Kulikoni Waziri Liberata Mulamula! Au Ameparura Mahali?

"Balozi namba mbili ni waziri wa mambo ya nje. Kazi yake kubwa ni kumshauri balozi namba moja ambaye ni rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Prof. Palamagamba A.J Kabudi

"Naamini ntakuwa mshauri mkuu kwa Mhe.Rais".Mhe.Liberata Mulamula

 

Monday, May 23, 2022​

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND​


Na Mwandishi wetu, Dar
Mkutano wa 19 Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika Bara la Afrika na Nordic unatarajiwa kufanyika Helsinki, Finland kuanzia tarehe 13 – 15 Juni, 2022. Mkutano huo utakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika bara la Afrika na nchi za Finland, Norway Denmark, Iceland.
Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan amebainisha hayo alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mhe. Swan amesema mkutano huo utajadili masula ya amani na usalama, maendeleo endelevu na ushirikiano kati ya nchi za NORDIC na Afrika.
“Mkutano huo utajadili masuala ya amani na usalama, kuhusu umuhimu wa umini pamoja maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Swan.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema mkutano huo
umekuwa ukifanyika kila mwaka lakini kutokana na Janga la ugonjwa wa Uviko 19, mkutano huo haujafanyika tangu ulipofanyika mara ya mwisho nchini mwaka 2019.
Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Dkt. Donald Wright.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika sekta za Afya, Elimu, biashara na uwekezaji.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
Waziri Liberata Mulamula yupo na siku chache zilizopita alikuwa na Rais Samia kwenye ziara ya Nchini Uganda na akasaini mikataba kadhaa kwa niaba ya serikali.
Sukuma Gang punguzeni chuki na mnatakiwa kuamini yule bedui ameshakufa na hatorudi tena duniani.
 

Saturday, May 21, 2022​

WAZIRI MULAMULA AFANYA ZIARA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA KESI MASALIA ZA MAUAJI YA KIMBARI (IRMCT)​

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya ziara ya kikazi katika Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) tarehe 21 Mei 2022 katika eneo la Lakilaki, jijini Arusha.
Pamoja na mambo mengine dhumuni la ziara hiyo lilikuwa kukutana na Uongozi wa IRMCT na kujadili utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimsingi unaofanywa na taasisi hiyo sambamba na yale ya kimahakama.
Waziri Mulamula alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Tanzania inathamini imani inayotolewa na mashirika ya kimataifa pamoja na kikanda ya kuifanya kuwa mwenyeji wa mashirika hayo na kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania.
‘’ Serikali inafuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Mahakama hii, hivyo ni vema mkatekeleza kwa tija malengo mahsusi ya kuanzishwa kwake,” alisema Balozi Mulamula.
Pia akasisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano wa kiutendaji wakati wowote itakapohitajika ili kuiwezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kukamilisha taratibu za kesi zilizosalia na lile la kuwa kituo cha kumbukumbu kwa kesi hizo linatekelezwa kwa ufanisi.
Naye Msajili wa Mahakama hiyo Bw. Abubaccar Tambadou amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mulamula kwa kuthamini Mahakama hiyo na kutenga muda wake kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.
Pia akaeleza kuwa kikao hicho kimewezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa papo kwa papo katika baadhi ya mambo na kuleta uelewa wa pamoja kati ya uongozi wa Mahakama na Serikali mwenyeji juu ya masuala ya kiutendaji wa taasisi hiyo.
Naye Jaji wa Mahakama hiyo Mheshimiwa William Sekule alifafanua kwa kina juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimahakama na pia akaeleza kuwa kufanikiwa kwa Mahakama hiyo kunahitaji msaada kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nchi mwenyeji katika kutetea maslahi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa shughuli za taasisi.
‘’Naipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupigania upatikanaji wa bajeti ya uendeshaji wa Mahakama, hivyo ni vema tukatambua thamani ya mahakama hii kuendelea kuwepo nchini na kukamilisha majukumu yake,” alisema Jaji Sekule.
Tangu Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe Azimio Nambari 1966 mwaka 2010 la kuanzisha Mahakama hiyo nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisimamia hatua mbalimbali za awali ili kuhakikisha ujenzi wa Mahakama hii unakamilika hususan upatikanaji wa eneo la ujenzi, uwepo wa huduma ya umeme, barabara na maji katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
================================================

