Lemme shooting off the hip, according to credible sources.
Jumbe alitaka kuvunja muungano, wakati huo Seif Sharif Hamad Waziri kiongozi Zanzibar. Hamad aliposikia habari hizi akamtonya Nyerere, wakamtumia katibu muhtasi wa Jumbe kuiba makaratasi ambayo Jumbe angeyatumia kuuvunja muungano, yakiwamo yale ya kuupitia muungano kwa review kila miaka 10. Na hati nyingine za muungano ambazo Wazanzibari mpaka leo wanazidai. Inasemekana hizi hati zilipochukuliwa na Nyerere hazikurudishwa Zanzibar mpaka Nyerere alipofariki. Wengine wanasema hii ni siri kali kati ya Nyerere na Hamad, na pengine katibu muhtasi huyu ambaye anaonekana amenyamazishwa (na labda hakujua hata umuhimu wa makaratasi haya) sijui kama yuko hai bado .
Ndiyo maana mpaka Nyerere anafariki, na hata baada ya Seif Sharif Hamad kuingia upinzani. Nyerere na Hamad walikuwa wanateta, na kuna mengine Nyerere kaenda nayo kaburini na Hamad mpaka leo hataki kusema alipokuwa anateta na Nyerere walikuwa wanaongea nini. Wametoka mbali.
Nyerere alipopata vielelezo vyote akamlazimisha Jumbe ajiuzulu, kukatangazwa "mchafuko wa hali ya hewa ya kisiasa" Zanzibar. Nyerere akamchagua Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar, balozi Ali Hassan Mwinyi (no relation), kuwa "rais wa muda" wa Zanzibar na hivyo makamu wa rais. Watu wa usalama kama kina Mashiba wakatuambia "vijana huyu Mwinyi ndiye atakuwa rais baada ya Nyerere". Tukaona kama utani vile.
Baadaye marehemu Maneti (pamoja na wengine wengi) akaimba "Ali Mwinyi, Ali Mwinyi, Ndiyo, Ndiyo, Ndiyo". The rest is much documented in Tanzanian history.
Hivi ndivyo Jumbe alivyoanguka na Mwinyi kupanda.
Makamu mwingine wa rais aliyekuwa anaandaliwa kwa urais alikuwa daktari wa mifugo Omar Ali Juma, yeye anguko lake la umauti lilitokana na kuchanganya Viagra na kahawa- a deadly combination-, kitu ambacho kama mtaalamu wa mambo ya baiolojia angetakiwa kukijua. Mkapa hakupenda Kikwete awe rais na alikuwa anamuandaa Dr. Omar kuchukua urais, kwa mujibu wa watu wa familia ya Mkapa waliokuwa wanaishi naye Ikulu na Sea View. Ila Viagra ambayo Makamu wa rais aliiongezea kahawa - a deadly combination- ikakatili ndoto hizi na kufanya nyota ya Kikwete iendelee kung'ara.
I don't know which is worse, a Kikwete presidency or a Juma presidency.