KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,221
- 5,450
" si haki kukilaumu chama au Serikali kwamba havifanyi kazi zake barabara kwa kosa ambalo limefanywa na kiongozi mmoja wa Chama au wa Serikali au wa shirika la Umma". Edward Sokoine, Oktoba 12, 1983.CcM hawawezi kujisafisha na kashfa hizi za wizi kwenye ripoti ya CAG.Wao ndio waliounda Serikali,sasa asije kutuhadaa kwamba CcM haihusiki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kapigwa ganzi na ujio wa Lowassa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Katika sakata la 1.5 Trillion Polepole alijitokeza kwa ushujaa kufundisha taifa hesabu na kuonyesha hakuna fedha imepotea.
Polepole ni katika watu walio mstari wa mbele kuunga lolote lifanywalo na Rais hata kama halina maslahi kwa nchi.
Lakini kabla ya haya yote, kabla ya Polepole kupata vyeo CCM alikuwa kijana mahiri mwenye kulitetea taifa na kusimamia maslahi ya taifa na alivuma sana kipindi cha katiba mpya.
Kimya chake cha ghafla baada ya watu kuanza kumuandama mitandaoni Je kuna jambo kashtukia sivyo alivyotegemea au kashaona muelekeo mbaya wa taifa na anaanza kujitoa taratibu na kukabidhi kazi kwa akina Musiba.
Polepole tumjuae asingeacha ripoti ya CAG imchafue Magufuli lazima lawama zingepelekwa kuwa kuna vibaraka wa mabeberu.
Je, nini kimemsibu?
Alipo anzisha mahakama ya mafisadi, aliamini kuwa ufisadi unafanywa na wapinzani hasa baada ya mamvi kuhamia upinzani. Amekuja kugundua kwamba unafanywa na wanaCCM hasa wasaidizi wake anao waamini sana, mahakama haina kazi tena. Kilangila.nimeguswa na hii mada kwa maswali lukuki kuwa je ni huyu mzee kijana tu alie kimya wakati huu? je kwanini yuko kimya? yupo ofisini? busy? lakini mbona na wakubwa zake pia nao kama wamemwagiwa maji wako kimyaaa, ripoti hii imetaja mafisadi wote ofisi walipo na kiasi walichoiba, ni aibu sana kwa nchi na serikali kwa ufisadi huu wa kutisha uliofanyika na wenye ushahidi, je mahakama ya mafisadi ofisi zao ziko wazi au wapo likizo? je kwanini hawaanzi kukamata na kuwahoji wahusika wote simply kuanzia na all budget holders na signatories wa kila wizi ulioandikwa na CAG, ni aibu na kichekesho kikuu kusema serikali inapambana na ufisadi na kuwaacha mafisadi wenye ushahidi wakidunda mitaani , shime sana mahakama ya mafisadi ifanye kazi yake sasa kuwakamata mafsadi wote walioainishwa kwenye ripoti ya CAG , ni bora tutafute kauli mbiu ingine!!
Duuhhh, kwa hiyo wabunge wa CCM na CCM kwa ujumla imempuuza speaker Job Ndugai. Hivi waliopitisha Azimio la kumkataa CAG wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje walikua wabunge wa chama gani!!??? Mkuu nadhani hapa umetupia tu ili uone watu wanasemaje. This is a joke kiongozi. CCM hoyeeeeeee.Chama Cha Taifa CCM kipo Pamoja Na CAG
CCM ndio imeamuru Wabunge wake wapuuze Azimio la Bunge la kumsusia CAG
Duuhhh, kwa hiyo wabunge wa CCM na CCM kwa ujumla imempuuza speaker Job Ndugai. Hivi waliopitisha Azimio la kumkataa CAG wakati wabunge wa upinzani wakitoka nje walikua wabunge wa chama gani!!??? Mkuu nadhani hapa umetupia tu ili uone watu wanasemaje. This is a joke kiongozi. CCM hoyeeeeeee.
Sent using Jamii Forums mobile app
Anaweza maana ndugai haoni mbeleMfupa uliomshinda Ndungai, Polepole atauweza?
bado yuko bize anafanya yale mahesabu yake ya kukokotoa ili atoke vizuriKatika sakata la 1.5 Trillion Polepole alijitokeza kwa ushujaa kufundisha taifa hesabu na kuonyesha hakuna fedha imepotea.
Polepole ni katika watu walio mstari wa mbele kuunga lolote lifanywalo na Rais hata kama halina maslahi kwa nchi.
Lakini kabla ya haya yote, kabla ya Polepole kupata vyeo CCM alikuwa kijana mahiri mwenye kulitetea taifa na kusimamia maslahi ya taifa na alivuma sana kipindi cha katiba mpya.
Kimya chake cha ghafla baada ya watu kuanza kumuandama mitandaoni Je kuna jambo kashtukia sivyo alivyotegemea au kashaona muelekeo mbaya wa taifa na anaanza kujitoa taratibu na kukabidhi kazi kwa akina Musiba.
Polepole tumjuae asingeacha ripoti ya CAG imchafue Magufuli lazima lawama zingepelekwa kuwa kuna vibaraka wa mabeberu.
Je, nini kimemsibu?
Mhu mbona sijaagiza wine saa hivi, hivi huyu ni Pohamba au amedukuliwa? Yaliyopo yanashangaza.Chama Cha Taifa CCM kipo Pamoja Na CAG
CCM ndio imeamuru Wabunge wake wapuuze Azimio la Bunge la kumsusia CAG
Kwani nani aliyetoa azimio la kutofanya kazi na CAG? Vibaraka mnapata tabu sana kutetea ujingaChama Cha Taifa CCM kipo Pamoja Na CAG
CCM ndio imeamuru Wabunge wake wapuuze Azimio la Bunge la kumsusia CAG
Wabunge wa CCM hawakukutana Kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM kupata ridhaa ya Chama kwa Azimio Hilo
Walikurupuka ndio sababu Chama kimewaamuru kutupilia mbali Azimio linalovunja Katiba
CCM ipo kusimamia Na kuelekeza Wabunge wake sio Wabunge kuelekeza CCM
SwadaktaBado anamalizia kuandaa ' Propaganda ' itakayobadili upepo wote wa ' Sakata ' zima. Vuta subira!
Mkuu, twende taratibu. Baada ya kamati kumhoji CAG na kutoka na Azimio la kumkataa ambalo kiukweli lilishakua limeandalia na Job Ndugai kabla hata ya CAG kuhojiwa, kamati ilileta mapendekezo yaliyo kwenye Azimio ndani ya Bunge kuungwa au kukataliwa na wabunge. Utakumbuka wabunge wa upinzani walilipinga hilo Azimio na baada ya hoja za mh Lema kulipinga kwa nguvu na kumuunga mkono mh Mdee juu ya hoja ya kukubaliana na CAG ambayo maana yake Lema pia alikubaliana na hoja za CAG, speaker alimtoa mh Lema nje ya Bunge na baada ya hapo wabunge wa upinzani walitoka kumuunga mkono Lema.Wabunge wa CCM hawakukutana Kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM kupata ridhaa ya Chama kwa Azimio Hilo
Walikurupuka ndio sababu Chama kimewaamuru kutupilia mbali Azimio linalovunja Katiba
CCM ipo kusimamia Na kuelekeza Wabunge wake sio Wabunge kuelekeza CCM