Kumbe 2016 tulikopa tril 2.7 Benki ya dunia na tumeomba mingine, huku tunaambiwa ni kodi za ndani. Tunamatumizi makubwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,568
2,000
PIC+RAIS.jpgKwa ufupi
  • Baadhi ya maeneo ya kipaumbele ni miundombinu na hasa ya barabara na reli.
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Benki ya Dunia imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi ya maendeleo nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Mwakilishi wa benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird amesema hayo alipozungumza na Rais John Magufuli.

Bella ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 4,2017 Ikulu jijini Dar es Salaam na kubainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu na hasa ya barabara na reli; kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme; Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na elimu kwa kujielekeza katika ubora na kuhakikisha idadi ya wanaopata elimu inaongezeka.

Maeneo mengine ni kuboresha sekta ya afya, kuongeza upatikanaji wa maji, usimamizi bora wa ardhi, mawasiliano, huduma za fedha jumuishi, vituo vya pamoja vya Serikali na kusaidia familia masikini.

Bella amempongeza Rais Magufuli kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Benki ya Dunia. Amemuahidi benki hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mingine.

“Mwaka uliopita Benki ya Dunia ilitoa mikopo nafuu yenye thamani ya dola 1.2 bilioni za Marekani (Sh2.7 trilioni), fedha hizi zimekwenda katika miradi na tunafurahi kuwa inakwenda vizuri na wananchi wanafurahia; kwa sasa tunapanga namna tutakavyotoa mikopo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika kipindi kijacho,” amesema Bella.

Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano na Tanzania na amemhakikishia Bella kuwa Serikali itasimamia fedha zote zinazotolewa na benki ili zilete matokeo yanayotarajiwa.

Amesema maeneo ambayo benki hiyo imeyataja kuwa ya kipaumbele katika fedha zitakazotolewa ni muhimu kwa ustawi wa Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom