Kulikoni Polepole kukaa kimya sakata la CAG?

Sasa hiyo CCM imuelekeze speaker Job Ndugai awarudishe waheshimiwa Halima Mdee na Godbless Lema, waliomuunga mkono CAG Prof Mussa Assad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nimeelewa naongozwa na mbunge mjinga,asie na mimi mwananhi,anawaza masilahi ya chama,akigombea tena simchagui tena!
 
Safi sana, ila kwa taharifa yako mahakama ya mafisadi iko kwa ajili ya kuwakomoa mahasimu wake mkuu and not otherwise, hili la CAG in sindano ilowachoma sawasawa makalio yao.
Waako wapi...
Polepole.
Bashuru ally.
Kibajaji.
Kitila mkumbo.
Na makapi mengine yanayosifiasifia mda wote bila kutumia akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aseme nini tena huyu mzee kijana? Kashachoka kujitoa ufahamu.
 
Chakubanga ni mtaalamu wa sanaa za maigizo kuliko Lowassa aliyezisomea kiwango cha shahada ya chuo kikuu; yuko chimboni aka "War room" anachonga maumbo na ngonjera ili akiibuka ang'are ng'ari ng'ari! subiri uone.
 
Kama ilivyo kawaida ya Chama Cha Mapinduzi kutolea ufafanuzi wa mambo baada ya ripoti ya CAG.

Mwaka Jana Ndugu Humphrey Polepole, Katibu Mwenezi wa CCM alitolea ufafanuzi upotevu wa 1.5T na somo lililieleweka na Watanzania wengi (Pongezi Kwa Polepole)

Swali langu ni Lini Polepole atatupa darasa murua la hisabati kutumia njia zake pendwa za MAGAZIJUTO kutolea ufafanuzi upotevu wa Trillions na Billions kadhaa kama ilivyoelekezwa na Ripoti ya CAG?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa nasikia anagonga mvinyo sana, ngoja akikaa vizuri atatupa nondo zake.
 
ila siyo Siri CCM Kuna watu wa Ajabu.

Nasikia,zile calculation zilifanya atunukiwe PhD

ila now yupo na jopo la ma CAG wa lumumba wanataka kupika kitu,ambacho akitoka hapo,Moja kwa Moja atakuwa Professor wa CAG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
,kimya kinamaanisha kukubaliana na tuhuma
 
... yuko chimbo ana andaa somo Mkuu. Akiibuka, atairarua vibaya ripoti ya CAG huku 93% ya wanyonge wakiichanachana ripoti ya CAG na kuomba kibali cha maandamano kuunga mkono juhudi na kulaani ripoti ya kichochezi!
 
Jamaa nasikia anagonga mvinyo sana, ngoja akikaa vizuri atatupa nondo zake.
Nilidhani jamaa aliyenidokeza mwongo! Kumbe wengi wana hii taarifa, anyway acha wanywe huenda wataharakisha ule mpango wa kurasimisha gongo.
 
Hana darasa anahitaji darasa PhD aliyookota dampo ni feki ndo maana ilitupwa na aliyeipata Manzese University.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…