Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,764
- 13,370
Habari za majukumu wakuu.
Nilikuwa nangalia Azam TV asubuhi hii. Mtangazaji alikwenda stand ya Segerea kuwahoji watumishi wa stand ile.
Miongoni Mwao ni mfanyabiashara mdogo. Kwa mujibu wa mfanyabiashara yule ni kwamba wao walishalipia VITAMBULISHO VYA WAMACHINGA tsh 20000 kwa mwaka.
Hata hivyo cha kushangaza ni kwamba manispaa unaendelea kuwatoza KODI / USHURU kila uchao. Wakiuliza kulikoni wanaambiwa vitambulisho vya Wamachinga pesa yake ilienda serikali kuu na kwamba haihusiani na manispaa.
Unajiuliza maswali.
Je, mbona raisi wa wanyonge alisema hakuna kuwabughudhi Wamachinga baada ya kulipa ile 20000/ na tena akasema vitambulisho vitatumika hata kwa matibabu?
Tofauti kati ya kodi za manispaa na serikali kuu ni nini na kwanini mtu mmoja tena nyongeza kama anavyoitwa alipe kodi mara mbili?
Uko wapi ule msimamo kwamba Wamachinga akilipa kodi na kupata vitambulisho mpaka mwakani?
Tulidanganywa kwenye kampeni? Kwanini?
Chanzo: Azam TV morning trumpet