LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,349
- 36,302
Yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya kuhifadhiwa kwa mwili wa mpendwa wetu,Muasisi wa Makanisa na Huduma za wokovu nchini Tanzania, Marehemu Askofu . Dk. Moses Kulola, imefahamika kuwa Mwanajeshi huyu wa kiroho aliyetumikia Jeshi la BWANA YESU katika kipindi chote cha maisha yake ya hapa duniani alikuwa ni mtu wa nyota ya MAPACHA ama GEMINI. Kinyota , watu waliozaliwa kati ya MEI 20 na JUNI 21 ni watu wa NYOTA YA GEMINI. Imefahamika kuwa Marehemu Askofu Kulola alizaliwa tarehe 02 JUNI 1930. SIFA KUU ya watu wa NYOTA ya GEMINI, huwa ni kufanya mambo makubwa sana na ya kipekee sana iwe ni katika michezo, sanaa, uongozi, utumishi,elimu nakadhalika. . Maisha ya watu wa mapacha huongozwa (kwa kujua ama kutokujua ) na nishati " energy " inayo patikana kwenye andiko linalopatikana kwenye kitabu cha ECCLESIASTES 9:10
" Whatever your hand finds to do, do it with all your might, for in the realm of the dead, where you are going, there is neither working nor planning nor knowledge nor wisdom. ".
Ndio maana chochote kile akifanyacho mtu wa nyota ya mapacha huwa kinafanikiwa sana iwe ni kizuri ama kibaya. Utafiti unaonyesha kuwa , karibu katika kila eneo la maisha ya mwanadamu kuanzia kwenye michezo, uongozi,sanaa, biashara, elimu nakadhalika , kuna mtu wa nyota ya mapacha ambaye anachukuliwa kuwa wa kipekee sana katika eneo hilo husika...
N.B: Ninaomba radhi kwa nitakao kuwa nime wakwaza kwa kulihusisha jina la Marehemu Askofu Kulola na mambo ya nyota, ila kwa wasio fahamu, elimu ya nyota ipo toka enzi za Pontyo wa Pilato, hata wale Mamajusi walitumia nyota kugundua kuwa Mfalme Yesu amezaliwa.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI, NA AWAFARIJI WAFIWA. AMINA