 

Tuesday, May 17, 2022​

BALOZI MULAMULA ATETA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA SWITZERLAND​


Na Mwandishi Wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Nchini Switzerland katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula ameuhakikisha ujumbe wa wafayabiashara hao kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni salama na hivyo wasisite kuwekeza.
“Serikali imejitahidi sana kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hivyo nawasihi kutumia fursa hiyo kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo, kilimo, nishati, madini na nyinginezo," alisema Balozi Mulamula
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 'Global Network', Bw. Stefan Barny emeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa maboresho makubwa katika sekta ya biashara na uwekezaji.
“Mazingira ya biashara hapa Tanzania nilikuwa nayasikia tu, ila baada ya kuja na kuonana pamoja na kujadiliana na wadau wa sekta za biashara na uwekezaji tumeridhishwa na mazingira ya biashara hapa Tanzania,” alisema Bw. Barny.
Bw. Barny ameongeza kuwa atawashawishi wafanyabiashara wenzake kutoka Uswisi kuja kuwekeza Tanzania kwan fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania ni nyingi.
“Tumepanga kuwekeza katika sekta ya kilimo hasa katika sekta za kilimo hasa katika usindikaji wa mazao ya chakula, biashara na uwekezaji, madini na nishati....tumepanga kufungua kiwanda rasmi hapa Tanzania mwakani,” aliongeza Bw. Barny
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini Switzerland katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Switzerland hapa Nchini, Mhe. Didier Chassot
 

Monday, May 16, 2022​

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E​


Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022.
Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa UAE nchini, Jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula ametoa salamu za pole kwa Serikali ya UAE na kuwasihi wananchi wake kuendelea kuwa watulivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na kiongozi wao.
“Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano, umoja na undugu wetu na ndugu zetu wa UAE. Kifo cha Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kimewagusa pia Watanzania kwa kuwa Tanzania na UAE zina uhusiano mzuri,” alisema Balozi Mulamula.
Aliyekuwa Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan alifariki dunia tarehe 13 Mei, 2022 akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kuugua kwa muda.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), nchini kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo kufuatia kifo cha Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 Mei 2022
 

Thursday, May 12, 2022​

MWAKILISHI MKAZI WA AfDB AWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO​


Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley amewasilisha Barua za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kupokea barua za utambulisho, viongozi hao pamoja na mambo mengine, walijadiliana masuala ya miundombinu endelevu pamoja na uboreshaji wa mazingira katika sekta binafsi.
Bibi. Laverley amemhakikishia Balozi Mulamula ushirikiano wa kutosha kutoka AfDB katika kuchochea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na bank hiyo hapa nchini.
Nae Balozi Mulamula amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini na kuonmgeza kuwa AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania jambo ambalo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na bank hiyo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akipokea barua za utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Source : Habari zote na picha kwa hisani kubwa : Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
 
Waziri Liberata Mulamula yupo na siku chache zilizopita alikuwa na Rais Samia kwenye ziara ya Nchini Uganda na akasaini mikataba kadhaa kwa niaba ya serikali.
Sukuma Gang punguzeni chuki na mnatakiwa kuamini yule bedui ameshakufa na hatorudi tena duniani.
Tatizo mnatembea mkiangalia kivuli cha Magufuli ingawa amekwishafariki.

Mimi nimeulizia kwa sababu kidiplomasia si kitu cha kawaida kumuona rais akiwa ziarani nchi za nje bila waziri husika na mambo ya nje.

Wacheni tuhoji kama nyinyi mnavyokaa mkihoji walipo kina Ndugai na Makonda!

Wewe inakukera nini tukimuulizia mtu ambaye anatumikia serikali tuliyoipigia kura?

Wewe mtumbuliwa endelea kuuguza kidonda cha jipu lako.

Kama una hasira sana na Magufuli,kunywa Sumu umfuate alipo mkamalizane.
 
Tunaomba mwenye kujua nini kilichomsibu waziri wetu.
Atuwekee hadharani, kwa sababu huyu ni kiongozi wa umma na anapaswa kuwepo kwenye eneo lake la kazi kwa mujibu wa sheria na katiba.
'Trivia,' lakini inaweza kuwa na maana kubwa..., mkubwa anafunika kichwa na mabega yote, halafu mdogo ana'contrast' mkubwa kwa kufunua hivyo!

