Vitambulisho vya Wamachinga

FROWIN

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
213
84
Leo nimepita maeneo flani nimekuta kuna mtu wa kutoka Manispaa akitangaza kwamba wamachinga na wajasiliamali wote wanapaswa kwenda ofisi za mtendaji kwa ajili ya kupata vitambulisho vya ulipaji kodi ,Tangazo linawataka Mafundi kushona ,Wabeba makapu ya ndizi mitaani na mafundi selemala wote inatakiwa wakachukue vitambulisho kwa gharama ya Tsh 20000 ,sina shaka na hili zoezi kwa sababu kama wafanya biashara wadogo wanapashwa kulipa kodi kidogo iwezekanavyo,ila shida yangu ni kwamba Mama aliyebeba ndizi zenye thamani ya Tsh 3000 anawezaje kulipia kitambulisho cha Tsh 20000?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitamburika rasmi manake utakuwa una weza kufanya biashara popote palipo rasmi 20000 kwa mwaka kwa mfanya biashara ata ya 2000 ana weza kuimudu na itaongeza tija kwenye biashara ukichukua elfu 20000 ukagawa kwa mwaka 365 ni sawa kwa siku ni shilingi 54
 
Back
Top Bottom