi zaidi ndipo chini ya maandishi hayo nikakuta maandishi mengine mapya, tena yamewekwa juu ya wino MWEKUNDU; kuashiria TAHADHARI bila kuandikwa neno lenyewe la TAHADHARI.

Maandishi haya yameandikwa katika lugha ya Kiingereza yanasomeka hivi:

"High caffeine content (31.5mg/m100) Taurine(0.03%). Do not Drink More than 2battles per Day, Not suitable for persons Sensitive to Caffeine, Children, Pregnant, Breast feeding women and Avoiding Drinking before sleeping".

TAFSIRI YA MANENO HAYA KWA TUSIOJUA!
Ina kiasi kikubwa cha CAFFEINE, Usinywe zaidi ya chupa 2 kwa siku, Haifai kwa watu wenye matatizo na CAFFEINE, haifai kwa watoto, wajawazito, wanamama wanaonyonyesha na mwisho Usitumie muda mfupi kabla ya kwenda kulala kinywaji hiki.

Kwanini usinywe muda mfupi kabla hujakwenda kulala?

Kiwango cha 31.5mg/ml100 za caffeine ni nyingi kwa matumizi ya kawaida hivyo kuna hatari ya blood pressure kushuka ukiwa usingizini na hatimaye ukapoteza maisha, hivyo ni hatari kunywa wakati unakwenda kulala, inaathiri ubongo pia kwa watoto na hata watu wazima, pia kwa wajawazito na wanaonyonyesha.

Sasa Mzee wangu Bakhress ni watanzania wangapi wanatumia kinywaji hiki pasipo kujua? Kuna wajawazito watoto, wazee wote wanakibugia tu hawajui kinachoendelea katika kinywaji hiki mzee.

Sina uhakika, lakini inawezekana kikapita hata kiwango cha kwenye Heinken. Caffeine drink kuna baadhi ya nchi kama Ufaransa, Marekani, Hispania, Uingereza wamepiga marufuku kutokana na athari zake, hasa katika ubong

Hakuna shaka Mzee baada ya muda mfupi wa matumizi ya kinywaji hiki, watanzania wengi hasa kina mama na watoto na hata wanaume watapata matatizo haya;

Mfumo wa ubongo kuathirika (hili halina shaka), Vidonda vya tumbo, kwa wanamama wajawazito wanaobugia pia watazaa watoto wenye matatizo hasa akili kutokana na Ubongo kuathiriwa, wanaonyonyesha pia!

Mzee, kama ujumbe huu utakufikia naomba tuondolee janga hili, maana haya matatizo tuliyonayo yanatushinda. Watanzania wengi wataumia SIKU CHACHE ZIJAZO na hazipo mbali.

Caffeine ni nini?
Caffeine is a central nervous system stimulant of the methylxanthine class of psychoactive drugs. It is the world's most widely consumed psychoactive drug, but unlike many other psychoactive substances,



EEEEEBWANA EEEEEE.
 
Vijana huku uswazi wanazinywa sana ila huwa wanakunywa jirani na nyumba za wauza gongo kuna mangi mmoja ana duka hapa mtaani anakwambia kinywaji kinachotoka kuliko vyote ni azam energy nadhani watakuwa hawa vijana wanamix na gongo.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Chochote chenye kukupa nguvu ya ziada nje ya asili kina madhara
Kibaya zaidi kuna wale wanaochanganya na konyagi huwa nawaonea huruma sana, ni vile tu hawajui ni sumu gani inayoenda kutengenezwa ndani ya mwili
 
Madhara yake ni makubwa kuliko unavyozania pata ushauri wa daktari utavifahamu na hutotumia tena itafika wakati utaweka jiwe inaruka unaweka kigogo inaruka moja haikai mbili haipatikani abilia anatoka nduki unabaki mwenyewe
 
BmDSEcMIAAAw5b9.jpg:small
 
Nafikiri hii kitu huenda ikawa mbadala wa vumbi la kongo kwa wanaume wa Dar!!
 
Hizo ni energy drink mkuu zina madhara sana ongeza nguvu kwa asili mfano penda kunywa juisi ya ndizi na tikiti maji hiyo ni natural energy drink
 
Yes hizi energy drinks zote zina side effects mbaya sana,kama ni dereva unaendesha masafa marefu epuka fatique,kila baada ya masaa mawili simamisha gari ,park sehemu safe toka nje na jinyoshe,kimbia kimbia,kunywa maji,fungua vioo ili fresh air iingie ndani ya gari,then endelea na safari ukiona umechoka park gari na lala,hivi vinywaji vyenye caffine sio vizuri.
 
Back
Top Bottom