Like I said, it may appear trivial, but carry a huge meaning to some people.
 
Kwa vile kati ya mwaka 2002 na 2004 nilifanya kazi nyingi sana na Pentagon na nilikuwa na marafiki wengi wa ngazi za juu sana, wengi waliamini kuwa Sadam alikuwa na silaha za maangamizi ambazo zingeweza kutumiwa na Al Qaeda dhidi ya marekani ila walikuwa bado wanalifanyia kazi jambo hilo. Tatazo ni kuwa baada ya 9/11wakageuka kuwa katika mode ya kufanya maamuzi ya haraka kuzuia hilo lisotokee. Hata hivyo bado kuna diplomats kadhaa waliojiuzuru, kwa mfano John Brown alijiuzuru kwa kuona kuwa uamuzi huo ulifanyika kwa haraka sana.
EEeeenHeeeee!

Huo mstari wa kwanza unachekesha, (nilitaka kuandika 'unatisha') ,..., John Brown ndiiye nani mkuu?
 
Ajabu, wakati Kabudi anatolewa kwenye uwaziri kisingizio kilikuwa umri mkubwa. Aliyeteuliwa kazaliwa 1956, mwaka ambao ndio Kabudi naye alizaliwa.
Maza Mizinguo huyo, unategemea nini?
Lukuvi na huyo wa Jalalani hawakutenguliwa ili wakajiandae vizuri na kusaka urais 2025?
 
EEeeenHeeeee!

Huo mstari wa kwanza unachekesha, (nilitaka kuandika 'unatisha') ,..., John Brown ndiiye nani mkuu?
Nini kimekuchekesha hapo; ukiwa serious tafuta hapa kwenye posts nyingi nilizowahi kuandika kuhusu research mbalimbali nilizokuwa nafanya na Army Research Lab (ARL) na kila kila mara tukawa tunakutana Virginia ama Pentagon au Crystal City Hotelini kupena progress reports. Hilo ukitaka litafute liko wazi na halihitaji kukuchekesha wala kukutisha; ARL huwa inafanya research kwa kushirikiana na Universities mbalimbali. Labda ulikuwa hujui kuwa jeshi la Marekani hufanya kazi na wataalamu wa kutoka nyanja mbalimbali; wao siyo watu mtutu tu.

Kuhusu swali la pili Kuna diplomats wengi waliojiouzuru baada ya kuona kuwa serikali ilikurupuka sana kuchukua uamuzi wa kuivamia Iraq. John Brown ni mmoja wa madiplomat hao ambaye kujiuzuru kwake kulingazwa sana. Inawezekan ulikuwa hujaanza kufuatilia habari za dunia hivyo humjui.

1653512165265.png
 
Interest gani mkuu za kwenda Madagascar kutuletea dawa feki ya COVID-19 na wakaipiga wenyewe hapo jengo jeupe
Ni kweli; wakati Covid inaanza, kulikuwa na mkanganyiko sana, na hivyo Kabudi akafanya hayo makosa ya kuamini shortcut. Hilo ni kosa lake moja tu kati ya mengi mazuri aliyofanya katika kuproject interests za Tanzania.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akipokea barua za utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za

Huyu Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika nchini Tanzania ndio yule mama aliyempokea Rais Samia kule Accra Ghana!!!
 
Huyu Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika nchini Tanzania ndio yule mama aliyempokea Rais Samia kule Accra Ghana!!!
Inawezekana, lakini huyo Dr. Patricia Laverley ni raia wa Sierra Leone siyo wa Ghana. Inawezekana alimpokea kiundugu kwa vile ameishi sana Tanzania.
 
Inawezekana, lakini huyo Dr. Patricia Laverley ni raia wa Sierra Leone siyo wa Ghana. Inawezekana alimpokea kiundugu kwa vile ameishi sana Tanzania.

Dr. Patricia Laverley amekwenda kumpokea Rais kule kama representative wa African development Bank Tanzania; kumbuka hao African Development Bank ndio walimualika kwenda Ghana kumpatia tunzo!
 
Back
Top Bottom